Mh Pinda, Eti TSh 2bn/- ni Posho ya Kikao ya Vigogo 2? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh Pinda, Eti TSh 2bn/- ni Posho ya Kikao ya Vigogo 2?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Buchanan, Nov 1, 2009.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Nov 1, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Wakati sakata la posho mbili au zaidi kwa kazi moja likiendelea kuchukua sura mpya kila siku huku "mpambanaji" Ole Sendeka akitishia kumharibi Mh Rais Kikwete kwa kuanika mabaya ya serikali endapo kama hataacha suala la posho mbili kwa kazi moja Waziri Mkuu alidai wakati anafungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwamba fedha kinachopata chuo hicho ni kidogo sana, TSh 2bn/-, ambazo amedai ni posho ya vigogo wawili au watatu tena kwa kikao cha ovyo ovyo tu! Jamani suala la posho za vikao liangaliwe, kumbe sio dogo kama wengine walivyodai! Yaani TSh 2bn/- kwa posho ya vigogo wawili watatu? Hivi Serikali hutumia TSh ngapi hasa kwa vikao? Hili itabidi liwekwe wazi kwa kweli!


  Bajeti ya OUT kama posho ya vigogo wawili - Pinda

  Na Salim Said

  WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesikitishwa na kiwango kidogo cha bajeti inayotengwa na serikali kwa ajili ya Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), akisema kiwango hicho ni sawa na posho za vigogo wawili wa serikali, tena kwenye vikao vya ovyo.

  Waziri Mkuu alisema hayo jana wakati akiwahutubia wanafunzi wa jumuiya ya OUT katika mkutano mkuu wa mwaka wa chuo hicho kwenye majengo ya ofisi zake zilizo Kinondoni jijini Dar es Salaam.

  Pinda alisema alikuwa mmoja wa watendaji walioshiriki kupitisha bajeti ya mwaka 2009/10, na kwamba kiasi kilichopitishwa kilikuwa Sh2 bilioni kwa ajili ya shughuli za OUT.

  "Nimemuuliza Profesa Tolly Mbwette bajeti ya mwaka huu ameniambia ni Sh2 bilioni, lakini fedha hii si chochote kwa shughuli zinazoendeshwa chuoni hapa mimi nilikuwa sijawahi kufika na kujionea shughuli za hapa," alisema Pinda.

  "Shilingi bilioni 2 ni sawa na posho za wakubwa wawili au watatu tu serikalini tena katika vikao vya ovyo ovyo tu."

  Alisema licha ya kuwa karibu na OUT kutokana na marafiki zake ambao wengi ni wadau wakuu wa chuo hicho, alikuwa hajui kinachoendelea chuoni hapo.

  Miongoni mwa watu wa karibu na waziri mkuu ambao ni wadau wa chuo hicho ni mke wa wake, Tunu Pinda ambaye ni mwanafunzi, mkuu wa OUT, Samuel Malecela (mbunge), mwenyekiti wa baraza la chuo hicho, Profesa Samuel Wangwe na mama Anne Kilango (mbunge).

  "Nitaishauri serikali kuongeza bajeti ya chuo ili kuhakikisha kwamba inapata fedha nzuri za kukifanya kiwe miongoni mwa vyuo vikubwa duniani. Pia nitawashawishi wadau mbalimbali kuchangia... kwa kweli kazi zinazofanyika ni kubwa," alisema Pinda.

  Panda alifafanua kuwa kumekuwa na mtazamo potofu juu ya elimu masafa na huria (DLO) kwamba si elimu nzuri na inafananishwa na elimu isiyo rasmi.

  Chuo kikuu huria ambacho kina matawi yake karibu mikoa yote nchini Tanzania kinatoa elimu kwa njia huria na ya masafa ili kuwawezesha hata watu waliomo kazini kupata fursa ya kusoma.

  "Ni wajibu wetu serikali, nyinyi na wadau wote wa elimu nchini kuhakikisha kwamba tunaielimisha jamii kuhusu ubora wa elimu ya DLO ili jamii iondokane na mtazamo huo potofu," alisema Pinda.

  "Msikate tamaa wala kuvunjika moyo OUT ni chuo kikubwa nchini tena kizuri na kinachotoa elimu bora, jitahidini na mimi nitazidi kuwashawishi watu mbalimbali kusoma hapa."

  Akijibu swali kuhusu suala la jinsia katika vikao vya maamuzi, Pinda alisema suala hilo linafanyiwa kazi na serikali na kwamba mategemeo yake katika serikali na bunge lijalo uwakilishi wa wanawake utaongezeka hadi kufikia kati ya asilimia 40 na 47.

  "Kwa sasa bungeni wanawake ni asilimia 30 na katika baraza la Mawaziri robo ni wanawake, lakini mategemeo yangu ni kwamba serikali na bunge lijalo uwakilishi wa wanawake utaongezeka hadi kufikia asilimia 47 kwa sababu huenda wabunge wengi wanaume wakaanguka," alisema Pinda.  (Source: www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=15660).
   
 2. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #2
  Nov 1, 2009
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,050
  Likes Received: 3,958
  Trophy Points: 280
  washampiga kipapai huyu! Kwa kuropoka watakuwa wenye vichwa bapa wamemuendea kwa ustaadhi baada ya kukataa Zanzibar si nchi!
   
 3. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #3
  Nov 1, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kaazi kweli kweli!
   
 4. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #4
  Nov 1, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Tehe waendelee kulumbana tu tujue mengi
   
 5. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #5
  Nov 1, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Sure!
   
 6. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #6
  Nov 1, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Hii ndio Tanzania bwana.

  Billioni mbili (2 Bill TZS) ni kifungu maarufu sana pale bungeni:

  "kifungu 1001 mshahara wa waziri"!​

  Ati imetengwa kwa ajili ya chuo kikuu, tena chuo kikuu ambacho bado kinajengwa kwa kuwa hakijakamilika!!!!

  Aaah aaah, wenzetu, watanzania wenzetu ninyi wanasiasa mnatupeleka wapi?
   
 7. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #7
  Nov 1, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Wezi wamo ndani kwa ndani, sisi tunalalamika Richmond na EPA. Hivi vikao wakikaa mara 50 tu, pesa ya EPA hiyo. Kwanza sitashangaa nikisikia na Baraza la Mawaziri linalipwa posho linapokutana! Unajua tunafanana na mtu anayejaribu kujenga ukuta kuzuia wezi kuingia home, huku ndani amejaza mapanya wanaomaliza mtama na chakula ghalani. OVYO KABISA. SITAKI KUSIKIA TANZANIA KWA LEO TENA. Ntarudi hapo kesho hasira zikiwa zimepungua.
   
Loading...