Mh. Ndugai, Wabunge wetu walituwakilisha kutoka nje | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Ndugai, Wabunge wetu walituwakilisha kutoka nje

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tuko, Feb 9, 2011.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Feb 9, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Mh Ndugai pamoja na wenzako fulani inaonekana uliumia sana wabunge wetu walipotoka nje wakati rais anahutubia. Leo naibu spika amesema eti wananchi waliowatuma wabunge hao kuwawakilisha bungeni walikerwa pia kwa wabunge hao kutoka bungeni. Napenda nimuambie Ndugai kuwa kwa usahihi kabisa hicho ndicho tulichowatuma wabunge wetu hawa wapendwa kukifanya. Tena kwangu ningewakilishwa vizuri zaidi kama mmoja angemrushia kiatu.
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Hana hoja huyo achana naye aendelee kubwabwaja tu lakini ujumbe ulifika!
   
 3. F

  Froida JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Haijioni yeye kwamba anaipeleka Tanganyika Kuzimu kwa kuipalilia ndoa ya CCM na CUF Zanzibar kutoka nchi jirani Ya Zanzibar yenye bendera ,wimbo wa Taifa,Raisi,Makamu wa Raisi Baraza la wawakilishi badala ya kuacha kanuni zilizowekwa katika bunge la tisa ili kuweka sawa kwa Wabunge wa Tanganyika kuweza kuwemo kwenye upinzani,leo wapinzani wa bunge la watanganyika wananyanyswa kwa sababu Spika na naibu spika wake wanataka kuwafurahisha wake zao wanaotoka nchi jirani ya Zanzibar siku moja Ndugai itakuja kuelewa kwa nini Chadema wanasimamia haki
   
 4. M

  MMASSY JF-Expert Member

  #4
  Feb 9, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 225
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Nimekuwa nikiwauliza rafiki zangu kuhusu mwendo na mwelekeo wa bunge hili la kumi sikupata jibu la moja kwa moja.
  Ndugai ambaye ni naibu spika na mbunge mtiifu kwa sisiem asiye na meno na aliyewekwa kwa ajili ya kusaliti taifa,jana ndiye aliamua kuhutubia bunge kama vile anahutubia kikao cha wanamipasho wa ccm makao yao makuu,akalitumia jukwaa lake hilo kuhalalisha ndoa yao na CUF huku Nccr na Tlp wakifanywa vimada na kushangilia kwa nguvu zote,wakafanikisha kufitinisha kanuni za bunge,wakati wa kuhitimisha akashirikiana na Spika wa mafisadi kukandia wabunge werevu na kugeuza tena bunge kugharamia ndoa ya ccm na cuf,leo asubuhi kupitia TBC Ndugai huyuhuyu akarudi na hoja ileile na kuwashtaki wabunge wa CDM kwetu.Jibu letu ni moja tu kwamba Tunawaunga mkono wa dhati wabunge wetu makini wa CDM.Ndugai huyu akiwa anahitimisha kikao cha bunge katuasa Wananchi kuwatosa wabunge wakini wa CDM.Tunasema na kusisiza kuwa tupo pamoja sana na wabunge wetu makini na mwaka 2015 ni mwaka wa kuwaadhibu nyie wa ccm na cuf mnaotumia muda na kodi zetu kurembesha ndoa yenu haramu na kuchakachua kanuni za bunge kwa maslahi yenu.Mjue hizo kanuni zinageuka kuwabana nyie 2015.
   
 5. F

  Froida JF-Expert Member

  #5
  Feb 9, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  ni vizuri kuanza kutoa adhabu mwaka 2012 ukingoja 2015 utakuwa umechelewa
   
 6. z

  zamlock JF-Expert Member

  #6
  Feb 10, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  hivi wewe naibu spika wa bunge unajua unazungumza na wananchi wa kisasa siyo wale mliowazoea sisi ni watafiti wa mambo hasa kutoka kwenye mabunge ya nchi mbalimbali na tunajua nini tunafanya wabunge wetu walichokifanya ni sahihi na tuko nao pamoja mtafute wa kuwaambia hayo mnayozungumza ila sisi na cdm ni kama pete na kidole
   
 7. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #7
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Tatizo hajui tulichowatuma, sasa anajifanya kama mganga wa kienyeji.... kama wao walitumwa kwenda kuiba na kuvuruga sisi tuliwatuma kwenda kusimamia haki!!!:coffee:
   
 8. S

  Selungo JF-Expert Member

  #8
  Feb 10, 2011
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mh. Ndugai asitake kuwasemea wananchi. Yeye kama naibu spika, kitendo cha Waheshimiwa Wabunge wa CHADEMA kutoka nje ya ukumbi wa bunge, akiwa ni kiongozi wa bunge, hawezi kukifurahia kabisa. Kwani tayari anajuwa CHADEMA imeweza kuujulisha umma wa watanzania ni jinsi gani kwa sasa bunge linavyotumiwa na viongozi wa chama kilichoko madarakani kuwakandamiza na kuwanyima haki watanzania.

  Hawezi kufurahia tukio lile ambalo kwetu watanzania tunaliona ni la kichujaa ukizingatia ni njia mojawapo sahihi na ya kiungwana kuonyesha hisia zako za kutokukubaliana na jambo fulanai. Au Mh. Ndugai alitaka pendekezo la Mbunge wa Mtera la kupigana ngumi ndiyo liwe sahihi kuonyesha kwamba CHADEMA hawakubaliani na angena ya kubadilisha kanuni za bunge, ambazo dhahiri zinalenga kukandamiza haki ya chama fulani?

  Kwa sisi watanzania ambao tumechoshwa na hali hii, tunapenda kumueleza Mh. Ndugai kwamba, kitendo kile tunakiunga mkono kwa dhati na kwetu ni ushujaa uliotukuka. Kuliko kushiriki katika kukandamiza haki za watanzania ilikuwa vyema na busara Wabunge wa CHADEMA kutoka nje. Tunalikubali kwa dhati tukio lile, tunaomba pale Wabunge wa CHADEMA wanapoona kuna uhalali wa kufanya hivyo wasisite. Na zaidi wasiishie hapo, warudi kwa wananchi na kuwaeleza/kulishitaki bunge kwa kile kilicho fanyika.

  Nawasulisha.
   
 9. F

  Fenento JF-Expert Member

  #9
  Feb 10, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 320
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mh. Ndugai tunaomba ufahamu kuwa sisi wananchi watanzania daima tutawasapoti wabunge wa CDM kwa ujasiri wao na tunawaombea kwa Mungu waendelee na ushujaa wao hadi kieleweke. Mh.Ndugai huwezi kutufumba macho kwa vile sisi tunaona...,tunatafakari....kama unataka mteja wa kumdanganya basi uende jimboni kwako ukawandanganye wale ulio wadanganya wakakupa kuwa Mh.
   
Loading...