Mh.Ndalichako umejiandaaje na kuvuja kwa mitihani ya form four

herewego

New Member
Oct 16, 2016
1
0
mheshimiwa waziri wa elimu kwanza hongera kwa kazi unayofanya ili kuboresha elimu yetu ila kwa kifupi sana kungoja nikwambie kinachoenda kufanyika kwenye mtihani huu ambacho kimsingi kimekuwa kikifanyika kwa mda mrefu sana kwa shule zetu.
Mheshiwa ili kuipotosha kasi ya serikali yetu ionekane iko vema kuna mpango mkakati wa kuiba mitihani ya kidato cha nne ili kupata sifa mkuu sijui kama jambo hili linabaraka kutoka kwenu au la maana sasa linafanyika kama jambo la kawaida kabisa
iko hivi mitihani siku hizi haivujii halmashauri au baraza kama zamani kama iko hivo basi ni kwa sehemu siku hizi mitihani inavujishiwa ndani ya chumba cha mtihani yani msimamizi anakuwa amekwisha pewa pesa na mkuu wa shule ili aachie baada ya kufungua mitihani mtihani mmoja huchukuliwa na kukabidhiwa kwa mwalimu wa somo husika katika shule ambapo yeye huchukua vitabu vya somo husika na kuufanya mtihani huo kwa saa moja maana ana nyenzo kisha anarudisha majibu darasani ambapo wanafunzi hutumia masaa mengine mawili au chini ya hapo kujaza majibu na kisha kukusanya paper
mheshimiwa ni zaidi ya uchafu ambao hufanywa na wakuu wa shule kwa kushirikiana na walimu wengine ili kufanikisha mpango huu muovu sana na kwa mwaka huu tayari jambo hilo limekwisha pangwa na litafanyika kama hutaweza kuzuia basi jua hakuna cha top 10 wala last ni wizi tu ambao umehalalishwa ili kuwapumbaza nyie
Mh.watoto hawasomi watoto hawakeshi tena maana paper sio tu kwamba zitavuja wakapewa nafasi ya kusaidiana ni watakaa chini na kungoja mwalimu alete baada ya kusolviwa kwa sasa ni bangi na beting basi
 
Back
Top Bottom