Trust None
JF-Expert Member
- Feb 12, 2018
- 1,260
- 4,415
Mheshiniwa Rais, ulishawahi kuwakemea wateue wako kutogombea ubunge ukiwaonya kuwa hiyo ni tamaa.
Nakumbuka ulitolea mfano kwa Mwananzira aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Tabora na ukasema aliwahi kuwa Naibu Waziri enzi za Mh. Kikwete. Ukasema kuwa aliona ukuu wa mkoa hautoshi akaenda kugombea ubunge.
Nakumbuka ulisema kuwa uliona ni mtu mwenye tamaa sana, hafai hata kuwa katibu tarafa na ndiyo maana amepotea.
Nilitegemea mkuu wa wilaya ya Ikungi alipochukua fomu ya Ubunge ungemchukulia hatua mapema sana lakini naona bado kimya.
Huenda kuna TEUZI inaandaliwa baada ya huyo Miraji Mtaturu kushinda ubunge kwa kupita bila kupingwa kwasababu mpaka wakati huu sijaona harakati zozote za wapinzani. Au uliona ukimvua uDC halafu ukamteua ingeleta picha mbaya?
Binadamu tumeumbwa na tamaa ya kuwa na kipato kikubwa zaidi kwa maendeleo yetu.
Hata wewe mheshimiwa Rais unapotekeleza miradi ya maendeleo una lengo la kuifanya Tanzania ipige hatua kimaendeleo (tamaa ya maendeleo), usingekuwa na tamaa ya maendeleo ungepiga kimya tu.
Hata wewe mheshimiwa ulikuwa Mwalimu, ukawa mkemia, ukagombea ubunge, ukateuliwa kuwa waziri na baadae ukagombea Urais. Naamini hizi zote ni juhudi (tamaa) za kila mwanadamu kupiga hatua moja kwenda nyingine.
Hata mimi nilikuwa natembea kwa mguu kwenda shambani lakini sasa hivi nimenunua baiskeli, baadae nitanunua pikipiki na mbeleni magari na mabombadia. Hizi zote ni tamaa za maendeleo kama ilivyo kwa kila mwanadamu.
Jumapili njema.