Afyayaakili
JF-Expert Member
- Sep 12, 2012
- 923
- 1,255
Wanafunzi waliochaguliwa scholarship za Mozambique mwaka wa masomo 2015/16 mpaka sasa hawaeleweki wataondoka lini au ndio zishaota mbawa maana walitakiwa kuondoka mwezi wa 2/2016 lakini mpaka leo wanapewa majibu yasiyoeleweka na wizara kwa kutokuelewa kuwa wataondoka au ndio basi tena. Wenzao waliopo vyuo Tanzania waliodahiliwa pamoja na TCU wanaingia semister ya 2 sasa huku wao hawaeleweki. Tunaomba wizara ya elimu kutupa majibu rasmi kama hatuendi au tuanze mikakati ya ku apply mwaka huu maana tunashindwa kuanza kufanya mambo mengine tukijua tunaondoka ila kila siku mambo yapo kimya.