Mh. Pinda ati hajui kama Polisi hawafanyi kazi zao!

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
528
Mh Pinda kaja juu, ati kama Polisi wameshindwa kuzuia uvushaji wa sukari kwa magendo kwenda Kenya, Serikali itatumia JWTZ! Siku mbili baadae Makao Makuu Polisi wanadai kuwa Polisi imejipanga kudhibiti uvushaji wa sukari kwenda Kenya.

Hapa ni usanii mtupu, upande wa Serikali na Polisi. Hivi ni kweli mh Pinda hajui kuwa Polisi wetu ni kama vile wameajiriwa partime na serikali? Polisi wetu muda mwingi hufanya kazi zenye maslahi kwao, wawapo Vituoni, Doria, na Mipakani; Kote huko ni kwa maslahi yao kwanza.
 
kweli kabisa Mheshimiwa, maslahi yao kwanza, ya taifa wakipenda au mpaka wafuatiliwe mienendo yao ya kazi ndio wabadilike kidogo, viongozi wakikaa kimya, wao wanazembea tena, hata watu wengi wanaofanya kazi kwenye ofisi za serikali wana tabia hiyo, Mi nakumbuka polisi waliniudhi sana miaka kadhaa iliyopita kwa kuwa wakali zaidi na majambazi baada ya wenzao I think wawili na mbwa wao kuuawa na majambazi pale Kawe, wakati wananchi wa Mbezi walikuwa wakilalamika kila mara kabla ya hilo tukio kuhusu kero za ujambazi serious kwenye maeneo yao, baada ya hilo tukio Dar palichimbika, majambazi na wageni waliokuwa hawana vibali vya kuishi nchini walikiona cha moto, nashindwa kuelewa kwanini leo hii pia wasiwe wakali kama kipindi kile, wawe wakali ipasavyo siku zote wananchi wanapodhuriwa na mali zao kuporwa sio mpaka majambazi wakiwadhuru wao au familia zao, it's not fair.
 
Pinda kuna kipindi anachemka, hajui ili jeshi la wananchi litumike ni mambo gani inabii yajiri! Pia amewadhalilisha polisi kuwa si watendaji bali ni watu wa maslahi hata kama hili lina ukweli lakini yeye kama PM alitakiwa alichuke kama changamoto
 
Back
Top Bottom