Mh. Rais shtuka mapema, hapo umechezewa akili wewe na chama chako

sexologist

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
2,289
1,195
Nimetafakari na kufanya uchunguzi kidogo..

Escrow ni mchezo uliopangwa kwa ustadi mkubwa sana ili kuiangusha CCM, utaligundua hilo ukisoma vizuri ripoti ya CAG na PAC.. Ni mchezo uliolenga viongozi wapenzi wa Kikwete na ambao wana kiburi sana nchini na wanashindwa kuguswa kwa mgongo wa Rais..

Ni wazi Rais anampenda na kumkubali sana Mh. Muhongo, ni wazi anamkubali mama Tibaijuka, ni wazi Maswi ni chaguo lake.. Sasa hii ripoti ikaenda kugusa wizara nyeti ambayo ndio viongozi wanapigia hela ndefu kabisa. Ni ngumu kufanya maamuzi.

Sasa washauri wa Rais wamemdanganya muheshimiwa na kufikia hatua ya kushindwa kufanya maamuzi kwa wakati.. Kitendo cha kuahidi kufanya maamuzi baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa itakuwa pigo sana kwa CCM.. Utafiti wangu unaonesha sasa upinzani unakubalika zaidi mitaani na vijijini zaidi kwa turufu ya ESCROW.. Ni matarajio yangu kura nyingi zitaenda upinzani uchaguzi huu kwa asilimia 60. Au zaidi.

Sababu watu hawana imani na CCM hasa baada ya kushindwa kufanya maamuzi juu ya ESCROW na kuaminika kwamba CCM wanaunga mkono ufisadi..

Nawasilisha.
 

Nyanya mbichi

JF-Expert Member
Nov 10, 2011
3,612
2,000
Eti rais kadanganywa na wasaidizi wake??? Kauli ya kuujipendekeza wewe ni mmoja wapo.wewe ujue rais kadanganywa yeye mwenyewe asijue hadi leo kuwa anadanganywa tu???

Mimi mwenyewe hii ngonjera naiona ni ya kinafki tu
 

Cybercrime

JF-Expert Member
Feb 14, 2014
3,248
2,000
Mengi yatasemwa lakini ukweli utabaki pale pale kuwa ESCROW ilikuwa ni kwa ajili wa Muhongo na MASWI, na mfadhili mkubwa ni Reginald Mengi
 

nkongu ndasu

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
22,524
2,000
Rais hajadanganywa, bali yeye ndo muhusika, kwa hiyo anamwandaa kisaikolojia wa kutolewa kafara!
 

nkongu ndasu

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
22,524
2,000
Mengi yatasemwa lakini ukweli utabaki pale pale kuwa ESCROW ilikuwa ni kwa ajili wa Muhongo na MASWI, na mfadhili mkubwa ni Reginald Mengi
teh teh, kwa hiyo mengi alifanya mpango wa mafisadi kwenda kuchota mabilioni pale stanbic kwenye sandarusi na viloba? Hii akili ya kushikiwa ni mbaya sana!
 

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
18,939
2,000
Huwezi kuwajibisha watu kwa fitina bana kila kitu lazima kwanza tupate wahusika siyo fitina tu mtu anaadanishwa hiyo nchi gani.
 

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
18,939
2,000
Hakuna hata sehemu moja ripoti zote za PCCB, CAG na PAC zimemgusa Rais , wewe haya unayatoa wapi?
Huyu mleta mada anamatatizo makubwa kichwani mwake mengi kashindwa kupenyeza ujinga wake hata hawa anaowatuma watakwama tu huwezi kumuonea mtu kizembe kiasi hiki.
 

nkongu ndasu

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
22,524
2,000
Hakuna hata sehemu moja ripoti zote za PCCB, CAG na PAC zimemgusa Rais , wewe haya unayatoa wapi?
fuatilia vizuri, na utagundua nani aliidhinisha malipo ya escrow yafanyike! Katika jambo hili ikulu ilihusika kwa 100%, unadhani kigugumizi cha jk ni nin? Za kuambiwa changanya na zako..
 

Jagarld

JF-Expert Member
Apr 7, 2011
1,993
2,000
Yaani wewe umwambie ashtuke aliyeagiza na kuyapokea mafurushi kutoka stanbic au yeye ndo akushtue kwamba unachowaza hakipo...!
 

gollocko

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
2,950
2,000
Huyu raisi kibila siku anadanganywa na hwawajibishi wanaomdangaya, inaelekea anapenda kudanganywa
 

nkongu ndasu

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
22,524
2,000
Huyu mleta mada anamatatizo makubwa kichwani mwake mengi kashindwa kupenyeza ujinga wake hata hawa anaowatuma watakwama tu huwezi kumuonea mtu kizembe kiasi hiki.
mengi ndo aliowatuma kina chenge na tibaijuka wakachote milioni 1600 pale mkombozi benki?
 

Jagarld

JF-Expert Member
Apr 7, 2011
1,993
2,000
Yaani wewe umwambie ashtuke aliyeagiza na kuyapokea mafurushi kutoka stanbic au yeye ndo akushtue kwamba unachowaza hakipo...!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom