Wanabodi, moja ya mambo ambayo wananchi hasa watumishi wa umma wanayoyatarajia raisi kuyaongelea siku ya wafanyakazi ni haya yafuatayo:
1. Kutolea ufafanuzi suala la watumishi kupitia kozi maalum ndipo wapande madaraja. Watumishi wanalitegemea sana hili uliongelee mheshimiwa.
2. Kutolea ufafanuzi suala la RC Paul makonda kuendelea kubaki madarakani huku akitumia vyeti vya mtu mwingine, hill litolee ufafanuzi raisi wangu!
3. Je madeni ya watumishi wa umma waliyoyatolea jasho utatuambiaje Mkuu? Au tayari kama ulivyosema kuwa hutalipa sababu ni madeni hewa ulikuwa unamaanisha?
4. Suala la tumbua tumbua kwa watumishi wa umma bila kujali taratibu za utumishi wa umma.
5. Suala la udhalilishaji kwa watumishi wa umma haswa madaktari, linalofanywa na wateule wako. Mfano kuwasweka rumande madaktari bila sababu za msingi.
6. Suala la ajira mpya Kwa vijana ambao wengi walikupigia kura wakiwa na Tumaini Kubwa kuwa utawavusha kwenye janga hili Kubwa lililobatizwa jina la " Bomu linalosubiri kulipuka".
7. Suala la uhamisho kwa watumishi wa umma, suala hilo mpaka sasa limezuiliwa na watumishi hawajui hatima yake, hivyo watumishi tunasubiri kauli yako mtukufu raisi.
8. Suala la kuwapandishia mshahara watumishi wa umma; hili ni suala muhimu kuliko yote kwani serikali imekuwa ikiwaongezea mshahara watumishi kila mwaka ili kuendana na gharama za kupanda Kwa maisha.
# Mwisho kabisa nipende kukutakia heri mheshimiwa raisi katika utendaji kazi wako wa kila siku, ila hakuna siku wafanyakazi watakayo furahi kama siku hiyo utakapozungumzia hizo changamoto zao hapo juu zinazowakabili, aidha utaonekana shujaaa pia kutokana na ukweli kuwa kila mfanyakazi ana kundi Kubwa la wategemezi wanaomtegemea, umeweza suala la Nay wa Mitego tutatulie na sisi changamoto zetu zinazotusibu!!
AHSANTE.