Mh.Rais: Kupuuza Wanaopewa Mimba Shuleni ni Uasi.

Toosweet

JF-Expert Member
May 27, 2012
2,141
1,982
Heshima Kwenu,
Naandika Uzi huu kwa masikitiko. Unaweza usifaulu toka shule ya msingi kwenda sekondari au ukawa umefaulu lakini mzazi/mlezi akawa hana uwezo japo wa kununua unifomu.
Tarehe 22/06/2017 siku ya Alhamis, Rais Magufuli akiwa katika ziara Bagamoyo mkoa wa Pwani alisema, "serikali inatoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya elimu bure, halafu zinakuja NGO zinasema eti anayepata mimba akishazaa(siyo kujifungua), aruhusiwe kurudi shuleni... ".Rais aliendelea, "azae halafu aende kuwahubiria wenzake? Unajua ooh ilikuwa hivi, halafu nikafanya hivi. Zipo kazi nyingi tu za kufanywa na hawa, siyo lazima warudi shule, kuna kushona cherehani na hata kilimo cha bustani"
Ikumbukwe kuwa hawa wanaopewa mimba ni watoto, si watu wazima. Mara nyingi wanaowapa mimba hutumia nguvu, hutumia ushawishi wa nafasi zao kwenye jamii au familia(undue influence), hutumia fedha kwa kuangalia umasikini na uhitaji wa msichana na pia hutumia mazingira ya msichana kwa wakati huo, yaani umbali kutoka shule mpaka nyumbani na uwepo wa msitu au vichaka. Haya yote hayaletwi na msichana. Kubakwa hakutokani na "kiherehere" kama alivyopata kusema Rais mstaafu Kikwete. Tunawapa watoto wa kike adhabu ya kuwanyima elimu kwa kuwa tu ni dhaifu. Wengi wa wanaowapa mimba hawakamatwi wala hawafungwi.
Rais anaposema wasichana waliopata mimba washone cherehani au kulima bustani anamaanisha nini? Anataka kazi hizo zifanywe na wasio na elimu hata ya msingi.Hii ni kinyume na ilani aliyoombea kura mwaka 2015.Ilani ya CCM 2015-2020 ibara ya 52:Elimu ya kisasa na hasa yenye mwelekeo wa kisayansi na teknolojia ina nafasi ya pekee katika kufanikisha ujenzi wa msingi wa uchumi wa kisasa wa taifa linalojitegemea... I) ii inasema
Wasichana wote wa elimu ya msingi wanaoacha shule kwa sababu ya kupata ujauzito wataendelea na masomo.
Hichi anachokifanya Rais ni ilani ya wapi? Haoni kuwa anafanya uasi? Urithi pekee wa maana kwa maskini ni elimu hata ya msingi. Ni laana kunyima mtoto wa kike elimu japo ya msingi kwa sababu zozote zile.
Kwa mujibu wa Ripoti ya Serikali ya Utafiti wa Idadi ya Watu na Afya (TDHS) ya mwaka 2016,kiwango cha mimba za utotoni nchini Tanzania ni asilimia 27.Yaani kwa kila wasichana 100,wasichana zaidi ya 20 hubeba mimba za utotoni. Angalia mikoa na asilimia zao :Kilimanjaro 6%,Arusha 15%,Kagera 15%,Iringa 20%,Njombe 20%,Tanga 21%,Manyara 26%,Mtwara 26%,Lindi 28%,Mwanza 28%,Rukwa 29%,Geita30%,Pwani 30%,Simiyu 30%,Singida 30%,Kigoma 32%,Ruvuma 32%,Mbeya 33%,Shinyanga 34%,Mara 37%,Dodoma 39%,Morogoro 39% na Katavi 45%.
Kwa kuangalia takwimu hizo na ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020,Rais anataka kujenga taifa la namna gani?
Nawasilisha tujadili.
 
Tanzania, Tanzania

Ni nchi ya ajabu sana,ss tunaitaji mtu dikteta ili tuache kutegemea watu
 
Kajenge shule yako ya wanafunzi wa hivyo manake Rais hajakataza hilo.Tanguapo hakuna shule ambayo ilishawahi kuruhusu wanafunzi waja wazito kurudi shule Rais ametilia mkazo msimamo huo Sasa sijui kwanini mtu unalalamika kama vile hapo awali ilikuaga inarushuiwa.Acheni unafiki.
 
Huu ulioandika ndio unafiki wa kiwango cha juu sana, umesoma kilichonukuliwa kwenye ilani yenu?
 
Sishangai kwa kuwa hufugiki. Sina hakika kama ni simba au nyumbu.
Kuna mambo yanahitaji fikra mkuu. Hayataki kushangilia kila anachosema rais. Jifunze.

Kama asilimia 80 ya wasichana wana uwezo wa kuendelea na shule bila kupata mimba ina maana sera zetu za kukataa wajawazito wasiendelee na shule zinafanya kazi...ni kuongeza msisitizo ili hao wachache asilumia 20 waingie kwenye kundi la wanaojitambua.
 
Huu ulioandika ndio unafiki wa kiwango cha juu sana, umesoma kilichonukuliwa kwenye ilani yenu?
Acha upuuzi si kila kitu kichopo kwenye ilani ni lazima kifuatwe kwakua ilani si Sheria ya nchi.Jenga shule yako ya hivyo manake MH keshaweka msimamo na huna unaloweza kufanya kumbadilsha.
 
Heshima Kwenu,
Naandika Uzi huu kwa masikitiko. Unaweza usifaulu toka shule ya msingi kwenda sekondari au ukawa umefaulu lakini mzazi/mlezi akawa hana uwezo japo wa kununua unifomu.
Tarehe 22/06/2017 siku ya Alhamis, Rais Magufuli akiwa katika ziara Bagamoyo mkoa wa Pwani alisema, "serikali inatoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya elimu bure, halafu zinakuja NGO zinasema eti anayepata mimba akishazaa(siyo kujifungua), aruhusiwe kurudi shuleni... ".Rais aliendelea, "azae halafu aende kuwahubiria wenzake? Unajua ooh ilikuwa hivi, halafu nikafanya hivi. Zipo kazi nyingi tu za kufanywa na hawa, siyo lazima warudi shule, kuna kushona cherehani na hata kilimo cha bustani"
Ikumbukwe kuwa hawa wanaopewa mimba ni watoto, si watu wazima. Mara nyingi wanaowapa mimba hutumia nguvu, hutumia ushawishi wa nafasi zao kwenye jamii au familia(undue influence), hutumia fedha kwa kuangalia umasikini na uhitaji wa msichana na pia hutumia mazingira ya msichana kwa wakati huo, yaani umbali kutoka shule mpaka nyumbani na uwepo wa msitu au vichaka. Haya yote hayaletwi na msichana. Kubakwa hakutokani na "kiherehere" kama alivyopata kusema Rais mstaafu Kikwete. Tunawapa watoto wa kike adhabu ya kuwanyima elimu kwa kuwa tu ni dhaifu. Wengi wa wanaowapa mimba hawakamatwi wala hawafungwi.
Rais anaposema wasichana waliopata mimba washone cherehani au kulima bustani anamaanisha nini? Anataka kazi hizo zifanywe na wasio na elimu hata ya msingi.Hii ni kinyume na ilani aliyoombea kura mwaka 2015.Ilani ya CCM 2015-2020 ibara ya 52:Elimu ya kisasa na hasa yenye mwelekeo wa kisayansi na teknolojia ina nafasi ya pekee katika kufanikisha ujenzi wa msingi wa uchumi wa kisasa wa taifa linalojitegemea... I) ii inasema
Wasichana wote wa elimu ya msingi wanaoacha shule kwa sababu ya kupata ujauzito wataendelea na masomo.
Hichi anachokifanya Rais ni ilani ya wapi? Haoni kuwa anafanya uasi? Urithi pekee wa maana kwa maskini ni elimu hata ya msingi. Ni laana kunyima mtoto wa kike elimu japo ya msingi kwa sababu zozote zile.
Kwa mujibu wa Ripoti ya Serikali ya Utafiti wa Idadi ya Watu na Afya (TDHS) ya mwaka 2016,kiwango cha mimba za utotoni nchini Tanzania ni asilimia 27.Yaani kwa kila wasichana 100,wasichana zaidi ya 20 hubeba mimba za utotoni. Angalia mikoa na asilimia zao :Kilimanjaro 6%,Arusha 15%,Kagera 15%,Iringa 20%,Njombe 20%,Tanga 21%,Manyara 26%,Mtwara 26%,Lindi 28%,Mwanza 28%,Rukwa 29%,Geita30%,Pwani 30%,Simiyu 30%,Singida 30%,Kigoma 32%,Ruvuma 32%,Mbeya 33%,Shinyanga 34%,Mara 37%,Dodoma 39%,Morogoro 39% na Katavi 45%.
Kwa kuangalia takwimu hizo na ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020,Rais anataka kujenga taifa la namna gani?
Nawasilisha tujadili.
Halarisheni sasa nyie
 
Kwa hili bandiko ndio nauona umuhimu wa stori za LEGE

HASA HII YA WUIN MONICA
Mwandishi aliitabiri hii kutokea tz
 
Acha upuuzi si kila kitu kichopo kwenye ilani ni lazima kifuatwe kwakua ilani si Sheria ya nchi.Jenga shule yako ya hivyo manake MH keshaweka msimamo na huna unaloweza kufanya kumbadilsha.
Pathetic! A very low thinking capacity. Learn to respect others, it won't cost you.
 
Back
Top Bottom