Mh. Msigwa awekwa kitimoto leo jimboni kwake, yeye alonga ukweli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Msigwa awekwa kitimoto leo jimboni kwake, yeye alonga ukweli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kamandamakini, May 10, 2012.

 1. k

  kamandamakini Senior Member

  #1
  May 10, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 158
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  [​IMG]
  Mh. msigwa akiwa katika mdahalo leo.​

  [​IMG]


  akizungumza


  [​IMG]  [​IMG]
  akisikiliza swali, nakisha kujibu kwa ufasaa

  MBUNGE wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (Chadema) amewatakawananchi wa jimbo hilo na watanzania kuendelea kupiga vita vitendo vya ufisadikwa vitendo ikiwa na pamoja na wao wananchi kufanya kazi badala yakuwanyoshea vidole mafisadi wakati na wao wananchi ni mafisadi wa muda.

  Alisema kuwa kuvunjwa kwa baraza la mawaziri ni kutokana na hasa wabunge wa chadema kuchukizwa na vitendo vya ufisadi kwa mawaziri waliotemwa katika wizara zao na Rais na kuwa hata baraza jipya lililoteuliwa sasa iwapo litaendeleza vitendo vya ufisadi kama lile lililovunjwa basi watashughulikiwa kama wenzao .

  Mbunge Msigwa alitoa kauli hiyo leo katika ukumbi wa chuo chamaendeleo ya jamii Ruaha katika mdahalo wa pamoja kati yake na wapiga kura wa jimbo la Iringa mjini mdahalo ulioandaliwa na mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Iringa na kuratibiwa na asasi ya ICISO .

  Akiongea kwa umahiri alisema, jitihada mbali mbali zinazofanywa na wabunge katika kuchukizwa na vitendo vya ufisadi ila bado kwa upande wa wananchi pia wamekuwa wakishiriki kufanya ufisadi ambao ni mkubwa zaidi na wenye kulifanyaTaifa kuendelea kuwa nyuma katika maendeleo kutoka na tabia ya baadhi yawananchi kuendekeza uvuvi wa kushinda vijiweni bila kazi.

  Hivyo alisema kuwa wakati mawaziri na viongozi wanatuhumiwa kwa ufisadi nakuondolewa katika nafasi zao bado wananchi nao wanapaswa kujitathimini kwakufanya kazi kwa bidii badala ya kushinda vijiweni.

  Aidha mbunge Msigwa alisema kuwa kamwe hatakuwa tayari kuwatetea wananchiwa jimbo lake ambao wanakiuka sheria za mipango miji kwa kujenga nyumba bilakufuata taratibu za mipango miji.

  Kwani alisema kuwa kuendelea kuwatetea wananchi wanaojenga nyumba kiholelakatika maeneo ya hifadhi ya barabara ni sawa na kujipalia makaa ya moto kwa madai kuwa leo ni serikali ya CCM ndio ipo madarakani ila ipo siku serikali ya Chadema itakuwepo madearakani hivyo kama wavunja sheria wataendelea kutetewa nchi haitatawalika pia kwa Chadema.

  Mbunge Msigwa aiendeleza falsafa yake kuwa yeye si mbunge wa kugawa samaki kwa wapigakura bali ni mbunge wafundisha wapigakura wake kuvua samaki.

  Hivyo lazima ataendelea kuwaongoza wapiga kura wake kufuata sheria na siokuwatetea hata pale wanapokiuka ama kuendelea kuwahonga fedha kama njia ya ushawishi badala ya kuwapa mbinu za kuzifuata.

  Aidha aliasema kuwa iwapo utaona mbunge anaendesha jimbo kwa fedha zake za mfukoni basi ujue ni mwizi ama ni mfanyabiashara mkubwa hivyo alisema kuwa hapendi kuwadanganya wapiga kura hao kuwa ataboresha miundo mbinu wakatiserikali yenyewe imekwama kufanya hivyo
  Mratibu wa midahalo hiyo Raphael Mtitu alisema kuwa mdahalo huo umeonyeshakufana zaidi na kuwa lengo la midahalo hiyo ni kuwakutanisha wapiga kura nawabunge wao ili kuongeza kasi ya maendeleo kwa matakwa ya wapiga kura .

  Hata hivyo alisema midahalo kama hiyo itaendelea katika jimbo la Isimani kwa kumweka kitimoto mbunge wa jimbo hilo Wiliam Lukuvi ambaye ni waziri wa nchiofisi ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge , jimbo la Kalenga linaloongozwa na waziri wa Fedha Dkt Wiliam Mgimwa na jimbo la Kilolo linaloongozwa na Prof.Peter Msola na kuwaomba wabunge hao kushiriki midahalo hiyo.

  pia aliwaasa vijana kwa jumla kwamba kila kijana anapaswa kuwa na vision, goal, and plans katika maisha yake na kamwa asiwepo mtu anae kubali kutumiwa na mtu yoyote, maana sisi sote ni watu wa muhimu. aliwaasa washiriki wa mdahalo huo kuwa kukubali kutumiwa nikukanbidhi utu wako kwenye rehema na huruma za mtu mwingine, ambako huko nikufilisika kifikra kupita kiasi, alisema mheshimiwa Msigwa.
   
 2. ipogolo

  ipogolo JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2012
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 4,096
  Likes Received: 2,972
  Trophy Points: 280
  nilitamani sana kuhudhuria mdahalo huo; muda wake ulikuwa mbaya saa 4 asubuhi wakati wa kazi. ushauri: next time tufanye midahalo week ends mpate washiriki wengi zaidi.
   
 3. K

  KISAKA MORIS JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 372
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo imekaa vizuri, kwa kweli huu mpango utawezesha wananchi wengi kuwajua vyema wabunge wao na utendaji wao kiujumla, Mungu awabariki.
   
 4. james chapacha

  james chapacha JF-Expert Member

  #4
  May 10, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 942
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Mbunge wangu Maji marefu sijui anayaweza? mpaka leo sijui elimu yake.
   
 5. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #5
  May 10, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  CDM Tunakwenda kuchukua nchi 2015 maandalizi yashakamilika
   
 6. T

  Tewe JF-Expert Member

  #6
  May 10, 2012
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 744
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 60
  Kwa maelezo hayo msigwa ameiva
   
 7. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #7
  May 10, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hii ingerushwa live, ingesaidia sana watanzania kupima viongozi wao, na kutoa ushauri. Namkumbuka Tido.
   
 8. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #8
  May 10, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  hakuwa anapikwa, bali anawiwa kuitendea nchi yake miongoni mwa mazuri anayoyafahamu.
   
 9. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #9
  May 10, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,610
  Likes Received: 3,911
  Trophy Points: 280
  very attractive speech,

  huyu ni kiongozi...ukweli daima!! ''kosoa serikali lakini eleza wajibu wa wananchi''

  Impressive na nadra sana kupata utamu huu kwa viongozi wa chadema,

  mna hekima humo
   
 10. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #10
  May 10, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,817
  Likes Received: 36,921
  Trophy Points: 280
  msigwa ni kiongozi mahiri kwa kweli.
   
 11. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #11
  May 10, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,787
  Likes Received: 2,684
  Trophy Points: 280
  Haitachukua Muda midahalo hiyo kukwama kufanyika kwenye majibo ya wabunge wa Chama Tawala kama itaendeshwa kwa uhuru, subirini tu muone.
   
 12. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #12
  May 10, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Kaka msigwa Mungu wa israel akubariki.
   
 13. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #13
  May 10, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,080
  Trophy Points: 280
  Msigwa mbunge bora sana, na mara nyingi huongea yagusayo mitima.
   
 14. IKHOIKHOI

  IKHOIKHOI JF-Expert Member

  #14
  May 11, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 366
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kibajaji alisema kazi ya maji marefu ni kuchanja watu chale tuuuu mpaka za m***koni. Maaaaaweeeeeee Kibajajiiiiiiiiiiiiii kweli niliamini bangi ni mbaya.
   
 15. JOYCE PAUL

  JOYCE PAUL JF-Expert Member

  #15
  May 11, 2012
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 1,007
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  ndio achakarike sio kuzingua watu tu...
   
 16. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #16
  May 11, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  CDM wanakuja na style ya ulaya ambayo ccm wakiiga tu majimbo yote wanayapoteza. Mdahalo na ccm ni sawa na paka na panya.ccm wanapendana na pilau tshirt , chachandu na Matusi
   
 17. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #17
  May 11, 2012
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,565
  Likes Received: 624
  Trophy Points: 280
  Ndio yupi tena huyu wa Israel? Nyinyi watu bana...kwa hiyo wako wangapi??
   
Loading...