Mh. Mwakyembe, fuata nyayo za Mrema; acha porojo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Mwakyembe, fuata nyayo za Mrema; acha porojo!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salary Slip, Aug 11, 2012.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,007
  Likes Received: 37,715
  Trophy Points: 280
  Leo hii nimeangalia taarifa ya habari ya ITV saa 2 usiku huu.

  Moja ya taarifa iliyovuta hisisa zangu ni ile ya mh. Mwakyembe kutembelea karakana ya TAZARA ili kijionea ukarabati wa mabehewa unaoendelea katika karakana hiyo. Kwa kifupi amefanya ziara ya kushitukiza.

  Hata hivyo, mh. Mwakyembe ameonekana kutokuridhishwa na maendeleo ya kazi hiyo na kupokea malalamiko ya wafanyakazi hao kutolipwa mishahara yao na posho zao kwa muda mrefu. Kama kawaida yake Mwakyembe ameishia kutoa vitisho kwa wahusika na kutokuchukua hatua yoyote ya kuridhisha. Tukumbuke hii si mara yake ya kwanza bali alishafanya ziara za kushitukiza TRA, stand kuu ya mabasi Ubungo na sidhani kama ziara hizi za kushitukiza zimeleta tofauti iliyokusudiwa.

  Ushauri wangu kwa mh. Mwakyembe ni kuwa asipokuwa makini itaonekana ziara zake ni kama za kupiga mkwara tu na kuonekana kwenye vyombo vya habari. Atapoteza heshima yake na imani ya watanzania kama ataacha kuchukua hatua za papo kwa papa kama alivyokuwa anafanya Mrema alipokuwa waziri wa mambo ya ndani.

  Mrema alikuwa anatoa siku saba kwa wahusika kuchukua hatua vinginenyo anawachukulia hatua mara moja. Sasa Mwakyembe yeye anangoja nini kuwatia adabu hawa TRA na TAZARA kwa uzembe?

  Alichokifanya shirika la ndege kinatakiwa kifanyike kwenye taasisi nyingine chini ya wizara yake.
   
 2. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Mkuu ungeangalia TBC kasema jtatu atarudi kuona kama maagizo yake yametekelezwa hasa ili la posho na atadeal na Shimwela!
  Mkuu uliyaka amfukuze mtu kazi on the spot nini kumbuka ni mwanasheria huyu lazima awe na vigezo vya kutimua tuone iyo jtatu kama watakuwa wamezembea
   
 3. Utamaduni

  Utamaduni JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 1,198
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160

  Hapo kwenye red,

  Hivi unaweza kuwa na imani kwenye nguo unayowekea kiraka? Siku zote watu wanakuwa na imani kwenye nguo mpya iliyonunuliwa, ndio maana wanavaa siku maalum kama iddi, krismas etc.,

  Eti muwe na imani na treni alizoziacha mkoloni mwaka gani vile tena sijui sitini na ngapi. Kama kweli wana lengo la kuweka miundombinu imara, siku zote nitasema tunahitaji kujenga mipya, kama ni treni tujenge mpya, mabehewa mapya kila kitu kipya na njia mpya, sio kutumia viraka na kuanza kuwakaripia watu eti msipomaliza hivi na vile,,,,, hata kwa fundi kati ya nguo mpya na ya kuweka kiraka anaanza kwanza kushona mpya kiraka baadae.

  Hamna kitu hapo watu wanajitafutia umaarufu na wapate cha kusema 2015 kinchoonekana since wameshindwa kutimiza ahadi walizoweka kama flyover etc...
   
 4. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #4
  Aug 11, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,007
  Likes Received: 37,715
  Trophy Points: 280
  Mkuu kusimamisha mtu kazi siyo sawa na kumfukuza.Nchi hii bila maamuzi magumu watu wataendelea kunyanyasika.

  Hebu fikiri wale wafanyakazi wamelalamika kuwa hawajalipwa posho zao na mshahara tangu mwezi juni na fedha zimeshatolewa na serikali ili walipwe lakini wanazungushwa tu.

  Yale madai ni mazito na ni ushahidi tosha wa uzembe wa wahusika.

  Hata yule kiongozi aliehojiwa na Mwakyembe ni wazi kajichanganya tu na ndio maana hata waziri kwa kutokuridhika na majibu yake akatishia kumfukuza kazi huyo bosi wake.
   
 5. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #5
  Aug 11, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Huyu mwakwembe napata shida sana kumuelewa plans zake
   
 6. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #6
  Aug 12, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Inasemekana Mwakyembe ameunda task force ya wataalam ili kumshauri jinsi ya kufufua ATCL, ingekuwa busara kama baadhi ya hao wataalam angewateua kwenye board ya shirika hilo ili wasimamie yale watakayoyapendekeza kuliko kusimamiwa na watu wasioamini kile kilichopendekezwa!
   
 7. k

  kajembe JF-Expert Member

  #7
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 756
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Tanzania siyo nchi yakukubali kua kiongozi hata mtu ajitahidi kiasi gani ataonekana anatafuta sifa tu,Tanzania imekua nchi ya watu wasiojua wanataka nini! nikulaum tu kila kitu.Mtu akijitahidi tumpe moyo basi,ndiyo maana mrema aligeuka akaamua kisifia tu CCM nilijiuliza mara nyingi kwanini? nimepata jibu.Magufuli kila akijitahidi watu wanasema anataka sifa,Mr six watu wanasema anataka sifa na unafiki,sasa hebu wafanye nini sasa?
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Salary Slip, usemayo ni kweli lakini naona tumpe kama mwaka halafu tumjaji kwa sababu nadhani hafanyi ziara za kustukiza bila kuchukuwa hatua stahiki za kurekebisha makosa anayoyakuta. Kumbuka kujenga ni rahisi kuliko kubomoa.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. L

  LIpili Member

  #9
  Aug 12, 2012
  Joined: Apr 14, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Usanii tu, ziara ya kushtukiza unaalika waandishi wa habari kwenda nao kwenye tukio. Yale yale ya kutafuta sifa badala ya kuwa serious na kazi
   
 10. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #10
  Aug 12, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,007
  Likes Received: 37,715
  Trophy Points: 280
  Kuhusu Mrema ujue aliktaa tamaa baada ya kukosa uraisi.Alitarajia na kweli alistahili kuungwa mkono ila watanzania wamengangania ccm licha ya uovu wote na ndio maana nae siku hizi ameamua kuwa hivyo.Kwa kifupi amechoshwa na unafiki wa watanzania pale linapokuja swala la uchaguzi.

  Watanzania ni watu wa kulalamika kila kukicha lakini unapofika wakati wa uchaguzi huchagua watu wale wale ambao miaka nenda miaka rudi huwalalamikia.Hata hawa walimu wanaogoma ni wanafiki wakubwa kwani wakati wa uchaguzi ndio vinara wa kuunga mkono ccm.CCM bila kuwajibishwa kamwe hawatakuwa na heshima kwa mwajiri wao ambae ni mtanzania.Hivi hata wewe kama mwajiri wako hakupi hato onyo unapovurunda kweli utamheshimu?
   
 11. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #11
  Aug 12, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,007
  Likes Received: 37,715
  Trophy Points: 280
  Mkuu Zomba nashukuru kwa leo kuunga mkono hoja.
   
Loading...