Mh. Rais Dr. Magufuli, Uhuru unaotupatia ktk mitandao ni mkubwa mno, sasa tumepinda migongo hata kulea watoto tumewaachia wengine, bana kidogo....

FrankLutazamba

JF-Expert Member
Aug 9, 2018
449
408
Rais Dr. John Pombe Magufuli, tuokoe kwa hili, umetupa Uhuru mkubwa kwani vifurushi vimekuwa chee, hivyo kupelekea muda wote tuwe mtandaoni, kiasi ambacho migongo inauma na watu wengi kuharibikiwa macho.

Kutuokoa ni ama kuruhusu internet iwe Bure kabisa ili watu waone kitu cha kawaida au gharama zipande.

Kwa lugha nyepesi mh. Rais, wewe ni sawa na mzazi anayempenda sana mwanae kila akirudi toka kazini anamletea peremende (Pipi), bila kujua kuwa anamuozesha meno, na siku zijazo mtoto akikua atalazimika ama kuziba meno kwa gharama kubwa au kung'oa na kubaki kibogoyo na lawama kumrudia mzazi kwa matunzo hafifu

Watu migongo inatupinda polepole,sasa najiuliza mh.Rais utupe nini tulizike sina jibu maana Uhuru umetupa,sasa unatumaliza wenyewe kheri utunyooshe tu.

Mwisho nachomekea kabarua kangu nilikoandika 2018 kwa EMS sijui kalikufikia.Ushindi mwema wa kishindo.

NB: Kuna watumiaji wamekili kuwa addicted yaani wanashindwa kujizuia kuingia mtandaoni,wanaingia huku wanalia hawawezi kujizuia hata kwa dakikia tano.
 
Watu wengine mnapenda kutukanwa! Mitandao kwa sasa inahabarisha, inawaunganisha wajasiriamali, nk. Halafu wewe unaleta stori gani tena? Kama binafsi umekua addicted si uachane nayo! Keani imelazimishwa?

Kwa hali hii utamuambia huyo Rais wako atupige marufuku pia kutumia simu, laptop, nk!! Akili gani hii tena!?
 
Back
Top Bottom