Mh. Rais ingilia kati suala la mikopo ya wanafunzi elimu ya juu

Afrikasana

JF-Expert Member
Oct 27, 2021
320
283
Mh. Rais ninakusalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia hongera kwa safari ya Glasgow ambapo uliiwakilisha nchi yetu na kutusemea, pole kwa majukumu ya kulipigania taifa letu.
Nikienda moja kwa moja kwenye mada ni kwamba baadhi ya wanachuo ambao wanakila sababu ya kupatiwa mkopo na HESLB mpaka sasa bado wanaona matumaini kuyeyuka.
Mh. Rais wapo wanachuo ambao wametoka kaya maskini tena niyatima na wameambatanisha kila kitu lakini hawajapewa mkopo. Ukifika bodi kuulizia huruhusiwi kuwaona viongozi unaishia kukaa kwenye hema nje pale na majibu anakuja secretary eti ndio anawapiga kiswahili mara aseme mmekosea kujaza fomu na ukiwapa nakala wakuoneshe ulipokosea wanaishia kukusimanga mbele za watu.

Siku chache zilizopita alienda katibu wa itikadi na uenezi wa CCM ndugu Hamdu Shaka lakini waombaji mkifika hakuna majibu tofauti ya kabla au baada ya yeye kwenda. Wanadai hawasukumwi na watu wa CCM kufanya kazi na eti hawawajibiki kwa Hamdu Shaka.
Mh. Rais ajabu ya HESLB ni kwamba wapo waliotoka familia bora wazazi wao wote wapo na wanasoma kozi zinazofanana na hao mafukara na yatima lakini wanaotoka familia bora baadhi yao wamepewa mkopo. Kwanini yatima na maskini baadhi wanyimwe?
Wapo watumishi wa umma ambao wamepewa mkopo lakini mafukara na yatima wamenyimwa
Hivi HESLB hawajui kwamba wengine hata hiyo hela ya kujaza hizo fomu za bodi wamefanya vibarua au wamesaidiwa?
Mh. Rais wapo waliokata rufaa baada ya kukosa mara ya kwanza lakini pia bado hakuna jipya. Hali ni mbaya sana
Mh. Rais Mkurugenzi wa HESLB bado hajaamua kufanya uchambuzi wakina na wa haki ili kusaidia yatima na maskini wasidhalilike

Mh. Rais HESLB wameamua kukuhujumu wewe na serikali yako kwakuwanyima baadhi ya yatima na maskini tena ambao wengine kaya zao zinasaidiwa na TASAF na viambatanisho wamepewa. INAUMA SANA MH. RAIS .

Mpaka kufikia jana wametoa majina lakini bado yatima leo wameenda kulalamika ila hakuna msaada.Watumishi wa bodi wanachunguliatu kwenye madirisha na milango wala hawaguswi na maisha ya yatima waliojaa pale nje.

Mh. Rais tuma watu wako kwanamna utakavyoona wewe inafaa ili ubaini madudu ya mkurugenzi wa HESLB na timu yake. Fanya SAMPLING kwa vyuo vichache ili kubaini ukubwa wa shida waliyonayo watu wa HESLB na wahitaji waliokosa kusaidiwa.

Mh. Rais waonee huruma yatima wa nchi hii nao wapate elimu ya juu kwa kupatiwa mkopo vinginevyo watarudi nyumbani na kuwa kama vile hawahitajiki katika ujenzi wa taifa letu.
Kabla hawajabeba mabegi kurudi nyumbani,toa kauli yenye uponyaji mama.

Tanzania hii niyawote hivyo yatima na maskini wasibaguliwe katika nyanja zote.
 
Hata ningekuwa mimi Shaka nisingemsikiliza, aende waziri mwenye dhamana.
 
Kwanza kuna mtumishi wa bodi anadai Shaka aliendatu kupiga nao picha hakuna na jipya sana aliloongeza wala kupunguza
Shaka usiwe unaenda kupiga picha tena pale bodi
Kuna ukweli hapo maana matokeo chanya hayajaonekana ndani ya bodi.
Nikweli yatima bado wanalia nyuki. Bila mamlaka za juu kuwala watu vichwa hapo hiyo bodi hawatatenda haki
 
Hata wakati wake huyo Magufuli wapo yatima na maskini walikosa mkopo.
Wapo walioacha vyuo kwa kushindwa kulipa ada.
Hiyo bodi ya mikopo ni ileile haijabadilika menejimenti hata mtu mmoja.
Waziri anayehusika niyuleyule.

Nadhani ni bora iundwe bodi ambayo ina watu waadilifu,wanaoguswa na matatizo ya watu,bodi isiyojaa ubinafsi na ufedhuli,bodi yenye uwajibikaji kwa yatima na maskini.
Ninaamini siku sio nyingi Mh. Rais atafanya kitu maana hao wamefanya hiyo bodi ni yao
Huyo mkurugenzi wa bodi ili awajali yatima ambao nimaskini labda Mh. Rais aende akawabembeleze yeye lakini hawasikii la muadhini wala mnadi swala
 
Back
Top Bottom