Mh. Pinda sasa unapotoka! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Pinda sasa unapotoka!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by YanguHaki, Mar 21, 2011.

 1. YanguHaki

  YanguHaki Senior Member

  #1
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuanzia lini bei ya vitu inashuka kwa kauli ya Waziri Mkuu? Alipohutubia kwenye uwanja wa Mashujaa huko Bukoba aliagiza bei ya sukari ishuke kufikia shillingi 1800 na kabla hajamaliza ziara bei iwe imeshashuka!
  Sasa hapa ndio utata unapojitokeza. Wauzaji wa sukari kwa rejareja mara zote huuza kulingana na manunuzi yao na mara chache sana wao kuwa ndio chanzo cha mfumuko wa bei za bidhaa. Hata faida yao ni ndogo na pia mauzo (turn-over) yao ni ndogo. Ni vigumu wao kulimbikiza bidhaa ili bei ipande waweze kuuza kwa bei kubwa (hoarding) na kupanga bei pia (cartelling). Sababu kuu hapa ni kwamba wapo wengi mno-wapo karibu kila pembe na katikati ya mtaa! Ni vugumu kuwa-organize ili kuwa na msimamo mmoja wa bei.
  Ninachotaka kusema hapa ni kwamba haiwekani kwa muuzaji wa reja reja aliyenunua sukari kwa kilo shs 1800 au zaidi auze tena kwa bei hiyo hiyo kisa eti ni agizo la Waziri Mkuu! Hasara hii atalipa nani? Serikali?
  Mh. Pinda alitakiwa aende mbali zaidi kuchunguza chanzo cha mfumuko wa bei kwa bidhaa mbali mbali nchini-sio kwa sukari tu. Je, ni wazalishaji ama wasambazaji wa sukari? Kama ni wao tatizo ni nini? Lakini pia kuna jambo msingi la kuvutia hapa kila kitu kimepanda tangu Kikwete aingie madarakani. Tazama hapa kwa uchache:
  *Unga ulikuwa shs 300-350 sasa ni shs 650-700
  *Mafuta ya kupikia lita 20 ilikuwa shs 13,500 sasa ni zaidi ya 40,000
  *Mchele 50kg ilikuwa 25,000 sasa ni shs 55,000 n.k
  Serikali iamke sasa! Serikali ihimize kilimo sio siasa za "kilimo kwanza" ambayo sisi wananchi hatujui ni kitu gani! Kama yanashindikana yote Serikali iagize yenyewe bidhaa kwa wingi za vyakula na kuachia usambazaji ufanywe na wafanyibiashara ili kuwapa nafuu ya gharama za maisha kwa wananchi wake.
   
Loading...