Mh Mussa Azan "Zungu", waambie CCM waige Rwanda kwa hili la magari ya serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh Mussa Azan "Zungu", waambie CCM waige Rwanda kwa hili la magari ya serikali

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tuko, Jun 16, 2011.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Jun 16, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Mimi sio mshabiki wa CCM, lakini napenda kumuunga mkono Mh Zungu (kwa hoja ya umoja wa kitaifa) kwa hoja yake ya serikali kudhibiti matumizi ya magari ya ghali.
  Kwa ufupi tu, Mh Zungu aliongea yafuatayo
  - Viongozi wa serikali Tz wanatumia magari ya gharama sana, yanayoongeza matumizi yasiyo ya lazima kwa serikali
  - Serikali iwe na standard ya magari, kwa mfano Kenya wanatumia Volkswagen isipokuwa kwa viongozi wakuu wa serikali.
  - Mh Zungu alisisitiza sana mawaziri watumia magari yao binafsi, kwa kupewa tu posho ya mafuta, kwa safari za kawaida

  Kimsingi nakubaliana na Mh. Zungu, lakini hebu tuangalie mfano wa nchi nyingine ya Rwanda. Hii ni nchi ambayo hivi majuzi tu ilikuwa katika vita kubwa ya wenyewe, lakini kwa kasi ya maendeleo waliyo nayo leo, Tanzania hatuwagusi.
  Kuhusiana na magari ya serikali inasemekana (kwa niliyoambiwa na mnyarwanda mmoja aliyeko serikalini),

  - Ni viongozi watatu tu wa serikali wanaopewa magari ya kutembelea; Raisi, Jaji Mkuu na Spika wa bunge
  - Viongozi wengine wote wanatumia magari yao 'binafsi' kwa utaratibu ufuatao;
  Kiongozi wa serikali au shirika la umma anayestahili, hu-identify aina ya gari anayotaka kutoka katika kampuni ya kuagiza inayotambuliwa na gharama yake ya kununua. Serikali humpa 50% ya fedha ya kununua, na kumkopesha 50% nyingine bila riba, lakini kwa masharti ya kukata deni lake kwenye mshahara kwa kipindi kilichoamuliwa. Kila mfanyakazi anakuwa na haki hii kila baada ya miaka mitatu, tokea alipopata gari moja. Kila kiongozi anayestahili hupewa fixed amount ya posho ya mafuta kwa mwezi. Udhibiti umewekwa kwa makampuni yanayoagiza magari kiasi kwamba bei ya gari haiwezi kuchakachuliwa kwa manufaa ya kiongozi. Kiongozi (isipokuwa hao watatu), hapewi dereva na serikali, na kama anataka kuendeshwa basi anaajiri dereva kwa hela yake. Zimewekwa gari maalumu ambazo zinatumika kama kiongozi anakwenda kikazi katika safari ambayo inahitajika kutumiwa gari maalumu ya serikali.
  Kwa Utaratibu huu serikali ya Rwanda imeweza kudhibiti sana matumizi katika magari ya serikali.

  Nadhani ndg Watanzania mnajua hali ikoje hapa kwetu...
   
 2. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Chukua chako mapema,then gonga meza mjengoni ukisubili miaka5 ¨¬ishe upate 60m.they dont care at all
   
 3. Rocket

  Rocket Senior Member

  #3
  Jun 16, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hapa kwetu imekuwa ni wimbo wa Taifa kwani mafisadi wana maslahi yao Mkuu.....
   
Loading...