Mh. Mustafa Mkolo amuombe radhi Mh. Zitto Kabwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Mustafa Mkolo amuombe radhi Mh. Zitto Kabwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lyimo, Feb 3, 2012.

 1. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Inakumbukwa kuwa mwaka jana mwezi wa tano kulikuwa na vuta nikuvute kati ya Mh. Zitto Kabwe na waziri wa Fedha na Uchumi Mh. Mustafa Mkulo. Katika mkutano wa hadhara mjini Mbeya, Zitto alielezea habari ya kufilisika kwa serikali na hata kushindwa kulipa mishahara ya watumishi wake kwa wakati.

  Mh. Mstafa Mkulo alimkanusha vikali na kumuita ni mzushi. Mh. Mkulo aliungana na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Ndg. Harry Kitilya katika mkutando na waandishi wa habari mjini Dodoma na kumkanusha vikali Zitto Kabwe huku akieleza jinsi serikali inavyokusanya mapato yake kutokana na kodi mbalimbali.

  Pia alichanganua kiasi cha fedha katika ulipaji wa mishahara, lakini hakueleza uchangiaji wa serikali katika dshughuli za maendeleo na huduma mbalimbali.
  Tangu kipindi hicho, serikali imekuwa ikishindwa kuendesha shughuli zake nyingi kikamilifu (hasa huduma nyingi za kijamii na miradi ya maendeleo).

  Taasisi zake nyingi zipo kwenye ukata mkali na wakuu wake wakihangaika kuzisimamia kutokana na ufinyu wa pesa walionao. Jana katika kikao cha Bunge, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) Mh. George Mkuchika alikubali kuwa Serikali imefilisika na imeshindwa kuendesha shughuli zake nyingi zinazosimamiwa na Halmashauri na taasisi zake nyingine.

  Mara nyingi viongozi wa serikali yetu wamekuwa hawasemi ukweli katika mambo mablimbali, na hili ni tatizo kubwa nchini kwetu. Waziri mwenyedhamana anasema fedha zipo, wakati viongozi wa vitengo mbalimbali wanasimamisha shughuli na kutuambia serikali haina fedha. Maranyingine imetupelekea kuwalaumu viongozi wa vitengo kwa kuwa ni wafujaji wa pesa za serikali kumbe hawakupokea kasma stahili.


  Kwa uongo wa Mh. Mkulo, anastahili kumuomba radhi Mh. Zitto na watanzania wengine tuliopotoka na kumlaumu Mh. Zitto kuwa ni mropokaji wa vitu si vya kweli.

  Vilevile itatuwia vigumu sana kuamini matamshi yoyote ya viongozi wetu kwani hawana utamaduni wa kuwajibika pindi wanapobainika hawakuwa sahihi katika matamshi yao ama utendaji wao.
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono hoja
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Hawezi coz atasema kuwa serikali parse haijatamka kuwa imefilisika!
   
 4. B

  Baba Collins JF-Expert Member

  #4
  Feb 3, 2012
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 498
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Let us wait and see,watasema tu.
   
 5. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #5
  Feb 3, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Akiomba nitajua TZ imebadilika sana, mtu mwenye mkullo, akili hiyo katoa wapi?
   
 6. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #6
  Feb 3, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kwa staili hii JF haitasalimika! Lets pray iendelee kuwepo!
   
 7. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #7
  Feb 3, 2012
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Mficha maradhi...,walikanusha pia kuhusu mtikisiko wa uchumi baadaye tukashtuliwa na bail out ya ajabu ya zaidi ya TZS 1 trilioni ambazo nazo zilifisadiwa..sijui sasa watajikomboa vipi manake hata hao 'wajomba' nao kwao hali ngumu..
   
 8. nice 2

  nice 2 JF-Expert Member

  #8
  Feb 3, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kusema tu ule ukweli huyu waziri wa Fedha Mh. Mkulo ile wizara haiwezi kabisa, amekuwa akionyesha mapungufu kila mara. Waziri kivuli wa Fedha is 100 times smarter than him, na hapo ndipo tatizo linapoanzia. Kila mara Mh. Zitto anamuumbua Mh. Mkulo kwa kumueleza ukweli, lakini tatizo huyu mzee hapendi kujifunza kwa kuelezwa ukweli, ana siasa za kizamani sana, matokeo yake huwa anaishia kusema mara Zitto anamfuatafuata, mara Zitto muongo, lakini mwisho wa siku yeye ndiye anadhihirika kuwa muongo.

  Zitto alisema hali ya serikali kifedha mbaya, Mkulo akapinga. Zitto akasema tena Budget ya 2011/2012 kufikia Dec 2011 ina deficit kubwa kutokana na mfumuko wa bei, Mkulo akasema ni uzushi, sasa imedhihirika tena kuwa kweli.
  Na bado nakumbuka vizuri sana chuki za Mkulo zilienda mbali hadi bunge la budget mwaka jana akasema Zitto amehongwa na CHC, jamaa akasema kwamba uchunguzi ufanyike na ikidhihirika kweli atajiuzulu, akamuomba waziri naye aweke ahadi ya kujiuzulu ikidhihirika anayoyasema ni uongo, lakini waziri hakudhubutu. Badala yake akasema report ya uchunguzi itapelekwa bunge lijalo lakini tumeona kimya bunge la nov, na sasa hili la Feb ngoja tuone kama hili jambo litaibuliwa tena.

  Muda mfupi uliopita tena nimeona Zitto akichangia marekebisho ya sheria ya "Anti money Laundering" akawa anaeleza jinsi anavyoshangazwa na waziri wa Fedha anavyoleta marekebisho ya sheria iliyotungwa miaka 6 iliyopita lakini utekelezaji wake haujawa enforced na waziri wa fedha... TBC nao walivyo wachokozi wakawa wanamuonyesha tu Mkulo macho yalivyomtoka.
   
 9. m

  mtengwa JF-Expert Member

  #9
  Feb 3, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 1,745
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  Naunga mkono hoja
   
 10. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #10
  Feb 3, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Serikali yetu haiwezi kukiri udhaifu wake hata siku moja, kwa hiyo hata mkulo hawezi kuomba radhi kwa sababu hana tendency. Yeye kila kitu anasema Zitto ni muongo bila kujua kuwa yeye ndio anaoneka muongo mbele ya wananchi
   
 11. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #11
  Feb 3, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Baba hawezi kukubali kuwa amekosea japo anaweza kuwa amekosolewa.
   
 12. k

  kabuga Member

  #12
  Feb 3, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh! hata Silinde aliambiwa afute kauli baada ya kusema bungeni kuwa serikali imefilisika, lakini yaweza kuwa kweli, kwani masikini nae anafilisika?
   
 13. obm

  obm Member

  #13
  Feb 3, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ni bora mkulo akomba apatiwe ile budget ya upinzani ili waitekeleze kunusuru nchi kufilisika zaidi ni hatari jinsi inflation inavyopaa
   
 14. sterling

  sterling Senior Member

  #14
  Feb 3, 2012
  Joined: Aug 6, 2011
  Messages: 163
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  tatizo la viongozi wetu ni waropokaji na wanazungumza tu bila kupima impacy ya maneno yao
   
 15. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #15
  Feb 3, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Hivi tujiulize a very simple QN ni waziri gani wa JK toka CCM ana maslahi ya NCHI hii?

  Maana wengi wao wako kimaslahi ya kichama zaidi wao tamko lao ni CCM hawajui kuwa walio wachagua na kuwaweka hapo wao wana taka maendeleo na si upuuzi tuuu.

  Wizara ya Fedha na TRA wao wana lao jambo esp kipindi cha Campaign TRA hutoa pesa nyingi sana kwa CCM kuna kikao kiomoja kilifanyika huko Arusha na mkulo alihakikisha wafanya kazi wanao hudhuria kikao ni wa TRA na watu muhimu tuu na kwabahati nzuri mtu mmoja alijipenyeza kama mfanya kazi na akasikia yote ni mikakakti ya kuhakikisha kuipa pesa CCM kwenye uchaguzi nchi hii inaona uchaguzi ni deal kuliko maendeleo ya nchi hii hili liko wazi kabisa na ndio maana watu wengi wana kichukia CCM maana mawazo yao ni mufu sana


   
 16. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #16
  Feb 3, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  KIkwete liokoe taifa, tubadilishie waziri wa fedha
   
 17. nice 2

  nice 2 JF-Expert Member

  #17
  Feb 3, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe mkuu lakini hawa mawaziri wanatofautiana... ninachokiona kwa Mkulo ni uwezo wake ulivyo mdogo. Yani sijui hata kama huwa anaelewa kinachoendelea huyu jamaa, halafu wala presha hana, hana nia ya kutaka kujua. So relaxed! Sielewi JK ataendelea kumkumbatia mpaka lini.
   
 18. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #18
  Feb 3, 2012
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kweli hatuna serikali, Mh. Zito anajua mambo mengi ya serikali kuliko hata mawaziri wa serikali hizo, yaani anasema kitu wanakanusha halafu wanakubali baada ya muda

  Juzi alisema Rais hajasign posho Pindua Pindua akasema Rais amesign, Rais akasema hajasign. Alisema serikali imefirisika wakakataa sasa wanatangaza kweli serikali imefilisika, inaonekana Zito anafanya kazi zaidi ya mawaziri au am getting it wrong.
   
 19. everybody

  everybody JF-Expert Member

  #19
  Feb 3, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Hapo kwenye RED, mi nafikiri kwa sasa mawaziri wote wa JK wamezishindwa wizara zao, sio Mkulo tu. Inahitajika total reformation ya Serikali nzima kuanzia kwa Pinda mpaka kwa Hawa Fujo (a.k.a Hawa Ghasia).
   
 20. nice 2

  nice 2 JF-Expert Member

  #20
  Feb 3, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nilicheka sana nilivyosoma kwenye the citizen jinsi Zitto alivyomjibu Nkamia sikuile ya kikao baada ya kuulizwa amekuwa msemaji wa ikulu? some things are so simple to find out it doesnt even need one to sweat, ni kushughulisha ubongo tu. Hivi ndivyo hawa vijana haswa wa upinzani wanavyojipatia sifa... kwa kujishughulisha. Wazee wa CCM wamechoka sasa wapumzishwe jamani waneshaidumaza hii nchi vya kutosha.
   
Loading...