Mh. Ndalichako, umebariki huu wizi wa HESLB na NACTE/TCU?

Kaveli

JF-Expert Member
Dec 4, 2012
4,207
2,000
Heshima kwenu wanaJF wote.
Poleni kwa majukumu ya kila siku ndani ya gurudumu la 'hapa kazi tu' linalopaa kwa mwendo kasi, japo limejaa 'chenga za Pele'! Inshaallah life goz'on kimazabe.

Current guidelines ya HESLB juu ya utoaji wa MIKOPO inaeleza kwamba ni lazima muombaji, pamoja na vigezo vingine, awe kwanza ameshapata ADMISSION ya chuo.

Nanukuu kutoka kwenye guideline hiyo: ''Applicant must have been admitted to an accredited Higher Education Institution, as a candidate for Undergraduate Degree or Postgraduate Degree on full time basis, through the Central Admission System (CAS) or other accepted systems, in programmes recognized by TCU and NACTE.''

Na kwa mujibu wa tovuti ya HESLB, uombaji wa mkopo ulifunguliwa wazi kuanzia tarehe 27 Juni 2016 hadi tarehe 31 Julai 2016 .

CHA KUSHANGAZA SASA, mpaka leo hii tarehe 20 Julai 2016 (only 10 days towards the deadline ya HESLB), bado NACTE hawajatoa selection ya waliopata admissions (wale waliofanya applications hivi majuzi)! TCU nao pia hata kufungua application process tu bado!

Hii inamaanisha nini, watu waombe mikopo kabla ya kujua admission status zao? Yaani mtu akamuliwe Tsh. 30,000 ya Loan Application Fee (non-refundable) wakati hajajua au hana uhakika wa Admission ya chuo??!!

NACTE, TCU, HESLB... acheni hii janja ya kuwaibia wananchi. HESLB should extend the deadline ili kusubiri NACTE/TCU kutoa Admissios. Hizi ni taasisi ambazo zina closer linkage kwenye utendaji, lakini inashangaza sana wana-operate utadhani kila taasisi ipo sayari tofauti ama wanashirikiana kimkakati 'kuwapiga' wananchi. shame! Acheni huu utapeli nyie watu, au nalo hili mnangojea mpaka Rais Magufuli aseme??!!

Mama Ndalichako, tafadhari sana mkuu, rekebisheni hiki kitu!

Watanzia wengi ni masikini, ifike mahali tukemee huu upuuzi wa hizi taasisi zetu. Huu ni wizi kabisa na unyonyaji wa hali ya juu! Watanzania sijuwi tumerogwa na nani sie !

Hili ni moja ya maajabu ambayo mara nyingi sana hunifanya nijiulize kwamba... je hapa duniani, kuna nchi nyingine yenye maajabu kama Tanzania ? Huwa nachoka sana!

-Kaveli-
 

Kaveli

JF-Expert Member
Dec 4, 2012
4,207
2,000
Asante Kaveli,God bless you


Mkuu inasikitisha sana. wananchi wanaibiwa wazi wazi halafu hakuna hata kiongozi wa kukemea. Yani hili nalo eti mpaka wananchi wakalalamike kwa Mh Rais.

Unalazimishwa (kwa deadline) kuomba mkopo wakati hujajua status ya Admission chuo. Hii hata mwendawazimu hawezi kuelewa!

Ni wizi tu wa kuforce.
 

Mbekenga

JF-Expert Member
Jun 14, 2010
1,737
2,000
Ujue kuna watu walishaweka kanuni kwamba akiajiriwa cha kwanza in kupiga dili. Watu wa namna hii wana mtandao mkubwa ambao in kizazi Fulani kit aka chaotic humus muda kukiangamiza.
 

Kaveli

JF-Expert Member
Dec 4, 2012
4,207
2,000
Ujue kuna watu walishaweka kanuni kwamba akiajiriwa cha kwanza in kupiga dili. Watu wa namna hii wana mtandao mkubwa ambao in kizazi Fulani kit aka chaotic humus muda kukiangamiza.


Mkuu, kwahiyo tuendelee kuvumilia wizi wa wazi kabisa kama huu kusubiri mpaka hicho kizazi cha wapiga dili kiishe? Basi safari bado ni ndefu sana kumsaidia mwananchi masikini.
 

Kaveli

JF-Expert Member
Dec 4, 2012
4,207
2,000
Ni zaidi ya elf30 coz lzma utume kwa EMS.


Halafu kwa umakini wa waziri wa elimu, inashangaza nayeye kaufumbia macho huu wizi wa hizi taasisi.

Haiwezekani mtu aombe mkopo wakati bado hajajua hatima ya Admission chuo. Nchi hii ina mambo ya kijuha sana.

Ni wazi kabisa kuwa huu wizi umesukwa na taasisi zote tatu... HESLB, NACTE, na TCU. Pengine hata Wizara inahusika kwenye uhuni huu.
 

Kaveli

JF-Expert Member
Dec 4, 2012
4,207
2,000
Tunakoelekea ni wapi???mi sielewi na wala sioni mbeleni


Kwakweli Mkuu bado ni giza totoro. Kila idara ni upigaji tu.

Eti mtu analazimika kuomba mkopo wakati bado hajuwi kama atapata admission chuo.

Haingii akilini hata kidogo.
 

kasigazi kalungi

JF-Expert Member
Dec 22, 2013
3,881
2,000
Hicho kipengele ulichokiweka cha applicant should be adimitted to accreditted institution ni kwamba ili uje kupewa mkopo kama umekidhi ni pale utakopokuwa umeshapata chuo tayar, kitu ambacho unakuwa una uhakika nacho tayari. TCU washatoa minimum entry points kwa wa form VI na diploma hivyo kama unazo una uhakika wa kupata chuo then unakuwa na uhakika wa mkopo. So bodi ya mkopo hawajakosea kitu.
 

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
8,608
2,000
Halafu ni wizi wa mchana kweupe! Mchakato unaeleweka! Udahili wa TCU unapaswa kuanza, baada ya udahili utolewe muda wa kuomba mkopo kwa waliopata udahili!
 

kamwamu

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,653
2,000
Mambo yanayofanyika ndivyo sivyo katika nchi hii ni mengi sana. Hayarekebishiki kwa mwaka mmoja. Huu ni wizi wa mchana na wa siku nyingi. Heslb wanasema uwe umepangiwa chuo ndio uombe mkopo. Lakini fomu za mikopo hakuna sehemu inapojazwa kozi na chuo! Japo matokeo tayari lakini vyeti bado. Kifupi ni vurugu na wizi wa kidola.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom