Mh.Ole sendeka, hoja binafsi kutaka nyumba za serikali zilizouwa zirudishwe.Tunasubiri utekelezaji

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Katika bunge la mwezi November mwaka jana kama sikosei,mh.Ole sendeka ulitoa ahadi ya kupeleka hoja binafsi bungeni ukitaka nyumba za serikali zilizouzwa zirudishwe.Mh.ulikwenda mbali zaidi na kukiri kuwa ktk mambo ambayo serikali yako ya ccm ilikosea ni kuuza nyumba za serikali.Hata hivyo,nahofia kukubalika na kupitishwa kwa hoja hiyo kwani hata huko bungeni wapo wengi waliofaidika na uamuzi huu.

Ombi langu kwako, timiza ahadi yako na umma wa watanzania walio wengi wako nyuma yako.Itakuwa ni nafasi ya umma kujua ni mbunge yupi yupo kutetea wananchi na yupi yupo kwa maslahi yake binafsi.Pia naamini utaandika historia ktk hili.

Athari ya uamuzi huu ni kumuongezea ugumu wa maisha mtumishi ambaye mshahara wake hautoshelezi mahitaji yake kwa kumlazimisha kupanga mitaani, tena kwa kodi kubwa wakati nyumba zilikuwepo.Uamuuzi huu ulinufaisha wachache kwa gharama ya wengi.
 
Mhhh sijui mheshimiwa JK atasemaje kuhusu hili. Kama kweli JK angekuwa muadilifu na mtu mwenye kujali maslahi ya
wananchi wake, angeikataa ile nyumba. Kwa sasa imekwisha badilishwa sura, kwa maana nyingine Ole Sendeka et al mlie tu kuhusu zoezi hili.
'' NYUMBA HAZIRUDI NG'OOOOOOOO
 
na asimame basi Ole Sendeka apate kuhesabiwa kuwa yeye ni panya aliiyehubutu kumvika paka kengele,COME WHAT MAY!
 
Sijui Ole Sendeka atapendekeza utaratibu gani utumike kurudisha hizi nyumba (kama kweli atawasilisha hoja yake bungeni) kwa sababu nyumba nyingi zilizonunuliwa zimebolewa na kujengwa majengo mengine kabisa. Sasa, nini hasa kitarudishwa? na kama kutakuwa na fidia serikali ina hela?
 
Katika bunge la mwezi November mwaka jana kama sikosei,mh.Ole sendeka ulitoa ahadi ya kupeleka hoja binafsi bungeni ukitaka nyumba za serikali zilizouzwa zirudishwe.Mh.ulikwenda mbali zaidi na kukiri kuwa ktk mambo ambayo serikali yako ya ccm ilikosea ni kuuza nyumba za serikali.Hata hivyo,nahofia kukubalika na kupitishwa kwa hoja hiyo kwani hata huko bungeni wapo wengi waliofaidika na uamuzi huu.

Ombi langu kwako, timiza ahadi yako na umma wa watanzania walio wengi wako nyuma yako.Itakuwa ni nafasi ya umma kujua ni mbunge yupi yupo kutetea wananchi na yupi yupo kwa maslahi yake binafsi.Pia naamini utaandika historia ktk hili.

Athari ya uamuzi huu ni kumuongezea ugumu wa maisha mtumishi ambaye mshahara wake hautoshelezi mahitaji yake kwa kumlazimisha kupanga mitaani, tena kwa kodi kubwa wakati nyumba zilikuwepo.Uamuuzi huu ulinufaisha wachache kwa gharama ya wengi.

Waserikali watu wasokuwa na huruma kwa wenzao hata chembe. Nyumba za Serikali walikuwa wakikaa wao, wakauziana wao kwa wao tena kwa bei ya kutupwa na mwishowe wakazinunua kwa kutumia fedha zetu sisi walipa kodi
 
Mh.Ole sendeka narudia tena ombi langu kwako tunaomba utekeleze ahadi yako uliyoitoa bungeni.Taarifa kwenye gazeti moja la kingereza la jana kuwa waziri Tseba anaishi hotelini tangu apewe wadhifa huo mwezi may mwaka jana na gharama halisi anazolipiwa na serikali zimenichefua kama sio kutonesha kidonda na ndio maana leo hii nimekumbuka ile ahadi yako.

Kama umeshindewa au umekwama ni vema ukasema hadharani kama jinsi ulivyotoa ile ahadi yako kwa umma kupitia bungeni.

Mh.ahadi ni deni.
 
Mkuu ile ilikuwa danganya toto, kunataarifa kuwa jamaa alidandia hoja baada ya kuvuja kuwa wabunge wa CDM wanajiandaa kupeleka hoja binafsi ya kuzirejesha nyumba za watanzania...lengo kuu ilikuwa kuzima hoja wala si kupeleka hoja kwa manufaa ya watanzania...
 
Mkuu basi atakuwa mnafiki mkubwa.
 
Sijui Ole Sendeka atapendekeza utaratibu gani utumike kurudisha hizi nyumba (kama kweli atawasilisha hoja yake bungeni) kwa sababu nyumba nyingi zilizonunuliwa zimebolewa na kujengwa majengo mengine kabisa. Sasa, nini hasa kitarudishwa? na kama kutakuwa na fidia serikali ina hela?
fedha zilizoficha uswis,zkirudisha zitumike kurudisha nyumba za serikali,na nitaomba iwe ilani ya chadema kuanzia sasa mpaka 2015
 
Sijui Ole Sendeka atapendekeza utaratibu gani utumike kurudisha hizi nyumba (kama kweli atawasilisha hoja yake bungeni) kwa sababu nyumba nyingi zilizonunuliwa zimebolewa na kujengwa majengo mengine kabisa. Sasa, nini hasa kitarudishwa? na kama kutakuwa na fidia serikali ina hela?
fedha zilizofichwa uswis zitumike kurejesha nyumba za serikali,hiyo ni sera ya chadema
 
Mh.Ole sendeka narudia tena ombi langu kwako tunaomba utekeleze ahadi yako uliyoitoa bungeni.Taarifa kwenye gazeti moja la kingereza la jana kuwa waziri Tseba anaishi hotelini tangu apewe wadhifa huo mwezi may mwaka jana na gharama halisi anazolipiwa na serikali zimenichefua kama sio kutonesha kidonda na ndio maana leo hii nimekumbuka ile ahadi yako.

Kama umeshindewa au umekwama ni vema ukasema hadharani kama jinsi ulivyotoa ile ahadi yako kwa umma kupitia bungeni.

Mh.ahadi ni deni.
na akifika bungeni wakimuuliza fedha zitatoka wapi? aseme zitumike zilizofichwa uswis
 
Back
Top Bottom