Mh Rais Kikwete kauli zako zina utata

Ni ajabu kuifananisha Serikali ya Kikwete na Serikali ya Kikaburu, Halafu wakati huo huo unamuita kiongozi wa serikali hiyo Mheshimiwa. Mimi nadhani kaburu hana heshima au?

Kaburu hana heshima ilhal mshayasahau waliyoyapigania wazee wetu hawa.,sasa hivi mnawapigia magoti na kuwaomba waje kuwekeza huku mkifarakana na mwekezaji wa enzi na enzi jirani yenu.
 
ndiyo maana sisi WATANZANIA kwa kauli moja tunasema kwamba DR SLAA ni MANDELA aliye hai , CDM DAIMA kwa mustakabali wa nchi .
 
Akiongea katika maadhimisho ya siku ya uhuru amemsifia mzee Mandela bila kukumbuka yanayofanyika kwenye serikali yake. Ambayo amesema yafuatayo.
1.Mzee Mandela aliwapigania watu wake dhidi ya serikali ya kibaguzi iliyokuwa akiongozwa na Makaburu.
2.Mzee Mandela alipoona kutafuta haki na usawa kwa njia ya AMANI ilibidi aanzishe chama cha siasa yaani ANC
3.Akiwa ndani ya ANC na kuona watawala bado hawako tayari kutenda HAKI ilibidi azunguke nchi mbalimbali kwa lengo la kuanzisha JESHI.
4.Lakini kabla ya kuanza kulitumia jeshi alikamatwa na kufungwa gerezani.
5.Amesema mzee Mandela alipokuja Tanzania alilala kwa mama Nsilo Swai na kusahau viatu vyake kwa mama Nsilo Swai.
Mh rais ameona mabaya ya makaburu na kumuona mzee Mandela alikuwa sahihi wakati rais Kikwete anajua dhuluma zinazofanywa na serikali yake kwa kukikandamiza Chadema na hata Chadema inapoona HAKI inashindikana kupatikana kwa njia ya AMANI na zaidi ya yote kutumia vyombo vya dola kuvuruga mikutano ya Chadema iliamua kutangaza kuanzisha makambi ya ukakamavu kwa vijana wa Chadema kwa lengo la kulinda mikutano na viongozi, wanachama na wasiokuwa wanachama bado serikali ya mh Kikwete ilileta ubabe katika swala hili.

Sasa serikali hii ya CCM inatofautianaje na serikali ya makaburu wa Afrika ya kusini?

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Umeshindwa kufananisha na kuhisi kuwa CDM ndio Watanzania?
 
Kaburu hana heshima ilhal mshayasahau waliyoyapigania wazee wetu hawa.,sasa hivi mnawapigia magoti na kuwaomba waje kuwekeza huku mkifarakana na mwekezaji wa enzi na enzi jirani yenu.

Sasa hivi South Africa iko chini ya Wazalendo, Kama wasouth wenyewe wameshafanya reconciliation kwa nini sisi tuwe na nongwa?
 
ndiyo maana sisi WATANZANIA kwa kauli moja tunasema kwamba DR SLAA ni MANDELA aliye hai , CDM DAIMA kwa mustakabali wa nchi .

CDM kinapashwa kipitie njia zilezile na mikakati ileile ya Mandela kwani CCM hivi sasa hakina tofauti na chama cha makaburu wa enzi zile za akina Pik Botha na chama chao cha "National Party" waliokuwa wanang'ang'ania watawale milele huku wakitumia ubabe na dola wa kuua raia wasiokuwa na makosa, kutesa, kuwapa kesi za kubambikiza na kuwafunga bila sababu za msingi... hadi pale ANC ilipoamua kuunda jeshi ndani ya chama-Umkhoto we Sizwe" ili kuubana utawala wao uliokithiri kwa vitendo vya kinyama na mwisho uhuru wa kweli ukapatikana kwa msaada pia wa inchi marafiki waliokuwa hawapendi udhalimu huo,...Demokrasia bila maarifa na nguvu ziada ni sawa na mbwa mzee asiye na meno na ndio maana Mzee Madiba akiwa kijana alipita hapa akiwa safarini kwenda Algeria kuchukua mafunzo ya kijeshi..

Madiba alipingana na utawala dhalimu uliokuwa wa kibaguzi wakati wakitawala africa kusini,

CDM inapingana na utawala wa kidhalimu, kibaguzi kwa walionacho na wasionacho, utawala wa mafisadi kukalia uchumi na kuleta pengo kubwa la walionacho na wasio nacho, daima CDM inapingana na sera mbovu za umaskini wa kujitafutia na sio kupingana na watu

Nadhani Kuongea na hawa jamaa ni sawa na kumchekea nyani shambani kwani mwisho wa siku utavuna mabua,

Hebu tutafakari nini maana na tafsiri ya kusameheana, kama hivi sasa CDM hawapati haki yao ya msingi je nini kifuatacho? kweli kutakuwa na kusameheana hapo baadaye wakati watawala wetu hatuoni wakisamehe na kutenda haki?

ili pawe na heshima pande zote (bilaterally) zapaswa ziheshimiane mbali na hivyo kamwe hapatakuwa na maelewano ya kiukweli bali ni kulana kisogo tu
 
.....
..
4.Lakini kabla ya kuanza kulitumia jeshi alikamatwa na kufungwa gerezani.
5.Amesema mzee Mandela alipokuja Tanzania alilala kwa mama Nsilo Swai na kusahau viatu vyake kwa mama Nsilo Swai.
...
...
Sasa serikali hii ya CCM inatofautianaje na serikali ya makaburu wa Afrika ya kusini?

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
Utajiri wa Kichaga ni wa wizi na kukwepa kodi tu.
Haitatokea mchaga akawa Rais wa Nchi hii.
Nimeskia interviewe ya huyu mama na nikaguswa sana.
Kwa wale wanaoeneza propaganda chafu za ukanda na ukabila sasa mtaelewa kuwa watu wa kanda hii hawajaanza siasa za ukombozi leo, na huu ni uthibitisho ulio wazi.
Mama Swai:Mandela alinifunza uvumilivu - BBC Swahili - Medianuai


 
Sasa hivi South Africa iko chini ya Wazalendo, Kama wasouth wenyewe wameshafanya reconciliation kwa nini sisi tuwe na nongwa?

Je ushawahi kutembelea sehemu walizowekeza makaburu hapa home ukaona manyanyaso wayapatayo nduguzo au waja na hekaya za kigamba tu hapa nyonyonyo nyonyonyo nyonyo???
 
aache kuogopa kivuli chake. Kama anajua kuna visasi kwa nini asiongoze katika njia ambayo haitampa maadui?
UKIUA KWA UPANGA NAWE UTAUWAWA KWA UPANGA
nitofautiane kidogo na wewe juu ya Kikwete japokuwa sikubaliani naye kwa baadhi ya falsafa zake. 1995 kiukweli ni kuwa jamaa alimshinda mkapa kabla ya nyerere kupindua matokeo yake. lakini bado alivunja makundi yake na akaweza kufanya kazi na mkapa bila kinyongo kwa miaka yote 10. Lakini jiulize hawa wanaojihisi walimshinda kikwete (kitu ambacho siamini kama kweli walikuwa na ubavu huo) kama wallifanya kama alivyofanya Kikwete. Hao hao ndo wamekuwa wakwanza kumfanyia vitimbi. mkuu hebu toka nje ya box halafu jaribu kutafakari ukweli wa haya mambo.
 
Back
Top Bottom