Mh. Pinda anaposhindwa kujibu maswali mepesi

jnuswe

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
1,270
549
Mh. Pinda ameulizwa swali la msingi kabisa kutoka kwa Mh. Mbowe leo hii katika kipindi cha maswali na majibu, je ? uoni kuwa tume ya bunge itakayoundwa itashindwa kufanya kazi kwa sababu Jairo tayari amekwisha rudishwa kazini ? na akaulizwa pia kama kauli iliyotolewa na katibu mkuu Luhanjo juu ya utaratibu wa kukusanya pesa kutoka kwenye idara zake ni halali ? akajiumauma, inamaana tamko lake la kwanza kuhusu kumfukuza Jairo arikurupuka ?

CAG alisema kwamba utaratibu wa kuchangisha fedha za kuwasilisha bajeti ni wa kawaida. Japo hili linashangaza kwani kila Wizara huwa na bajeti ya kuwawezesha kuandaa na kuwakilisha bajeti.
Pinda ni Mwoga mno! Ameshaonja utamu wa Ufisadi anaogopa kumwaga unga.

Yule Mwanamuziki wa Kenya aliyeimba ule wimbo wa JK Kigeugeu, Pinda Kigeugeu, anaitwa nani vile!

Wewe unaleta habari za uzandiki hapa. Pinda ameshatoa tamko kwamba Jairo kasimamishwa kazi tena, au unafikiri TV unayo wewe tu?

Ameshachoka. Kwahiyo msimshangae kujibu maswali nusu nusu.

Wewe unaleta habari za uzandiki hapa. Pinda ameshatoa tamko kwamba Jairo kasimamishwa kazi tena, au unafikiri TV unayo wewe tu?
Itafika wakati tutawashuhudia hawa viongozi wetu wakiwa wanatoa matamko tofauti yanayojikanganya kila siku.

Baada ya Kumaliza kufuturisha mwezi huu ukiisha sijui ratiba JK inasemaje! Kwa anayempangia ratiba plizzz!!!!

Huyu baba wa watu amekuwa demoralised mno amefanywa kama dampo la kutupia uchafu wa serikali na anatolewa kafara mara nyingi na hivyo amepoteza kabisa confidence na anaposhindwa kujibu maswali ni sahihi kabisa. Hapo ajui ni bomu gani tena litamwangukia kutoka kwa mzee wa kutokota!!!!!

CAG alisema kwamba utaratibu wa kuchangisha fedha za kuwasilisha bajeti ni wa kawaida. Japo hili linashangaza kwani kila Wizara huwa na bajeti ya kuwawezesha kuandaa na kuwakilisha bajeti.

Pinda ni Mwoga mno! Ameshaonja utamu wa Ufisadi anaogopa kumwaga unga.

Yule Mwanamuziki wa Kenya aliyeimba ule wimbo wa JK Kigeugeu, Pinda Kigeugeu, anaitwa nani vile!

Anaitwa Jaguar.

Simply he was supposed to resign,majibu ya ovyo-ovyo na ya kusikizia/kupima upepo.
PM anaogopa

Wewe unaleta habari za uzandiki hapa. Pinda ameshatoa tamko kwamba Jairo kasimamishwa kazi tena, au unafikiri TV unayo wewe tu?

Unafikiria kwa tumia masaburi na tundu lake..Pinda kashindwa kujibu kwamba ni utaratibu wa kawaida kwa makatibu kuchangisha pesa kufacilitate kupitisha bajeti? Na kama ni kawaida, kilichomfanya ajifanye kashtuka siku ile hoja ya Jairo ilipowasilishwa ni kitu gani?

Tatizo ni tuna rais kikwete kilaza,na waziri mkuu pindamsomi mwanasheria.ingekuwa rais msomi mkapa na waziri mkuu kilaza sumaye ilikuwa sio mbaya,maana rais kichwa anaficha ujinga wa waziri mkuu!lakini ukiwa na rais kilaza hali huwa ni ngumu sana!

CAG alisema kwamba utaratibu wa kuchangisha fedha za kuwasilisha bajeti ni wa kawaida. Japo hili linashangaza kwani kila Wizara huwa na bajeti ya kuwawezesha kuandaa na kuwakilisha bajeti.
Pinda ni Mwoga mno! Ameshaonja utamu wa Ufisadi anaogopa kumwaga unga.

Yule Mwanamuziki wa Kenya aliyeimba ule wimbo wa JK Kigeugeu, Pinda Kigeugeu, anaitwa nani vile!
Please mkaguzi mwingine yeyote hata mwanafunzi aseme kama kulikuwa na best practices pale, independence of theaudit! Halafu kwa nini walimsimamisha? turejee kwenye sababu ya msingi, hizo porojo na michezo ya kuigiza intutuia aibu hata sisi tulio nje,Halafu Ngereja kaenda rasmi kumpokea na kumkumbatia, kweli tunahitaji busara ktk uongozi, huyu kijana ameshindwa kupima ni wapi anatakiwa awepo na kwa wakati gani? Wrong time, wrong place! nafikiri sasa anakaribia ku-resign!.

mizengwe pinda ni mbunge wa ccm kwa hiyo na yeye ni kama ze comedy(according to jairo comments) na anafikiri kwa kutumid masaburi yake badala ya kichwa

Maswali yangu nayafanyia kazi, Waziri mkuu kazi yake ni nini na je ana mamlaka kwa nani? Je Makatibu na mawaziri wanariport kwa nani direct? Je anaweza kumwajibisha mtu? Mbona Lowassa alikuwa anawatimua kazi immediately? Je tuseme Pinda anaogopa au ni mzee wa democracy sana?

Natamani jf ingekuwa ndio bunge, maana inashirikisha wananchi wengi na hoja zinajadiliwa kwa uwazi, hiyo tume ingeomba maoni na ushauri kutoka humu jamvini

Natamani jf ingekuwa ndio bunge, maana inashirikisha wananchi wengi na hoja zinajadiliwa kwa uwazi, hiyo tume ingeomba maoni na ushauri kutoka humu jamvini

Ikitokea hivyo basi nchi itasambaratika kabisa, maana kuna watu humu
wana mawazo ya ajabu sana kuliko hata ya... ah, nimesahau nilitaka kumtaja nani!

Wewe unaleta habari za uzandiki hapa. Pinda ameshatoa tamko kwamba Jairo kasimamishwa kazi tena, au unafikiri TV unayo wewe tu?

ndo tatizo la kutosoma between lines, suala la msingi hapo ni kiongozi kutokuwa na msimamo, kama umesoma shule walimu wako walipata taabu kukuelimisha na bado hujaelimika kama unaweza ukawa upande wa kiongozi dhaifu wa kufanya maamuzi na kutokuwa na msimamo

kweli tunapochagua Rais kilaza ndio matokeo yake haya. sasa tufanyeje? tumfukuze kazi :hungry:

Back
Top Bottom