Mh. Rais shtuka mapema, hapo umechezewa akili wewe na chama chako

Nimetafakari na kufanya uchunguzi kidogo..

Escrow ni mchezo uliopangwa kwa ustadi mkubwa sana ili kuiangusha CCM, utaligundua hilo ukisoma vizuri ripoti ya CAG na PAC.. Ni mchezo uliolenga viongozi wapenzi wa Kikwete na ambao wana kiburi sana nchini na wanashindwa kuguswa kwa mgongo wa Rais..

Ni wazi Rais anampenda na kumkubali sana Mh. Muhongo, ni wazi anamkubali mama Tibaijuka, ni wazi Maswi ni chaguo lake.. Sasa hii ripoti ikaenda kugusa wizara nyeti ambayo ndio viongozi wanapigia hela ndefu kabisa. Ni ngumu kufanya maamuzi.

Sasa washauri wa Rais wamemdanganya muheshimiwa na kufikia hatua ya kushindwa kufanya maamuzi kwa wakati.. Kitendo cha kuahidi kufanya maamuzi baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa itakuwa pigo sana kwa CCM.. Utafiti wangu unaonesha sasa upinzani unakubalika zaidi mitaani na vijijini zaidi kwa turufu ya ESCROW.. Ni matarajio yangu kura nyingi zitaenda upinzani uchaguzi huu kwa asilimia 60. Au zaidi.

Sababu watu hawana imani na CCM hasa baada ya kushindwa kufanya maamuzi juu ya ESCROW na kuaminika kwamba CCM wanaunga mkono ufisadi..

Nawasilisha.

JK hana mpango wa kufanya mabadiliko kwa mujibu wa matakwa ya wawakilishi wa wananchi ndio maana anaona bora damage ndogo hii ya kuhusika kwake na wapendwa wake ipite na uchaguzi wa serikali za mtaa kuliko akitangaza msimamo wake maana utaleta damages kubwa zidi kuliko ilivyo sasa.
 
Mengi yatasemwa lakini ukweli utabaki pale pale kuwa ESCROW ilikuwa ni kwa ajili wa Muhongo na MASWI, na mfadhili mkubwa ni Reginald Mengi

Hivi sasa Mengi na Mkono wajitapa na bado watatujua sisi ni nani. Hivi kweli wafanyabiashara ndiyo wanaoiongoza nchi hii, serikali iwe makini na watu hawa maana inaonekana ndio wanapanga Rais awe na nani na mawaziri wawe akina nani nakama hawatawapenda au wakiona hawako kwa ajili ya maslahi yao watafanya juu chini watolewe ndio haya tunayaona sasa.
 
Huyu mleta mada anamatatizo makubwa kichwani mwake mengi kashindwa kupenyeza ujinga wake hata hawa anaowatuma watakwama tu huwezi kumuonea mtu kizembe kiasi hiki.

Think twice.. Angalia dhima ya mada kama kuna sehemu ametajwa Mengi.. Na usihisi, Mengi na Escrow wapi na wapi wapi?? Mi sio msukule kama wewe unapewa cheo kwa fadhila za marehemu.. Poole mkuu!
 
Nimetafakari na kufanya uchunguzi kidogo..

Escrow ni mchezo uliopangwa kwa ustadi mkubwa sana ili kuiangusha CCM, utaligundua hilo ukisoma vizuri ripoti ya CAG na PAC.. Ni mchezo uliolenga viongozi wapenzi wa Kikwete na ambao wana kiburi sana nchini na wanashindwa kuguswa kwa mgongo wa Rais..

Ni wazi Rais anampenda na kumkubali sana Mh. Muhongo, ni wazi anamkubali mama Tibaijuka, ni wazi Maswi ni chaguo lake.. Sasa hii ripoti ikaenda kugusa wizara nyeti ambayo ndio viongozi wanapigia hela ndefu kabisa. Ni ngumu kufanya maamuzi.

Sasa washauri wa Rais wamemdanganya muheshimiwa na kufikia hatua ya kushindwa kufanya maamuzi kwa wakati.. Kitendo cha kuahidi kufanya maamuzi baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa itakuwa pigo sana kwa CCM.. Utafiti wangu unaonesha sasa upinzani unakubalika zaidi mitaani na vijijini zaidi kwa turufu ya ESCROW.. Ni matarajio yangu kura nyingi zitaenda upinzani uchaguzi huu kwa asilimia 60. Au zaidi.

Sababu watu hawana imani na CCM hasa baada ya kushindwa kufanya maamuzi juu ya ESCROW na kuaminika kwamba CCM wanaunga mkono ufisadi..

Nawasilisha.

Hivi wewe bado unaitetea CCM tu, huchoki?...
 
Duniani kote ni ccm pekee na serikali yake ina uwezo wa kumtetea mhalifu mkubwa kama Muhongo. Misaada hakuna watu hawana fedha, mahospitali hoi na hapo ni cha mtoyo tu bado muziki wake haujakolea.

Juzi China Waziri kahukumia kifungo cha maisha kwa wizi mdogo tu
 
Back
Top Bottom