Mh Rais Joseph Magufuli tengua kauli yako tupate mkopo.

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
19,454
25,372
Mheshimiwa rais tafadhari sana nakuomba nipo chini ya miguu yako naomba utengue kauli yako kuhusu wanafunzi wale tuliosoma shule za kulipia kwamba hatupaswi kupewa mkopo.


Mwanzoni kabla ya hili tamko lako jina langu lilikuwa miongoni mwa majina ya wanafunzi watakaonufaika na mkopo ila tu mara baada ya kuongea lile tamko lako jina langu likakatwa na mpaka sasa nasota sana kuhusu suala la mkopo.


Sikukata tamaa nikaamua ku appeal mkopo na nikaambatanisha vitu vyote vinavyohitajika ili upewe mkopo lakini wapi kote nikadunda.

Kwa sasa naishi maisha ya kifukara sana yote hii ni kwa ajili yako mh rais huku wewe na familia yako mkiishi maisha raha mustarehe


Kusoma shule ya kulipia hakumaanishi una pesa sana bali ni jitihada tu za mzazi za kukufanya upate elimu bora mfano wa jitihada hizo ni kama vile kuuza viwanja na nyumba ili tuweze kusoma kwa hiyo ulivyotuhukumu kwamba tuliosoma private ni watoto wa matajiri umetuonea sana tena sana


Kwa sasa ninaishi maisha ya kifukara sana ikiwemo kula mlo mmoja kwa siku na sifurahii kabisa maisha ya chuo na hua nina umia sana pale ninapoona wenzangu wanaenda kusaini ela ya mkopo na ukiangalia wao wana uwezo mkubwa sana wa kipesa kuliko mimi na isitoshe wana mkopo.


Mpaka sasa nimekuwa mtu wa kusearch mitandaoni fursa mbalimbali ili nijikwamue lakini wapi sioni chochote kile


Naandika haya kwa hisia kali sana kwa kukulilia wewe mh rais maana wewe ulituahidi mambo mazuri kuhusu mkopo lakini nashangaa wewe ndio umekuwa wa kwanza kwa kusababisha tusipewe mkopo.


Mh rais tafadhari tengua kauli yako na sisi watoto wa masikini tuweze kupata mkopo na tuweze kuyafurahia maisha ya chuo na tuweze kusoma vizuri

Mpaka sasa sina ada ya chuo mpaka natamani hata nighairishe mwaka .

Natumai ombi langu umelisikia mh rais

Na naomba nitoe rai kwa wanafunzi wenzangu wote wenye tatizo kama hili waweze kushare hii thread kadri wawezavyo kwenye mitandao mbalimbali ya jamii mpaka pale rais atakaopoona uzito wa suala hili maana yeye anachukulia simpo simpo kwa sababu yeye si ana hela bwana kazi kutunyanyasa sisi masikini tusio na kitu.
 
Inauma sana endelea kupambana hivyo hivyo.najua wanaotunzwa na taifa kuanzia chakula hadi mavazi hawawezi kuelewa mateso wanayopata wengine.kazi zao no kukurupuka na matamko ambayo hayajafanyiwa utafiti.pole sana.
 
Inauma sana endelea kupambana hivyo hivyo.najua wanaotunzwa na taifa kuanzia chakula hadi mavazi hawawezi kuelewa mateso wanayopata wengine.kazi zao no kukurupuka na matamko ambayo hayajafanyiwa utafiti.pole sana.
Asante mkuu

Naendelea kupambana hivyo hivyo ila naelekea kujishindwa kwa kweli
 
Mleta Uzi mimi huwa siwaonei huruma maana haya ma'ccm yamewekwa madarakani na wazazi wenu,ila una point,kusoma private haimaanishi wewe tajiri,so ni upungufu wa fikra kunyimwa mkopo kisa ulisoma private
 
Mleta Uzi mimi huwa siwaonei huruma maana haya ma'ccm yamewekwa madarakani na wazazi wenu,ila una point,kusoma private haimaanishi wewe tajiri,so ni upungufu wa fikra kunyimwa mkopo kisa ulisoma private
asilimia kubwa(above 75%) ya wanaosoma private ni wale wenye uwezo wa juu how comes wewe masikini kama mimi ukasome private?
 
Back
Top Bottom