Mh Rais Jakaya Mrisho Kikwete umefanya mengi mazuri jitahidi kufanya hili

emanuel mushi

Member
Aug 14, 2015
19
9
Mh Rais Jakaya Mrisho Kikwete umefanya mengi "mazuri" jitahidi kufanya hili;

Iweke sawa Tume ya Uchaguzi wewe wajua. Pia weka Majeshi yetu yote sawa wewe wajua.

Hivi vyombo visitumiwe kwa NAMNA YOYOTE kukisaidia chama chochote katika Uchaguzi Mkuu ulio mbele yetu.

Kumbuka Mungu wetu Alieziumba Mbingu na Nchi anakutazama wewe kwanza utawasaidiaje Watu wake Unao-waongoza wasipoteze pamoja na mambo mengine UHAI wao.

Najua Unajua kua kila Mtu atasimama peke yake siku ya Ukumu. Mh Una Jaribu (Mtihani) Mkubwa sana, ila jitahidi na Mungu atakusaidia.

Amen!
 
Kweli atafanya hivyo. Ebu tuingie magotini tuombe ili baba yetu asisahau kama Mola yupo na anaona na kusikiliza vilio vya watanzania.
 
Mh Rais Jakaya Mrisho Kikwete umefanya mengi "mazuri" jitahidi kufanya hili; Iweke sawa Tume ya Uchaguzi wewe wajua. Pia weka Majeshi yetu yote sawa wewe wajua. Hivi vyombo visitumiwe kwa NAMNA YOYOTE kukisaidia chama chochote katika Uchaguzi Mkuu ulio mbele yetu. Kumbuka Mungu wetu Alieziumba Mbingu na Nchi anakutazama wewe kwanza utawasaidiaje Watu wake Unao-waongoza wasipoteze pamoja na mambo mengine UHAI wao. Najua Unajua kua kila Mtu atasimama peke yake siku ya Ukumu. Mh Una Jaribu (Mtihani) Mkubwa sana, ila jitahidi na Mungu atakusaidia. Amen!
Kuna kitu unataka kukisema japo unasita. Maadam umeamua kuanzisha thread jikaze tu ukiseme waziwazi au unaogopa UHAI wako.

Kikwete mi ntamsamehe kwa makosa yote isipokuwa upole wake. Ni mpole mno hata kwenye mambo yanayohitaji maamuzi magumu. Angekuwa mkali kidogo tu leo hii chama chake kisingekuwa kinapita kwenye hii tufani kiliyomo. Inaudhi na kusikitisha sana. Right there pua na mdomo kuwa great president halafu anashindwa.

Imagine kama asingeingilia mchakato wa katiba mpya na kuacha katiba waliyotaka wananchi ikapitishwa. Leo hii angeondoka madarakani akiwa amewaachia Watanzania katiba nzuri ambayo ingesaidia kubadilisha mfumo uliopo na kuielekeza nchi katika dira mpya.

Imagine kama angekataa kusaini haya masheria mabovu ya takwimu, makosa ya mtandao, gesi, habari na mengineyo. Ngoja tu niache kwani mpaka napata huzuni. Destined to be a great leader and yet can't grasp the greatness. My president masikini yeye kazi yake kucheka cheka tu, kulalamika na kushusha mipasho...
 
Mkuu kudos,uswahili mno ukizidi ni hasara tupu!!

Kikwete sio visionary leader ila Magufuli ni hovyo zaidi!!

Kikwete anaenjoy zaidi kunyuka suti kuliko responsibilities,angalia tu hata akihutubia,anaweka vzuri hadi mkanda na kuchomekea vzuri,akimaliza then kurusha vijembe,zinafuata shombo kiasi,anashushia na kibwagizo cha kicheko then anasema "ASANTENI SANA KWA KUNISIKILIZA!!"
 
Yote alofanya yamefunikwz na ukiukwaji haki za binaadamu. Kuwaleta masheikh wa uamsho kutoka Znz kuja Dar na kuteswa , kufanyiwa kesi isiyo miguu hata mikono hilo hata waislam wengi walokua wakimtetea anapo simangwa sasa wanamuona kama mtumishi wa watu fulani dhidi ya waislam ...hakika pale kaharibu kila kitu wala hakionekani , vyote vizuri vimeingia doa
 
Mambo ya dini haya mimi huwa siyagusi kwani mijadala yake huwa inahemsha watu sana. Mimi nilidhani kwa kuwa huyu ni Mwislamu mwenzenu basi amejaribu sana kuwaridhisha. Nasikia kahakikisha kaweka waislam katika karibu kila idara nyeti serikalini na katika utawala wake hisia za udini zimefufuka sana. Anyway, inabidi mtambue kuwa yeye ni rais wa wote na anapohisi sheria zinakiukwa mpaka kiasi cha kuhatarisha amani basi inabidi ashughulikie bila kujali imani za wananchi anaowaongoza. Hili likieleweka pengine hata malalamiko ya kuonewa yatapungua. Again, huwa sipendi mijadala iliyoegemea dini period. Haina tija na ni kupoteza muda tu.
 
Mkuu kudos,uswahili mno ukizidi ni hasara tupu!!

Kikwete sio visionary leader ila Magufuli ni hovyo zaidi!!

Kikwete anaenjoy zaidi kunyuka suti kuliko responsibilities,angalia tu hata akihutubia,anaweka vzuri hadi mkanda na kuchomekea vzuri,akimaliza then kurusha vijembe,zinafuata shombo kiasi,anashushia na kibwagizo cha kicheko then anasema "ASANTENI SANA KWA KUNISIKILIZA!!"
Usinipeleke kwenye ushabiki wa kisiasa usio na kichwa wala miguu. Umejuaje kuwa Magufuli ni hovyo zaidi? Ameshawahi kuwa Rais? Mimi nimetoa general assessment ya J.K kwa jinsi ninavyomwelewa - young, charismatic, intelligent but somehow can't grasp the concept of being a great leader na upole wake is one of his greatest weaknesses. Simo kwenye hii mihemko ya CCM vs UKAWA. Ye yote atakayekuja naye tutampima na kumhukumu wakati wake ukifikika. Tuwe na subira hasa ukizingatia kuwa tunaongelea wanasiasa. They are unpredictable and totally untrustworthy.
 
Akisimamia vema uchaguzi ukafanyika kwa uhuru na haki na kisha matakwa ya wapiga kura yakaheshima na aliyeshinda akatangazwa mshindi, akazuia uchakachuaji wa kura ili kufunga goli la mkono, watanzania watamsamehe kwa mapungufu yote katika miaka yake kumi ya utawala, ataheshimika sana ndani na nje ya Tanzania. Kinyume cha hayo atakuwa amemaliza mwendo wake vibaya mno.
 
Mambo ya dini haya mimi huwa siyagusi kwani mijadala yake huwa inahemsha watu sana. Mimi nilidhani kwa kuwa huyu ni Mwislamu mwenzenu basi amejaribu sana kuwaridhisha. Nasikia kahakikisha kaweka waislam katika karibu kila idara nyeti serikalini na katika utawala wake hisia za udini zimefufuka sana. Anyway, inabidi mtambue kuwa yeye ni rais wa wote na anapohisi sheria zinakiukwa mpaka kiasi cha kuhatarisha amani basi inabidi ashughulikie bila kujali imani za wananchi anaowaongoza. Hili likieleweka pengine hata malalamiko ya kuonewa yatapungua. Again, huwa sipendi mijadala iliyoegemea dini period. Haina tija na ni kupoteza muda tu.

Ndugu hili linahusu haki za binadamu , ni bahati tu waonewa ni wailslam . Hapa kuna uonevu . Yeye kuwa muislam kiongozi haina maana yoyote na haki za binaadamu. Hawa jamaa wanateseka kwa kueleza mzimamo wao juu ya muungano tu. waliwamsha wazanzibari juu ya hasara ya muungano , ndio wakafanyiwa fitina na uongo wa kusingiziwa ugaidi. Halihusiani na kusali kwao na kanzu zao
Kwa hili waislam wanamuona mbaya kwani kila kitu kiko wazi mwaka wa pili sasa kesi yao haijaanza wala hakuna nia ya kuanza sijui labda akija lowasa kwa kura za hasira atawatoa na kuwarejesha kwao znz wakaungane na famulia zao.
na sasa kesi inasikilizwa bila ya kuwepo waandishi au jamaa zao kwanini ? Sababu kuu hawataki ukweli ujulikane na raia .Ni kuwanuima haki raia kujua mwenendo wa kesi hii.
Hizi tuhuma zilitolewa mpaka kwenye bunge kwamba hawa masheikh wanadhalilishwa, bunge mpaka leo halipo tena lilishindwa kutoa tamko.
Hivyo kafanya alio fanya lakini kwa hilo la uonevu la kuwaweka watu 20 jela kwa sababu za kisiasa hili waislam wanasahau kama alijenga DART au ameweka waislam kila idara....hasira yao ni oct. 25
 
Back
Top Bottom