Mh. Pinda ameulizwa swali la msingi kabisa kutoka kwa Mh. Mbowe leo hii katika kipindi cha maswali na majibu, je ? uoni kuwa tume ya bunge itakayoundwa itashindwa kufanya kazi kwa sababu Jairo tayari amekwisha rudishwa kazini ? na akaulizwa pia kama kauli iliyotolewa na katibu mkuu Luhanjo juu ya utaratibu wa kukusanya pesa kutoka kwenye idara zake ni halali ? akajiumauma, inamaana tamko lake la kwanza kuhusu kumfukuza Jairo arikurupuka ?