Mh. Pinda, Je hili nalo si la kulitolea Kauli/Msimamo

IshaLubuva

JF-Expert Member
Dec 4, 2008
250
11
Hivi karibuni Waziri Mkuu wa JMT Mh. M. K. Pinda alipata shime na kuwataka Wabunge wenye umri mkubwa (Wazee) na wale waliokumbatia majimbo ya uchaguzi na kuyafanya kama ya kwao binafsi waachie ngazi na kutoa fursa kwa damu changa ili nayo iweze kutoa mchango wao katika maendeleo ya nchi hii. Kuna waliojitokeza kumpongeza na wengine kumpinga.

Mimi naona kuna suala jingine nyeti sana ambalo nalo linahitaji kukomesha katika nchi hii. Suala hilo ni la baadhi ya watu kurundikiwa nyadhifa za uongozi kuanzia mbili hadi zaidi ya sita. Utakuta mtu mmoja yeye ni Mkuu wa Mkoa, yeye ni Mbunge, yeye ni mjumbe wa Sekretarieti ya Chama, yeye ni Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Ummma, nakadhalika, nakadhalika; wakati kuna watu kibao ambao hawana ajira.

Suala hili aliliulizwa Lowasa na mtoto mmoja kule Karatu nadhani, yule mtoto alionyesha kuchanganyikiwa kama siyo kukerwa na hali hiyo. Matokeo yake mtoto yule alijikuta matatani.

Nini suluhu ya suala hili, je liachwe likiendelea hivi hivi?
 
Back
Top Bottom