Mh Rais Magufuli wamulike wawakilishi wako huko Misenyi

tinkanyarwele

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
2,016
1,945
Sijui shetani alizaliwa mwaka gani lakini tungeujua huo mwaka basi ungefutwa kwenye kalenda, kwa miaka ya nyuma lilikuwepo jimbo la Nkenge (Misenyi) liliwakilishwa na huyu bwana Deodorus Kamala, katika umri wangu chini ya ubunge wake sikuwahi kuona chochote alichokifanya, tofauti na kutoa ahadi feki, zaidi aliimarisha miundombinu katika tarafa moja tu yaani tarafa mama huku zingine akizipa kisogo, Mungu si athumani huyu jamaa alitoka na Rais Kikwete alimpa kuwa balozi huko nje ya nchi, mrithi wake aliitwa Asumpta Mshama, huyu mama ndo aliharibu to the climax hakufanya chochote tofauti na kununua jezi na mipira kwa vijana wa timu ya pale Bunazi.

Shetani akarudi kuiandama wilaya hii mwaka 2015 yuleyule Kamala akachukua tena kiti cha ubunge, la kustaajabisha hadi sekunde ya leo sijaona chochote kutoka kwake. Katika vyeo vya wakubwa kutoka serikalini mfano RC, DC, DEO, Afisa Watendaji na Viongozi wengine wa serikali hadi ngazi za vitongoji ndo kabisaaa hii wilaya hawaijui japo wengine wanaishi humo.

Ni wilaya yenye rasilimali za kutosha ambazo zingepata usimamizi dhabiti zingesaidia sana kuliongezea tija taifa hili, mfano, kuna kiwanda cha sukari Kagera, kuna msitu mkubwa wa Minziro, kuna Mto Kagera ambao unafaa sana kwa kilimo cha umwagiliaji, kuna ziwa Victoria, aridhi yenye rutuba kwani inastawisha sana ndizi, mahindi, kahawa na miwa kama mazao makubwa lakini mazao madogo kama maharage , mihogo karanga huku ndo mahala pake.

Mbali na hayo sehemu hii hupata mvua za kutosha kwa mwaka, kuna mapori mazuri sana ya kuchungia mifugo. Mbali na tunu hizo zote bado wilaya hii ina masoko ya uhakika kuliko baadhi ya maeneo hapa nchini, mfano inapakana na Uganda sehemu za Mutukula na Minziro, mpaka wa Mutukula ni kitovu cha biashara katika mkoa wa Kagera , mazao ya mahindi, maharage na kahawa hapa kuna soko zaidi ya 100% .

Sasa hoja yangu kuu ni kwamba viongozi wateule na wale wa kuchaguliwa wameshindwa kutumia eneo hili kwa usimamizi na wananchi wamejisahau kwa kukosa usimamizi, mfano maeneo yote yanafikika kwa urahisi sana ila miundombinu hakuna, kwa mfano umeme, baadhi ya vijiji havina umeme , kwa mfano kijiji cha Mabuye na Itala havina sababu ya kukosa umeme lakini haupo, kama vijiji hivi vingekuwa na umeme basi ungesaidia wananchi kuvuta maji ambayo yangefaa kwa kilimo cha umwagiliaji, zahanati nahisi ni moja tu iko pale Bunazi.

Barabara za mitaa hakuna hivyo watu kupitisha mazao yao kwenda sokoni ni ngumu sana, vilevile suala la maji bado viongizi wamekaa kimya sana Mto Kagera unafaa kwa kufunga maji ambayo yangeuzwa kwa wananchi wa wilaya yote ya Misenyi, mfano kutoka mto Kagera kwenda kwenye vijiji vya Kassambya, Mabuye, Bunazi ni rahisi sana lakini hakuna ubunifu wowote juu ya hili serikali, viongozi na wachaguliwa wote wako kimya. Sasa sijui ni shetani yupi amekalia wilaya hii.

Rais naomba ujaribu kuwakumbusha sana wateule wako kuwa hapa taifa linapoteza sana mapato kutokana na ukosefu wa usimamizi makini wa kiutendaji.
 
Back
Top Bottom