Mh. Pinda tumekukosea nini watu wa lindi na mtwara?

luhombi

Member
Oct 17, 2012
85
19
tokea ushike wadhifa wako mwaka 2008, nimekuwa nikifuatilia utendaji wako wa kazi hususani ziara za kuhamasisha maendeleo na kuwaamsha watendaji waliolala huko mikoani na mawilayani. nilichogundua ni kwamba umejikita zaidi kutembelea katavi na rukwa. ni ukweli usiofichika kuwa hauwezi kaa miezi miwili bila kufanya ziara katika mikoa niliyoitaja. lakini hali imekuwa tofauti kwa mikoa ya lindi na mtwara kwani sikumbuki ni lini hasa ulitembelea mikoa hii.

kumbuka wewe ni waziri mkuu wa nchi yote, hivyo yakupasa utende haki kwa maeneo yote
kumbuka kusini tulishatoa rais lakini hakufanya upendeleo, alitenda haki kwa wote
ni hayo tu.
 
Anajua hayo maeneo yenu hayawaumizi vichwa ccm,
uchaguzi ukikaribia kama kawaida mnapatiwa wali maharage, t.shirt, kofia na kanga mnasahau shida zenu za miaka mitano mnawachagua tena.
Ukitaka kula lazima uliwe.

Hatari:
Weka Mbali na Tembo.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom