Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,409
- 13,259
Mh. Rais tufike mahali tujiulize ni nani anauhitaji mwenge kwa sasa hivi, je ni serikali au wananchi? Tukipata jibu basi tukubaliane huyo anayeuhitaji ndiye augharimie mbio zake na sio kwenda kuwabandika watu michango wakati huu wa hali ngumu ya maisha. Kila mkurugenzi anapotaka michango wanyonge wake wa kwanza ni walimu. Baadae wataambiwa washone tena sare za kuzima mwenge. Kama huu mwenge umewekewa bajeti na serikali ni vema ukatoa kauli kupiga marufuku michango ya lazima kwa walimu maana hatujasikia wabunge na mawaziri wakilazimishwa kuchangia mwenge. Lakini lingekuwa pia ni jambo la busara kama mwenge sasa utakimbizwa kila baada ya miaka 5 mfano mwaka 2020 ili kuhimiza watu kujiandikisha na kuboresha daftari la wapiga kura. Kama sivyo basi iwe kila baada ya miaka 10 kuhimiza sensa ya watu na makazi. Maisha ya sasa hivi kukimbiza mwenge kila mwaka ni hasara kubwa na usumbufu kwa wengi hasa hiyo michango. Sijui unajisikiaje unapoona walimu wenzako wakiitishwa michango ya mwenge na wakurugenzi wakati kipato na maisha yao ni duni. Walimu wamepigika sana mheshimiwa hawastahili kuendelea kupigwa kwa jambo linaloweza kuepukwa. Mbona mwaka jana tuliahirisha sherehe za uhuru wa Tanganyika kwani tulipata hasara gani zaidi ya faida ya barabara ya Mwenge Moroco iliyojengwa kwa gharama ambazo zingetumika kwenye sherehe?