Mh Mnyika, Tunakuomba Ukarabati Barabara; NSSF Wameharibu zilizopo Ubungo

SEBM

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
495
325
Mh Mbunge,
Sisi wapiga kura wako wa Ubungo, hasa maeneo ya Plaza na Ubungo NHC, tunakuletea kilio chetu cha ubovu usiomithilika wa barabara za mitaani.
Ni kwamba, Shirika la Hifadhi ya Jamii(NSSF) Mkoani wa Kinondoni, wamekuwa kltika zoezi la kuweka mfumo mpya wa maji taka na hivyo kulazimika kuchimba barabarani au pembezoni mwa barabara ili wapitishe mabomba na 'chambers, Kazi hiyo imefanyika lakini hawakufukia au hawakufukia vizuri kwenye mitaro na mvua hizi zinazoendelea kunyesha zimeacha mitaro na mashimo makubwa ambayo hayapitiki.
Mh, tunaomba utusaidie kutukarabatia barabara zetu za mitaani kwani NSSF wametufanya kitu mbaya
 
Mh, tunaomba utusaidie kutukarabatia barabara zetu za mitaani kwani NSSF wametufanya kitu mbaya
Awasaidie kuwatetea na kutafuta muafaka na mwisho barabara kujengwa au yeye mwenyewe ndio aikarabati, nadhani hapo cha maana ni nyie kumpelekea haya malalamiko na yeye pamoja na nyie kuwabana hao NSSF (after all nyie wote mna nguvu kuliko yeye mmoja) kwahio mpeni msaada ili nyie wote kuhakikisha barabara inakarabatiwa
 
haya maeneo yamekuwa korofi sana kwa muda mrefu. Hata mmiliki wa Ubungo Plaza anatakiwa afanye tukio maana njia ya kutokea kwenye hilo jengo ni balaa tupu.
 
si kwamba nssf walitakiwa warudishe barabara kwa kiwango walichokikuta?

tusiwatwishe wabunge mzigo tukawafanya waendelee kudai nyongeza ya posho. Kazi ya kukarabati barabara sio ya mbunge. Ni kazi ya halmashauri husika ikishirikiana na wadau wake. Mbunge anatumwa kuiuliza na kusimamia serikali kama kauli ya wananchi. Mkiona serikali kichwa cha panzi kama ya jk basi jitoleeni kuikarabati mkisaidiana na madiwani na mbunge, SIO YEYE NDO AKARABATI! Hiyo sio kazi yao.
 
Back
Top Bottom