Mh. Mwakyembe,treni mbona tena leo halisimami kamata?

NusuMutu

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
421
0
Salaam ewe mheshimiwa! Pole kwa majukumu (yako pamoja na ya wale wanaolala na kukusubiri ufikirie badala yao). Treni la mjini aka treni la Mwakyembe lishaanza kuboa wateja hasa wa maeneo ya kariakoo na maeneo jirani maana linatoka posta limejaa pomoni na kutuaacha 'wananchi' macho kodo. Dereva wa treni alikua anatoa mkono kama wafanyavyo madereva wa daladala kuashiria 'nyomi' kwamba watu wamejaa. Mheshimiwa hebu tena waambie na uwaagize TRL nini cha kufanya maana akili zao ziliishia kwenye lile agizo lako la mwisho, pia mvua zaja, stend za hili daladala treni halina pa kujikinga patakuwa hapatoshi mkuu!
 
Joseph

JF-Expert Member
Aug 3, 2007
3,521
1,225
Ndio taabu ya sisi watanzania kukurupuka na kutafuta suluhisho la muda mfupi bila kufanya utafiti wa kutosha kabla hatujafanya uamuzi,kuanzia Mwakyembe na wote walioshiriki kwenye mchakato wa kuanzisha usafiri huu akili zao zilifikiria karibu sana badala ya mbali maana kwa jinsi wakazi wa Dar es salaam wanavyopata shida ya usafiri ilifaa kujiandaa vema kwa kuweka mabehewa ya akiba kama kutatokea kuwa na ongezeko la wananchi kusafiri na treni,badala ya kutatua kero tunazidi kuongeza kero kwa wananchi

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
10,811
2,000
Suluhisho waongeze mabehewa maana yaliyopo yameshazidiwa na umati mkubwa watu wanaopandia stesheni na kariakoo....maana kuongeza muda hadi usiku zaidi ni hatari pia kwa usalama wa wasafiri vibaka wengi sana
 
jamii01

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
1,889
2,000
mwenzeni niko ukimbizini kila baada ya dakika 3 inapita tren najipandia lenyewe linamabehewa kumi lenyewe ninafunga watu ni balaa...hahahahaha
 
Kijakazi

JF-Expert Member
Jun 26, 2007
3,548
1,225
Ndio taabu ya sisi watanzania kukurupuka na kutafuta suluhisho la muda mfupi bila kufanya utafiti wa kutosha kabla hatujafanya uamuzi,kuanzia Mwakyembe na wote walioshiriki kwenye mchakato wa kuanzisha usafiri huu akili zao zilifikiria karibu sana badala ya mbali maana kwa jinsi wakazi wa Dar es salaam wanavyopata shida ya usafiri ilifaa kujiandaa vema kwa kuweka mabehewa ya akiba kama kutatokea kuwa na ongezeko la wananchi kusafiri na treni,badala ya kutatua kero tunazidi kuongeza kero kwa wananchi

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Acha kulalama hovyo, kila kitu kina mwanzo wake na mwanzo siku zote ni mgumu, mwanzoni tulikuwa hatuna kabisa treni sasa hivi tunayo na watu wanapata huduma, kama haitoshelezi au ina mapungufu hilo ni jambo lingine!

Sasa wewe ulitakaje, ulitaka iweje, kama ya New York au? usisahau kila kitu kinakwenda na bajeti na ukubwa wa mfuko wako, Waziri ameshasema wanajaribu tu kiubishi ubishi lakini sio kama eti ni Serikali nzima wameamua kuwekeza kwenye huo Usafiri, hilo ni fungu la kutoka Wizarani, kumbuka Wizara pia ina majukumu mengine Bandari, Reli za mikoani na kadharika, halafu isitoshe wakiwekeza pia sana ni lazima hiyo pesa irudi kwa kutoza nauli kubwa, labda kutoka Ubungo mpaka Posta itakuwa 5,000 shs, sasa ni Watz wangapi wanaweza kulipa, kama daladala tu 300 watu wanalia?

Na mwisho acha kulalama sana kama una suluhisho si useme nini kifanyike na utoe chanzo cha hizo pesa badala tu ya kulalamika, kitu ambacho kila mtu anaweza, na ndio maana watu wenye akili huwa hawalalamiki hovyo badala yake hubaki kimya, kwa maana wanajua ni kitu rahisi kufanya kuliko kutatua matatizo!
 
Naona msemaji wa Mwakyembe umetumwa kujibu mapungufu ya mradi wa Boss wako,tatizo lako unadhani kuwa mazezeta kama wewe ndio wenye akili maana ndio watu wanaokaa kimya hata wakiona jambo ambalo linatakiwa kusemewa.

Mijitu mingine haina maana kabisa,reli zinazotumika sasa ziliwekwa na nani?Mmekalia upuuzi tu kudhani kila kitu mnaweza kufanya kwa kukurupuka bila kufanya utafiti ndio maana maamuzi mengi na hata mipango ni ya muda mfupi kama akili zenu zilivyo.

Anayetaka suluhisho angenitafuta wakati wa mchakato wa kuifufua reli si sasa maana muda wa kufanya malumbano ambayo hayana tija sina.

Umenisoma zezeta mkaa kimya?Mkiiba na watu wakisema mnaiba mnakaa kimya na kusema watu wanalalama hovyo bila kuwapa suluhisho,sishangai kusikia kauli kama zako maana hazina tofauti na za wanaokutuma kuwasemea hapa.
 
Bado hujatatua tatizo, bado unalialia tu bila bila ufumbuzi!
 
Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
26,454
2,000
Kwanza nyinyi watu wa kamata ndio mnazingua, mkipandiaga hapo mnaenda bure mpaka Posta kugeuka nayo, mmeleta udaladala wenu kwenye treni, mbona kwanza kwenye daladala mnalipiaga ya kugeuza?

Sasa hapo Kamata hatutasimama mpaka mbadilike, nyi mnafikiri inatumia maji!?
 
Joseph

JF-Expert Member
Aug 3, 2007
3,521
1,225
Bado hujatatua tatizo, bado unalialia tu bila bila ufumbuzi!
Kama unasubiri ufumbuzi wa tatizo mlilolianzisha wenyewe basi una matatizo kichwani,wakati mnaandaa hamkujua kuwa mnatakiwa kujenga vituo vya kusubiria abiria hata mvua ikija wasiloe?Hamkujua kuwa watanzania wana shida ya usafiri hivyo mlitakiwa kujiandaa na si kukurupuka na kuwaletea shida watanzania walipa kodi ambazo mmetumia kuanzisha huo usafiri?Ni upuuzi kufanya biashara huku ukishindwa kutoa huduma ipasavyo wateja wanapoongezeka,sitoshangaa kusikia hata Rais wako hajui kwanini Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali zote tulizonazo,mbaya zaidi na wewe unataka ufumbuzi kama waziri wako Mkuchika anavyotaka majina ya walioweka pesa Uswisi toka kwa watanzania wakati serikali ipo na ni jukumu lake kutafuta na kujua ni kina nani wana pesa huko.

Zezeta kazini.
 
Eeka Mangi

JF-Expert Member
Jul 27, 2008
3,180
1,195
Naona msemaji wa Mwakyembe umetumwa kujibu mapungufu ya mradi wa Boss wako,tatizo lako unadhani kuwa mazezeta kama wewe ndio wenye akili maana ndio watu wanaokaa kimya hata wakiona jambo ambalo linatakiwa kusemewa.

Mijitu mingine haina maana kabisa,reli zinazotumika sasa ziliwekwa na nani?Mmekalia upuuzi tu kudhani kila kitu mnaweza kufanya kwa kukurupuka bila kufanya utafiti ndio maana maamuzi mengi na hata mipango ni ya muda mfupi kama akili zenu zilivyo.

Anayetaka suluhisho angenitafuta wakati wa mchakato wa kuifufua reli si sasa maana muda wa kufanya malumbano ambayo hayana tija sina.

Umenisoma zezeta mkaa kimya?Mkiiba na watu wakisema mnaiba mnakaa kimya na kusema watu wanalalama hovyo bila kuwapa suluhisho,sishangai kusikia kauli kama zako maana hazina tofauti na za wanaokutuma kuwasemea hapa.

Mimi sio mkaazi wa Dar! Lakini kwa kufuatilia tu majibu yako naona una lako la moyoni. Mkuu acha kumshambulia mwenzako badala yake tujadiliane ni nini kifanyike. Kutukanana haitatui tatizo bali huongeza tatizo. Nia na madhumuni sasa ni kuboresha kile ambacho kiliachoanzishwa!
Hapa nilitegemea ninyi mnaotegemea treni kama usafiri hapo Dar mtoe maoni ili idara husika ichambue nini wafanye kwa sasa na nini kifanyike baadae.
I do believe this was a short term projection and soon they can look for long term projection. Ili waweze kufikia long projection ni lazima mimi na wewe tuwaambie wafanye nini na waache nini. Tuwe na busara wakati wa kujadiliana kwa tija na maendeleo ya nchi yetu hata kama iko ICU! Mchango wetu utaiwezesha nchi yetu kutoka huko na kutimiza wajibu wake kwa Wananchi wake. Mungu awabariki sana
 
Suluhisho linajulikana na hakuna haja ya kuchangia lolote ili kupata ufumbuzi maana hata mtoto anajua akitaka kwenda shule abebe nini sasa unataka tujadili vitu ambavyo vinafahamika tayari?Ulikwishaona kituo hakina hata sehemu ya kujikinga jua acha mvua then unasema tujadili ufumbuzi wa tatizo!Suala hili lilichukuliwa kisiasa zaidi kuliko kiutendaji na matokeo yake ndio haya matatizo kwa wananchi,ukiishi kwenye nyumba ya vioo chunga sana kuwarushia wenzako mawe.
 
Wakati umefika sasa wa kusema bila kumumunya maneno. Sema hili ndilo suluisho ni hili. It might be your solution is not other are thinking. Sharing our views and ideas can lead us to a better solution!
 
Kijakazi

JF-Expert Member
Jun 26, 2007
3,548
1,225
Kama unasubiri ufumbuzi wa tatizo mlilolianzisha wenyewe basi una matatizo kichwani,wakati mnaandaa hamkujua kuwa mnatakiwa kujenga vituo vya kusubiria abiria hata mvua ikija wasiloe?Hamkujua kuwa watanzania wana shida ya usafiri hivyo mlitakiwa kujiandaa na si kukurupuka na kuwaletea shida watanzania walipa kodi ambazo mmetumia kuanzisha huo usafiri?Ni upuuzi kufanya biashara huku ukishindwa kutoa huduma ipasavyo wateja wanapoongezeka,sitoshangaa kusikia hata Rais wako hajui kwanini Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali zote tulizonazo,mbaya zaidi na wewe unataka ufumbuzi kama waziri wako Mkuchika anavyotaka majina ya walioweka pesa Uswisi toka kwa watanzania wakati serikali ipo na ni jukumu lake kutafuta na kujua ni kina nani wana pesa huko.

Zezeta kazini.

utasema unavyotaka kusema, utaponda unavyotaka, mimi kwangu najua ni maneno tu na hayana uzito na kila mtu anaweza kusema kama ulivyosema ni moja kati ya vitu rahisi kuliko vyote Duniani, na ndio maana nikakwambia hapo mwanzo watu wenye akili hawasemi semi na kulialia kila saa wanajaribu kutatua matatizo, yanayowakabili, wanaelewa kwamba mwisho wa siku tunajaribu kuboresha Tz moja, lkn pia mwisho wa siku Watz wamefurahia kupata usafiri wa Gari Moshi, na ndi kitu muhimu hayo mengine ni yako!

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom