Zitto: Hata kesi ya Mbowe ni jumba bovu kwa awamu ya 6. IFUTWE!

Huu ni utumbo tu ambao biashara yake mwisho saa 6. Mbowe anakabiliwa na tuhuma zilizotokea Magufuli akiwa Rais na Mahakama ndiyo yenye jukumu la kumuachia, ndiyo utawala wa sheria huo.

Kuhusu Mbowe kumsaidia Samia nakataa kabisa. Mbowe hana hekima hata kidogo.

Haina ubishi wanufaika wakubwa wa siku 100 za kwanza za Rais SSH ni CDM, Mbowe na Mdude kwa maelekezo, falsafa na haiba ya Samia. Mpaka tukaandika threads nyingi za kusema "Mama anaupiga mwingi".

Ningetegemea Mbowe na Lissu watumie busara katika madai yao kwa kuwa wasikivu na wavumilivu pale Samia aliposema suala la Katiba lisubiri ajenge uchumi.

On the contrary Mbowe na Lissu wakaanza kumfokea Rais kama vile ni mbunge wa BAWACHA?? Na Mdude akasema " nitamnyoa mama yenu kwa wembe uleule nilio mnyolea mtangulizi wake"

Nini kikiwapata hawa watu ambao kwa Mwendazake waliufyata miaka 5. Mwendazake kawapiga risasi, kavunja Bilicanas na kavunja na mashamba yake, kamchukulia na fedha kwenye akaunti. Hajawahi hata kulalamika.

Samia kamrudishia akaunti, kesi zao za kubambika zikapigwa chini pamoja na ya MDUDE. Halafu wao ndiyo wa kwanza kusema HATUWEZI KUMBEMBELEZA Samia.
Comment ina MADINI haswaa......
 
Ifutwe, tena alipwe kutokana na posho na mishahara za walioitunga, ili liwe fundisho.
 
Dhamira ya mama inaonesha wazi kuwa hataki maugomvi na kulipiza visasi.Lakini kwakuwa ameshajionea nia ovu ya baadhi ya watu dhidi ya uongozi wake,ni vizuri akatoa maamuzi magumu.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
Lakini ana jidikia raha kumuona Mbowe mahakamani kila siku? Mbowe ni baba wa familia kama Mama Samia alivyo mama wa familia. Kesi yenyewe haina kichwa wala miguu. Hadi sasa sio Kingai wala Mahita walio weza kuonyesha ugaidi ulifanyika wapi?
Kwa matendo Ccm inayo mfanyia Mbowe wasidhani hasira za Mungu zita acha kuwa andama.
Mbowe sio gaidi...
 
Si ulisema Magufur na samia, Hawa watu ni kitu kimoja....? Inabidi tu ukubali mama
Mimi nilisema kuwa msaidizi wa shetani hawezi kuwa Malaika na Samia akaja kuconfirm hili jambo yeye mwenyewe kuwa yeye na Magufuli ni kitu kimoja😁😁😁
 
Hii kesi ni kweli kabisa haina mashiko na doa lakini tusikatae ukweli kwamba Mh. Mbowe naye aliingizwa chaka na waliomwambia aanze kumtunishia misuli mama. Mama alianza vizuri sana kwa kuahidi mambo yaende kwa utaratibu na vikao. From no where mkaanza kumchomekea agenda ya Katiba mpya tena kwa ubabe huku mkijua miezi michache iliyopita mwendazake akiwepo mliufyata. Hii ilimpa picha kuwa mnataka kumpelekesha na kumfanya atoke kwenye agenda zingine. Tujisahihishe.
 
Hii kesi ilianza lini? Awamu ya tano imeingiaje kwenye hii kesi?
Shida Zitto anapenda sana kuonyesha kila tatizo ni tatizo la miaka mitano ya nyuma. Hata kama limeanza leo
 
Injili ya Luka Mtakatifu Mlango wa 3:

2 wakati wa ukuhani mkuu wa Anasi na Kayafa, neno la Mungu lilimfikia Yohana, mwana wa Zakaria, jangwani.

14 Askari nao wakamwuliza, wakisema, Sisi nasi tufanye nini? Akawaambia, Msidhulumu mtu, wala msishitaki kwa uongo; tena mtoshewe na mshahara wenu.
 
Back
Top Bottom