Mh. Rais, naomba Prof. Prosper Ngowi mteue awe Mshauri wako wa Uchumi

bigmind

JF-Expert Member
Oct 28, 2015
12,457
12,682
Mheshimiwa rais wangu John Joseph Pombe Magufuri kwa heshima na tahadhima nikuombe umteue huyu Prof. PROSPER NGOWI awe mshauri wako wa mambo ya uchumi.

Binafsi nijitambulishe kuwa huyu Prof. Anijui na pia hatujawahi kukutana wala kuzungumza, kila nimemfuatilia katika maandiko yake na Vipindi vyake katika TV has a ITV huyu Prof. Siyo mtu wa kisipoti kisipoti kiukweli. Akifanya uchambuzi wa angle fulani ya uchumi ni MTU mwenye wivu tu ndiyo hatamkubali.

Mh. Rais nikuombe kiukweli kuendelea kumwacha nje ya wapanga maendeleo ya nchi huyu jamaa kwanza yeye binafsi humtendei haki lakini pia Tanzania kama taifa linalohitaji wataalam hasa kama hawa wa uchumi utakuwa ulitendei hali. Wito wangu kwako Mh. Rais jenga utaratibu wa kuwatumia Sana hasa watu kwenye uwezo binafsi.

Nategemea iwapo utasoma bandiko hili Mh. Raid utafanyia kazi ushauri huu.

ASANTENI

Mtaalam huyu wa uchumi ni mtu ambaye serekali hii ya awamu ya tano inapaswa kumtumia vizuri nadhani vyema hata ushauri wake ukitumiwa na benki kuu unaweza kuimarisha thamani ya shilingi maana imekuwa ikidorora kila siku. Wanasiasa mtumieni mtaalam huyu

Jamaa yuko vzur sana kichwan aliwahi kunifundisha...anatumiwa na taasisi za nje

Mchawi mpe mwanao akulele....ila sio kwa wasomi wa bongo hii prof lipumba, nikimuona na mpango alivyo nakataa tamaa kabisa bora ushauri atoe kibajaji au maji marefu tunaweza piga hatua

Wasomi wetu wamekuwa misukule ya wanasiasa....taaluma zao wameziweka kando wamekuwa wachumia tumbo.....

Wanasiasa wetu nao vichwa vigumu...wanajiona wanajua kila kitu...hawashauriki.....

Kwao kupokea ushauri hasa kutoka upinzani ni sawa na kujivua nguo.....hawajui kuwa taifa ni letu sote haijalishi mtu upo chama gani.....

Wasomi wetu wasimame kwenye mstatiri wasimamie kile wanachokiamini kuwa ni sahihi na sio kuwa mavuvuzela ya watawala.....

Leo hii ukisikia hotuba za wasomi wanaojiita wamebobea kwenye fani mbali mbali.....mpaka unapata woga kumlipia ada mwanao.......

well said.............umesema bonge la fact. Kiukweli jamaa inabidi wajifunze kuwa sisi kama binadamu tunatakiwa kushirikiana maana ajenda ni maendeleo ya taifa si swala au ajenda ya mtu au kikundi cha watu fulani...................kwanini sijui hatujifunzi hiki kitu

ni raid au raisi maana umeandika mara ya kwanza nikajua umekosea kwa bahati mbaya ila

mara ya pili ukakosea tena nikavumilia mara ya tatu ukapatia vizur kwa ufasah ya nne ukakosea

embu niweke wazi labda sifaham ni raid au raisi

Mkuu unaweza ukawa una wazo zuri, lakini usichokijua ni kama usiku wa giza, prof. Ngowi ni one in thousands...
Hii nchi toka nyerere atoke madarakani haijawah heshim wasomi na taaluma zao....

Hujaona namna RC anavyomvimbishia kifua DMO, au Afisa ardhi, au hata kuwadharau hadharani?

Mheshimiwa raid wangu John Joseph Pombe Magufuri kwa heshima na tahadhima nikuombe umteue huyu Prof. PROSPER NGOI awe mshauri wako wa mambo ya uchumi.

Binafsi nijitambulishe kuwa huyu Prof. Anijui na pia hatujawahi kukutana wala kuzungumza, kila nimemfuatilia katika maandiko yake na Vipindi vyake katika TV has a ITV huyu Prof. Siyo mtu wa kisipoti kisipoti kiukweli. Akifanya uchambuzi wa angle fulani ya uchumi ni MTU mwenye wivu tu ndiyo hatamkubali.

Mh. Raid nikuombe kiukweli kuendelea kumwacha nje ya wapanga maendeleo ya nchi huyu jamaa kwanza yeye binafsi humtendei haki lakini pia Tanzania kama taifa linalohitaji wataalam hasa kama hawa wa uchumi utakuwa ulitendei hali. Wito wangu kwako Mh. Rais jenga utaratibu wa kuwatumia Sana hasa watu kwenye uwezo binafsi.

Nategemea iwapo utasoma bandiko hili Mh. Raid utafanyia kazi ushauri huu.

ASANTENI. NAWASILISHA.
ACHA KUHARIBU MAJINA YA WATU:
huyu anaitwa Profesa Prosper NGOWI

Unataka kutwambia Charles Hilary ni mchezaji mzuri kama Messi?

Uchambuzi na reality ni vitu viwili tofauti, like chalk & cheese! Mwalimu wangu aliyenisomesha kwa nini ndege inaweza kuruka, hawezi hata kubadilisha fan belt ya gari! And he was a damn good teacher.
Mkuu anaongoza mradi mikubwa ndani na nje ya nchi km consultant.

Back
Top Bottom