sexologist
JF-Expert Member
- Dec 5, 2010
- 2,283
- 976
Nimetafakari na kufanya uchunguzi kidogo..
Escrow ni mchezo uliopangwa kwa ustadi mkubwa sana ili kuiangusha CCM, utaligundua hilo ukisoma vizuri ripoti ya CAG na PAC.. Ni mchezo uliolenga viongozi wapenzi wa Kikwete na ambao wana kiburi sana nchini na wanashindwa kuguswa kwa mgongo wa Rais..
Ni wazi Rais anampenda na kumkubali sana Mh. Muhongo, ni wazi anamkubali mama Tibaijuka, ni wazi Maswi ni chaguo lake.. Sasa hii ripoti ikaenda kugusa wizara nyeti ambayo ndio viongozi wanapigia hela ndefu kabisa. Ni ngumu kufanya maamuzi.
Sasa washauri wa Rais wamemdanganya muheshimiwa na kufikia hatua ya kushindwa kufanya maamuzi kwa wakati.. Kitendo cha kuahidi kufanya maamuzi baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa itakuwa pigo sana kwa CCM.. Utafiti wangu unaonesha sasa upinzani unakubalika zaidi mitaani na vijijini zaidi kwa turufu ya ESCROW.. Ni matarajio yangu kura nyingi zitaenda upinzani uchaguzi huu kwa asilimia 60. Au zaidi.
Sababu watu hawana imani na CCM hasa baada ya kushindwa kufanya maamuzi juu ya ESCROW na kuaminika kwamba CCM wanaunga mkono ufisadi..
Nawasilisha.