Shebbydo
JF-Expert Member
- Feb 12, 2015
- 1,174
- 1,937
JHabari wana JF,
Mh. Rais hii ni kauli yako ambayo naweza kudiriki kuiita dira yako kwa kuwa umekuwa ukiitoa tangu kipindi cha kampeni, "Tanzania ya Magufuli ni Tanzania ya viwanda". Hakika ni jambo jema sana ambalo Watanzania tunatamani litokee katika nchi hii, kama ingewezekana kulala kesho yake tukakuta viwanda vimejijenga vyenyewe tungejua sasa matatizo yetu yamepungua kama si kuisha kabisa.
Kwanza kabisa tungejua matatizo ya ukosefu wa ajira yatapungua kwa kuwa viwanda ni sekta ambayo inaajili watu wengi, ikiwa ni wataalamu, mafundi wa kawaida na vibarua mbalimbali kwa ajili ya uendeshaji wa kiwanda husika. Pia bidhaa zake zingeleta unafuu wa bei kutokana na kuzalishwa hapa nchini, hali kadhalika tungeongeza fedha za kigeni kama viwanda hivyo vingezalisha pia bidhaa za kuuza nje.
Lakini Mh. Rais, viwanda ni mchakato. Mchakato huu unaanza kwa kufahamu kwanza ni viwanda vya aina gani tutakuwa navyo, mali ghafi za viwanda zitapatikana vipi, Wananchi wameandaliwa vipi hili kushiriki katika uchumi huo wa viwanda.
Nikianza na viwanda ni vya aina gani;
Mh. Rais nimekusikia mara nyingi kuwa viwanda hivi tunategemea sekta binafsi, hasa wawekezaji wa ndani na wa nje ndiyo wategemewa wakubwa. Mimi huwa najiuliza, kama ni viwanda vya kusindika mazao ya baharini, je Wananchi wameandaliwa kikamilifu kushiriki katika uzalishaji wa bidhaa hizo? Kwa maana kwamba kama ni samaki basi, wafanye uvuvi wenye tija ili kuleta hizo mali ghafi za viwandani au watabaki kuwa watazamaji katika nchi yao huku wawekezaji wakifanya shughuli zote za kutafuta mali ghafi, kuzalisha na kuuza?
Mh. Rais kama ni viwanda vinavyotegemea bidhaa za kilimo, je Watanzania wamewezeshwa je katika kilimo kinachohitajika kuzalisha mali ghafi za viwandani? Kamwe hutowatoa Watanzania kwenye dimbwi la umasikini kama watakuwa manamba katika mashamba ya wawekezaji kwani ujira wao utakuwa ni wa kukidhi mahitaji tena siyo yote, hivyo hata kuwa na ziada itakuwa ndoto.
Mh. Rais Mainjinia na mafundi mchundo viwandani wanahitajika. Tunawaandaa je vijana ambao ndiyo watakaokuja kuwa mainjinia na mafundi mchundo huko viwandani? Au tutabaki kuwaangalia wawekezaji wakija na wataalam wao kutoka huko watokako kwa kuwa sisi hata hawa wachache tulionao hawana uwezo kwa kutafsiri nadharia walizosoma darasani kutokana na mazingira ya kujifunzia kwa vitendo kuwa duni? Mh. Rais ni vyuo vingapi vinavyotoa kozi zinazotoa wataalam wa viwandani kama chuo kikuu kikubwa ambacho kinadahili wanafunzi wengi cha UDOM hakina mechanical engineering, electrical engineering, food processing engineering na nyingine nyingi zinazohusiana na uzalishaji viwandani?
Mh. Rais nasikia serikali yako inang'ang'ana na kupunguza idadi ya wanafunzi watakaodahiliwa chuo kikuu bila kuangalia dira yako kuwa watahitajika sana watu wa aina gani katika huo uchumi wa viwanda, kwa kigezo cha kuongeza ubora wa elimu kwa kudahili waliopata daraja la kwanza na la pili kidato cha sita. Hivi kweli ubora wa elimu hupimwa kwa idadi ndogo ya watu wanaohitimu vyuoni au ni kwa kuangalia uwezo wa wahitimu kutafsiri kile walichojifunza darasani? Je, ni kweli wahitimu hawa wameshindwa kutafsiri nadharia ya darasani kwa vitendo eti kwa sababu tu walienda vyuoni na daraja la chini? Au ni kukosekana kwa mazingira bora ya kujifunzia hivyo vitendo, na kama yakiwepo basi ni yale ya karne iliyopita?
Mh. Rais kama kweli una nia ya dhati ya kutufikisha katika nchi ya viwanda basi andaa barabara ya kutufikisha huko na si wewe mwenyewe tu kuwa na ndoto ambayo wengi tumeshindwa kuitafsiri.