Elimu bure
Mh Rais akihutubia wazee wa Dar alisema haya: Akizungumzia changamoto ya elimu bure alisema wanafunzi walioanza darasa la kwanza nchini mwaka huu ni 1,337,000, jambo ambalo alisema linaonyesha kuwa wananchi walikuwa wakishindwa kuwapeleka watoto wao shule kwa sababu ya kukithiri kwa michango.
Alisema changamoto zilizojitokeza baada ya Serikali kuanza kutoa elimu bure watazimaliza, ikiwa ni pamoja na kutenga fedha nyingi zaidi kwa ajili ya kuzipeleka katika shule.
Aliwashukuru wananchi ambao wameanza kujitokeza kuchangia ujenzi wa madarasa na kumsifu Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kwa kuendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa shule.
“Lakini angalau Makonda umeshajihakikishia walau utakuwepo ila na wewe usiende kulala, endelea kufanya juhudi. “Ukipanda cheo watu wasikuonee wivu.”
Alisema Makonda amejijengea heshima kubwa kwa kuhamasisha watu wa kada mbalimbali kumaliza changamoto za kuongezeka wa wanafunzi, uhaba wa madarasa na madawati.
Kuhusu changamoto za elimu bure, Rais alisema asilimia 80 ya viongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano wanaishi Dar es Salaam, akiwamo yeye, waziri mkuu, mawaziri, makatibu wakuu na naibu spika.
“Wao wakitoa milioni moja moja zinafika milioni 82 na zitabaki milioni 18, lakini kuna Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na mimi. Tuigawane hii na kila mmoja achangie Sh6 milioni itimie Sh100 milioni na tutaileta kwenye uongozi wa mkoa wa Dar es Salaam,” alisema.
Alisema kwa mamlaka aliyonayo ataongeza Sh2 bilioni na kumtaka mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kutozitumia vibaya, akitaka zigawanywe kwa kila wilaya ili zijengwe shule za kutosha kufidia wanafunzi wanaokaa chini.
Swali langu ni hili: Hivi michango ipo au haipo? Anachofanya Makonda ni sahihi kwa wakuu wengine wa wilaya kufanya? Je hiyo 80% ya viongozi waishio dar ni michango au? Je? Wakuu wa mikoa mingine wakiwachangisha watu kwaajili ya kujenga madarasa inakubalika? Na je kunatofauti gani ya shule zilizokuwa zinawachangisha wananchi kwa maendeleo wa shule zao? Hapa nadhan kuna kitu hakieleweki au kimejificha