Mh. Pinda, Je hili nalo si la kulitolea Kauli/Msimamo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Pinda, Je hili nalo si la kulitolea Kauli/Msimamo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by IshaLubuva, Feb 6, 2010.

 1. I

  IshaLubuva JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2010
  Joined: Dec 4, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hivi karibuni Waziri Mkuu wa JMT Mh. M. K. Pinda alipata shime na kuwataka Wabunge wenye umri mkubwa (Wazee) na wale waliokumbatia majimbo ya uchaguzi na kuyafanya kama ya kwao binafsi waachie ngazi na kutoa fursa kwa damu changa ili nayo iweze kutoa mchango wao katika maendeleo ya nchi hii. Kuna waliojitokeza kumpongeza na wengine kumpinga.

  Mimi naona kuna suala jingine nyeti sana ambalo nalo linahitaji kukomesha katika nchi hii. Suala hilo ni la baadhi ya watu kurundikiwa nyadhifa za uongozi kuanzia mbili hadi zaidi ya sita. Utakuta mtu mmoja yeye ni Mkuu wa Mkoa, yeye ni Mbunge, yeye ni mjumbe wa Sekretarieti ya Chama, yeye ni Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Ummma, nakadhalika, nakadhalika; wakati kuna watu kibao ambao hawana ajira.

  Suala hili aliliulizwa Lowasa na mtoto mmoja kule Karatu nadhani, yule mtoto alionyesha kuchanganyikiwa kama siyo kukerwa na hali hiyo. Matokeo yake mtoto yule alijikuta matatani.

  Nini suluhu ya suala hili, je liachwe likiendelea hivi hivi?
   
 2. s

  samvande2002 JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2010
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 414
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  yeye mwenyewe PM inabidi aachie ngazi!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...