mcfm40
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 4,452
- 3,150
Katika vyombo vya habari leo umesikika ukihimiza watanzania watunze amani na mshikamano ulipokuwa makanisani na misikitini huko Chato.
Lakini Mh pamoja na umuhimu wa kusisitiza swala amani, usisahau kuwa amani ni tunda la haki! Bila haki amani ya kweli ni ndoto. Haki na Amani ni maneno pacha. Huwexi kuzungumzia amani bila kuzungumzia na kusisitiza haki.
Watawala mnaogopa sana kutaja neno haki katika hotuba zenu kwa sababu mnajua haki ni gjarama na wengi hampo tayari kuongoza kwa haki!
Mh ni contradiction na unafiq kuhubiri amani kanisani na misikitini huku unabinya haki na uhuru wetu wa kidemokrasia.
Wewe unajipendelea kufanya mikutano na kuimarisha chama chako nchi nzima huku ukitumia vibaya vyombo vya dola kuwazuia washindani wako nao wafanye mikutano ya kuimarisha vyama vyao. Kumbuka hii ni nchi inayofuata misingi ya demokradia ya vyama vingi.
Kwa mtindo huu Mh ujue unapandikiza mbegu ya uasi katika nchi. Ukiminya haki za kikatiba za washindani wako watazitafuta kwa njia nyingine ambazo zinaweza kuwa na madhara! Na kuhubiri amani misikitini na makanisani haitasaidia km wewe mwenyewe hufuati misingi ya amani ambayo ni kuiheshimu katiba na sheria tulizojiwekea katika kuendesha nchi!
Hivyo mh nakusihi urudie mara kwa mara hii sentensi na uikariri na kuiishi katika uongozi wako (si utawala) kama kweli unataka kuliongoza hili taifa kwa mafanikio. "Amani ni tunda la haki." Hii iwe sala na dua yako kila ulalapo na uamkapo! Asante!