Mh. Rais Magufuli naomba uwasamehe watumishi "wafoji" umri

matunge

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
442
500
Mheshimiwa Rais awali ya yote napenda kukupongeza kwa dhati ya moyo wangu kwa namna unavyoiongoza nchi yetu. Pia napenda kukufahamisha kwamba mimi ni miongoni mwa watanzania waliokupigia kura wakati wa uchaguzi wa mwaka 2015. Aidha mpaka ninaandika jambo hili sijaona mahali popote uliponiangusha. Ninachokishuhudia ni kukuona ukipita kwenye mawazo yangu na ndoto yangu ya kuliona taifa likiwa na shirika la ndege lenye nguvu duniani. Taifa lenye mtandao wa reli za kisasa zinazounganisha bandari zetu za Tanga, DSM na Mtwara na bara mpaka nchi za Zambia, DRC, Burundi, Rwanda, Uganda na hata Kenya. Kuliona Taifa lenye viwanda vya kila aina na vinavyotoa ajira kwa vijana wetu. Kuliona Taifa lenye vijana wengi waliosoma na kujiajiri. Kuuona mji wa Dodoma ulioshamiri na kuwa makao makuu kamili ya nchi yetu. Kuuona serikali isiyokumbatia wazembe na wala rushwa. Kuliona Taifa linalojali watu wake na kuwaendeleza kupitia rasilimali zao mfano madini na gesi. Kuliona taifa linarudisha uhusiano na mataifa yenye watu wenye ubunifu wa hali ya juu ikiwamo Israel. Namuomba MUNGU amzuie shetani asije kukuingia na kukubadilisha. Pia akupe afya njema. Amina

Baada ya pongezi hizo naomba nirejee kwenye mada iliyokusudiwa. Mheshimiwa Rais kama unavyokumbuka Tarehe 01.05.2017 ulitoa kauli ya kuwashughulikia watumishi waliobadili umri ili wasistaafu mapema. Nakili wazi kwamba hili ni kosa la jinai na utakuwa sahihi kabisa ikiwa utawashughulikia watumishi wa aina hiyo. Lakini nikilitazama kwa mapana zaidi suala hili nawaona watumishi waliotoka familia masikini na za wazazi wasio na elimu yoyote wasio na uwezo wa kutunza kumbukumbu za Tarehe za kuzaliwa za watoto wao. Mtumishi wa aina hii akichunguzwa utagundua ameandikisha Tarehe tofauti tofauti wakati wa matukio mbali mbali mfano ubatizo, kuanza shule na wakati wa ajira. Kimsingi hawafahamu ni lini walizaliwa.

Mhe. Rais ikiwa utachukua hatua kali kwenye suala hili ni hakika utaumiza wengi. Itoshe KUKUOMBA tu Kwa JINA LA YESU KRISTO UWASAMEHE ili tuanze upya ikiwa ni pamoja na kuweka mfumo wa computer wa kurekodi Tarehe ya kuzaliwa kila mtanzania anapozaliwa na kwamba tarehe hii ndiyo itumike wakati wa kujiandikisha shule, chuo na kazi.

Kwa KUHITIMISHA Mhe. Rais kwa mara nyingine nakupongeza sana kwa kazi nzuri unayoendelea kuifanya kwa ajili yetu sisi wananchi. MUNGU akubariki afya njema, hekima na moyo wa uzalendo. AMEN
 

Ndukidi

JF-Expert Member
Jun 30, 2012
1,499
2,000
Hapana sheria isibague, kufoji ni kufoji tu , kwajina la Yesu, mtume Mohamed, Jehova au lolote lile.
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
41,856
2,000
Tutakuja kufuta na kinga za maraisi ili nao waje wawajibike kwa makosa yao hawa wakiwa wazee wa miaka 80.

Isitoshe, kuna watakokuja kuwajibika kwa makosa waliyoyafanya kabla hawajawa maraisi maana hawana kinga kwa makosa waliyoyafanya wakiwa mawaziri.
 

mzee wa manzese

JF-Expert Member
Oct 31, 2012
670
225
Hao waliofoji umri wako wengi sana serikalini,utakuta Mzee ana umri wa miaka 63 kwenye file data zinaonyesha 57,mheshimiwa Raisi watoe kama ulivyo watoa wenye vyeti feki,
 

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
10,525
2,000
Baada ya pongezi hizo naomba nirejee kwenye mada iliyokusudiwa. Mheshimiwa Rais kama unavyokumbuka Tarehe 01.05.2017 ulitoa kauli ya kuwashughulikia watumishi waliobadili umri ili wasistaafu mapema. Nakili wazi kwamba hili ni kosa la jinai na utakuwa sahihi kabisa ikiwa utawashughulikia watumishi wa aina hiyo. Lakini nikilitazama kwa mapana zaidi suala hili nawaona watumishi waliotoka familia masikini na za wazazi wasio na elimu yoyote wasio na uwezo wa kutunza kumbukumbu za Tarehe za kuzaliwa za watoto wao. Mtumishi wa aina hii akichunguzwa utagundua ameandikisha Tarehe tofauti tofauti wakati wa matukio mbali mbali mfano ubatizo, kuanza shule na wakati wa ajira. Kimsingi hawafahamu ni lini walizaliwa.

Je, hapa hajakupa jibu? Acha sheria ifuate mkondo wake. Kwa mujibu wa baadhi ya tafiti nchini karibu watanzania wote wanavunja sheria, sasa acha sheria ifanye kazi yake ya kukata mbele na nyuma kwani kujikata inawezekana.

 

Dan Zwangendaba

JF-Expert Member
Apr 25, 2014
2,598
2,000
Muache aendelee kuhakiki hadi idadi ya meno mlioambiwa mtalimia ila 2020 naye tutamhakiki tu ili ajue utamu wa kuhakikiwa ulivyo.
 

galindas

JF-Expert Member
Mar 3, 2013
980
1,000
uhakiki mpa unahusu hilo pia. Ndio maana mtumishi atatakiwa kuwa na salary slip na kadi ya nida.
 

ex1950

Senior Member
Dec 12, 2015
126
250
Mheshimiwa Raisi . Washughulikie wote waliofoji umri . Ni wengi mno . Achana na huyu aliekuja na shairi ndefu na unafiki wa kukupongeza inawezekana ni mmoja wao .
 

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
2,216
2,000
vijana wengi wanakosa ajira kwa sababu ya walio foji umri wa kustaafu!
kama hujui umri wako basi wewe umeziba nafasi za wengine.

watumishi wa umma ndio wanaogoza kuwa na wazee zaidi kuliko sekta binafsi na hii imesababishwa na kufoji umri,

mwenye umri wa miaka 60 anadai ana miak50

mwenye miaka 50 anadai ana 40 nk hili ni tatazo kamwe lisi fumbiwe macho.

wizara husika ni vyema ikahakiki jambo hili
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom