Mh. Rais, kujipa muda kabla ya kuagiza chanjo ni jambo jema lakini kukataa chanjo ni jambo ambalo halitowezekana na halitakuwa la busara!

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,182
42,001
Wasalaam wana jamvi.

Wanajamvi wasalaam, bila shaka kila mtu anajua fika kabisa kuwa janga la Corona limeathiri dunia na uchumi wa dunia kwa ujumla kabisa.

Na ni wazi kabisa Tanzania tuna Neema ya kipekee sana kwani ugonjwa huu haujawa na atahari kubwa kama nchi nyingine za wenzetu
Na katika hili kila Mtanzania ana haki na wajibu wa kumshukuru Mungu.

Lakini hivi karibuni kumekuwepo na taarifa ya za kupatikana kwa chanjo ambayo pengine kwa nchi za Ulaya inatarajiwa kutolewa kama sio January basi ni December.

Ukweli ni kwamba kama chanjo zinazo tajwa zitafanikiwa basi litakuwa jambo jema na tutamshukuru Mungu pia....
Ni lazima tujua kuwa chanjo ni kinga kwa hiyo kama zitafanikiwa kuzuia ugonjwa huo basi litakuwa jambo jema kabisa kwa Dunia nzima.

Lakini katika hili la chanjo naipongeza serikali kuto harakisha kuagiza kwa chnjo hiyo kabla hata haijaanza kutumika uko ulaya na marekani kwani kumekuwa bado na mjadala kuhusu uhakika hizo chanjo kwa hiyo kujipa muda ni jambo jema.

Lakini napingana naserikali kusema kuwa haito agiza chanjo wakati ugonjwa huu haijaweza kuupatia dawa au chanjo yake hapa nchini na litakuwa jambo la ajabu sana kukataa chanjo wakati bado Tanzania ina muingiliano wa kila aina ya watu wa mataifa mbalimbali duniani.

Lazima tukubali kuwa kama kuna chanjo ambayo itathibitika ina ufanisi dhidi ya CORONA ni lazima itaagizwa kwa kutaka au kutotaka kwani tanzania sio kisiwa cha peke yake.

Kama tuna jipanga kukataa chanjo dhidi ya Corona ni lazima tuhuthibitishie ulimwengu kuwa tunayo chanjo yetu ambayo ina ufanisi kuliko zao na ni ni kwa jinsi gani hatuwezi kupata Corona hata tukikutana na mwenye Corona.

Watanzania wanatakiwa kujua kutokuwa na Corona hauwezi kuwa ndio utetezi wa kutokuagiza chanjo.
Watanzania tuna chanjo nyingi sana ambazo zimekuwa zikitolewa kila leo na hatujawai kuzikataa na nina hakika hata hizo zote tulijipa muda kabla ya kuagiza.

Bado naamini hata chanjo ya Corona ni muhimu kwa tanzania na watanzania na ni vyema serikali ikaendelea kutafakari lakini lazima ijue kuwa kuagiza chanjo ya Corona hakuto zuilika kama itathibitika pasi na shaka ambazo zilizo tengenezwa zimwkuwa na ufanisi mkubwa sana kwa binadamu dhidi ya Corona.

Wasalaaam
 
Huyu atakuwa ni mmoja wa wale wanaokwea pipa mara kwa mara kwenda nje ya nchi kitu ambacho kitawacosti.

Si unajua mabeberu na dunia kwa ujumla wameandaa mpango wa kutoruhusu mtu yeyote kupanda ndege zao kama hajadungwa chanjo?
Hivi kumbe siwezi kutoa ushauri mpaka niwe nataka kusafiri? huu ni ushauri kwa serikali
 
Hakuna atakaekataa chanjo, hayo ni maneno.

Hakuna mwenye ubavu wa kukataa chanjo.

Unakataa chanjo ya corona halafu unapokea vidonge vya ARV, cancer na magonjwa mengine, hizo akili ama mavi?
Naungana na wewe na pengine ni swala la kujipa muda lakini kukataa chanjo ni jambo ambalo haliwezekani
 
D0A45EDB-F47D-4AF5-9AC0-4702635229D3.jpeg

Angalia wenzako
 
Lazima hili swala linataka kugusa maisha yako ndio maana leo umeweka unafiki pembeni!
Itafika muda tutaongea lugha moja tu hakuna namna
hahahaha unajua Bavicha huwa mnaharibu mijadala ndio maana wengine huwa wanaoa jf ni pawatu walijaa negativity tuu............... kwani ni lazima mabaya au mazuri niyasema mimi tuu kwani wewe ukisema hutoshi? wewe ni lini umemkosoa Mbowe na chadema?
Mimi nimehamua nisema kwenye hili kama wewe unaona mengine yasema na ndio uhuru wa maoni.
 
BAVICHA huwa mnanichekesha sana yani mnafikiri kila anayekubaliana na ninyi kwenye kila kitu basi ndio kamanda.................

Huwa unakubali kila upuuzi, leo unajitoa muhanga baada ya kufiwa na mtu kwa covid, ndio unajifanya kushauri. Nani anakusikiliza ww kapuku. Ww kazi yako ni kusifia tu, achia wenye akili wakosoe.
 
Huwa unakubali kila upuuzi, leo unajitoa muhanga baada ya kufiwa na mtu kwa covid, ndio unajifanya kushauri. Nani anakusikiliza ww kapuku. Ww kazi yako ni kusifia tu, achia wenye akili wakosoe.
hahahahaha Bawacha punguza hasira mbona unalazimisha kufiwa hahahaha
Wewe ni lini umemkosoa Mbowe? hahahaha
 
Back
Top Bottom