Sanctus Mtsimbe
R I P
- Jul 14, 2008
- 1,820
- 1,032
Wana JF Salaam sana
Awali ya wote napenda kutoa pongezi za dhati kwa jitihada zote anazofanya Mh. Rais
za kuleta Maendeleo kwa Watanzania. Imekwisha dhihirika kwa hakika nia yake yeye binafsi ni ya dhati hata kama kunaweza kuwa na mapungufu machache ya kiutendaji. Ninao uhakika baada ya kipindi cha mpito cha kama mwaka moja au miwili, maendeleo hali za neema itaanza kuonekana wazi kwa kila Mtanzania. Naongea haya kama Mtanzania nisiye na mlengo wa itikadi yoyote au ubaguzi wowote. Naongea kama mzalendo na nisiyetarajia maslahi yoyote wala fadhila zozote.
Tanzania ni Nchi yenye rasilimali nyingi sana kushinda hata baadhi ya Nchi ambazo kwa miaka mingi zimekuwa Nchi Wahisani kwa Tanzania (Mfano Nchi za Scandinavia). Utendaji na Usimamizi mbovu pia umekuwa kikwazo kikubwa. Lakini pia ubinafsi na uchu wa kujineemesha kwa kutumia madaraka pamoja na rushwa iliyokithiri ilikuwa pia ni shida kubwa. Pamoja na yote pia ukosefu wa fikra chanya na kiu ya kutaka maendeleo ikiambatana na uthubutu imekuwa siyo jadi ya Watanzania walio wengi. Watanzania wachache ambao wameweza kuthubutu mafanikio yao yameonekana.
Natumaini kuna baadhi ya Washauri na Wasaidizi wa Rais wanasoma JF. Pamoja na jitihada za Serikali zinazoendelea, napenda kutoa mawazo yangu machache ni namna gani hatimaye Tanzania inaweza kuwa Nchi yenye Neema kwa kila Mtanzania.
Mpaka sasa Mwajiri Mkubwa wa Watanzania ni Sekta ya Kazi za Asili kwa maana ya Kilimo; Ufugaji; Uvuvi nk. Hata hivyo uzalishaji katika sekta hii siyo wa kiwango cha juu kuweza kuleta maendeleo makubwa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo: Fikra za kutokukuwa na kiu ya maendeleo na kutaka mabadiliko; hamasa za vitendo toka kwa viongozi; mipango madhubuti; mitaji; usimamizi; masoko na mfumo endelevu.
Miaka ya awali baada ya Uhuru; Hayati Mwalimu J.K. Nyerere alikuwa na ndoto za kujenga Tanzania yenye Neema kwa Kuanzisha Vijiji vya Ujamaa. Hata hivyo hili halikufanikiwa kutokana na sababu kadha wa kadha. Baadhi ya sababu hizo ni maandalizi, usimamizi na umiliki wa wazo la Vijiji vya ujamaa kutokukubalika na wanavijiji, kukosa kujenga uwezo endelevu wa vijiji husika nk.
Kwa sasa vijana wengi sana Tanzania wanakimbilia mijini mara baada ya kumaliza elimu ya Msingi na Sekondari na kuacha Wanawake; Watoto na Wazee vijijini na vijana wachache. Hili kwa kiasi kikubwa ni kutokana na ukweli kuwa namna ya kilimo, ufugaji na uvuvi vinachoendeshwa na wengi havilipi. Asilimia kubwa sana ya ardhi ya Tanzania bado haitumiki ukiacha mambo ya mtazamo wa kisiasa. Sidhani kama hata asilima 10% ya ardhi ya Tanzania imetumika.
Napenda kutoa mawazo machache kwa Mh. Rais na Serikali yake:

- Vianzishwe vijiji maalumu vya Ujasiliamali (Si vya Ujamaa): katika vijiji hivi uzalishaji ufanyike kwa njia ya kisasa. Mfano: Kilimo cha Umwagiliaji; Bustani; Greenhouses; Ufugaji wa Kisasa wa Samaki katika Mabwawa; Ufugaji wa Nyuki; Ufugaji wa Kisasa wa Kuku; Ng'ombe nk nk.
- Serikali ichukue jukumu la kutenga maeneo kwa kuanzia katika kila wilaya ambapo kutakuwa na makazi ya familia zaidi ya 100. Kisha iwekeze katika miundombinu muhimu mfano: Visima virefu vya maji; ili kuhakikisha maji yapo wakati wote. Leo hii Saudi Arabia ni wazalishaji wakubwa wa Tende zinazolimwa jangwani huku waki-export tende hizo. Ukweli ni kuwa katika Jangwa wana visima virefu sana vingine zaidi ya kilometre 1 (1000 metres) chini ya ardhi kusaka maji tu. Na kutokana na maji haya wanaweza kuendesha Kilimo. maji yakipatikana, ufugaji wa samaki, na mifugo mingine pia inawezekana. Hii pia itapelekea kupunguza migogoro ya ardhi isiyo na tija kwani uzalishaji utaongezeka na wengi watajua faida ya kilimo na ufugaji wa kisasa.
- Serikali inaweza kama ikiamua kufanya hivyo kujenga nyumba ndogo na za kisasa na za bei nafuu sana kama 100 kila kijiji ambako kila nyumba inaweza kuwa na wanafamilia watano. Na kukawa na vivutio vichache vitakavyowafanya watu wapende kuishi vijijini kama Community Cente ambapo kutakuwa na TV; Viwanja vya Michezo nk. Pia maeneo ya Ujasiliamali kama Wajenzi; maseremala; mafundi mchundo; mafundi baiskeli, pikipiki nk nk.
- Serikali ya kijiji itenge maeneo ya kilimo; Ufugaji samaki; Nyuki; Mifugo nk katika kiwango cha biashara. Kwa matumizi ya familia kila kaya inaweza kuwa na bustani na mifugo.
- Watu hawa wanaweza kukopeshwa nyumba hizo na wakazilipa katika kipindi cha miaka 10-30 kutokana na uzalishaji katika shughuli zao. Nafahamu hayo ya Serikali kukopesha nyumba yanaendelea katika baadhi ya Nchi kama Rwanda; Namibia nk.
- Serikali isiingilie uendeshaji wa kijiji. Ijenge mfumo tu wa Uongozi na Ujasiliamali. kazi kubwa ya Serikali kwa vijiji vya awali iwe ni kutafuta Masoko ya mazao yao na kujenga mfumo thabiti wa kuhakikisha kuwa mazao yote ya kilimo na ufugaji yananunuliwa katika masoko ya ndani na nje. Wanakijiji wawezeshwe pia kuboresha mazoa yao kwa kuyasindika.
- Wenye uwezo wapewe nafasi ya kujenga nyumba pia na kuendesha shughuli zao Kijasiliamali. Wanaoweza kujenga nyumba nyingi na kupangisha wapewe fursa hiyo.
- Kwa kuanzia Serikali inaweza ikaanza na Pilot Scheme ambapo ikaanzisha vijiji vichache na kuboresha kila mwaka pamoja na kuongeza idadi. Lengo liwe kuwa na vijiji hivi kila kata au zaidi.
- Wakazi wa awali wa vijiji hivi waandaliwe kifikra kwa kuhamasishwa na kufundishwa juu ya kufanya shughuli zao kijasiliamali mfano, ufugaji; kilimo nk. Vijiji hivi vitaendelea kukua. Wachahaguliwe kwa kufuata uwiano wa Jinsia na mambo mengine muhimu yatakayozingatia umoja wetu wa Taifa.
- TBC1 TV na TBC Radio wawe na vipindi maalumu vya kuhamasisha uzalendo na fikra chanya, ujasiliamali na uzalishaji mara kwa mara badala ya vipindi vingi visivyo na tija.Kunatakiwa mageuzi makubwa sana ya vipindi TBC na wahusika ni vema walione hilo.
- Serikali inaweza ikatenga kiasi cha Shs Bilion 300 kila Mwaka kujenga vijiji vya kisasa 30 vya kaya 100 ambayo kila kaya inaweza kuwa na watu 5 (Kila kijiji kukamilika nakisia kiasi cha bilion 10 ila kukamilisha nyumba na miundombinu). Kila Mwaka idadi inaweza kuongezwa.
- Wakazi wa awali wapewe malengo ya uzalishaji na wale watakaoshindwa waondolewe. Kuwe na Wataalamu wa kuweza kuwasaidia kufikisha malengo ya Uzalishaji.
- Mfumo wa uendeshaji wa Kijiji na maisha uwe wa KIJASILIAMALI.