Mh. Mnyika ninakukumbusha

MANYORI Jr

JF-Expert Member
Mar 25, 2012
462
343
Heri ya sikukuu ya Krismas ndugu wana JF

Awali ya yote nipongeze hatua mbalimbali ambazo zimepigwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na zilizopelekea kupatikana kwa viongozi wake katika ngazi zote za chama.

Lakini zaidi nipongeze mchakato mzima wa kuwapata viongozi wa ngazi za juu kabisa na hivyo 'timu' imekamilika.

Pamoja na hatua hizi muhimu,ningependa pia kumpongeza Mh. J. J. Mnyika binafsi kwa kuchaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA kwa kuridhiwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama. Ninampongeza yeye binafsi kwa kuwa anastahili kulingana na unyeti wa nafasi hiyo katika chama.

Mh. Mnyika nimemfahamu kwa namna tofauti tofauti lakini zenye mwelekeo unaofanana. Nimemfahamu tangu akiwa mbunge wa Jimbo la Ubungo jimbo ambalo leo linaongozwa na ndugu Kubenea.

Nimemfahamu kama mwanaharakati na mpambanaji wa kweli katika kuyaleta mabadiliko ya kweli.

Nimemfahamu pia kama kiongozi asiyeogopa chochote katika kuusimamia ukweli;jambo ambalo ndilo linaloleta kila kilichochema.

Kwa muhtasari; Mh. J. J. Mnyika anafaa katika nafasi hiyo na hata ya juu zaidi.

Mwaka 2016 nilipata nafasi ya kuzungumza na Mh. Mnyika na nilimweleza yeye (Kama kiongozi wa ngazi ya juu ya chama na kijana mwenzangu) juu ya kiu ya vijana katika taifa letu.

Nilimweleza juu ya vilio vya vijana ambao kwa takwimu zisizo rasmi ndilo kundi kubwa la watu katika nchi yetu na ambalo ni 'turufu' muhimu katika maisha ya siasa za nchi.

Nilimweleza kuwa vijana wengi katika taifa hili wamekata tamaa kwa kuwa hawana tumaini wala mtetezi wa masrahi yao kama vijana na Watanzania.

Nilimwambia vijana wapo tayari kushirikiana na yeyote aliyetayari kushikamana nao katika harakati za kutengeneza hatma zao.

Nilimweleza kuwa vijana wapo tayari kuunganisha nguvu zao na yeyote anayedhamilia kuyabadili maisha yao.

Nilimweleza kuwa changamoto kubwa katika maisha ya vijana hawa ni 'ajira'!

Mh. Mnyika ulinimbia kuwa kwa namna hali ilivyo tete(kutokana na ukosefu wa ajira kwa vijana wahitimu wa fani mbalimbali hasa ualimu masomo ya sana) inabidi jambo hili litafutiwe jukwaa zuri la kuweza kusemewa na kufanyiwa maamuzi.

Na katika hatua hiyo ulinieleza kuwa jambo hili (la ukosefu wa ajira) mngeliingiza katika hotuba ya kambi rasmi ya upinzani bungeni (KUB) kupitia hotuba ya waziri kivuli wa wizara ya elimu, sayansi na teknolojia ambayo ingesomwa bungeni Dodoma.

Mh. Mnyika ulinipa matumaini mimi binafsi na vijana wote katika taifa letu.

Ni miaka takribani minne tangu tuzungumzie jambo hili (la ukosefu wa ajira kwa vijana) lakini nikiri kwamba ule utete wa hali kwa sasa upo juu kuliko nyakati zozote za maisha ya taifa letu.

Vijana bado wapo hoi bin taabani hasa wenye fani ya ualimu wa masomo ya sana.

Vijana bado hawana msaada wala yeyeyote wa kuwashuka mkono katika nyakati hizi za dhiki kuu.

Mh. Mnyika, Umeshakabidhiwa ofisi kurasimisha majukumu yako kama Katibu Mkuu wa chama kikuu cha upinzani katika taifa letu.

Mh. Mnyika, tayari umesha taja mikakati ya ofisi yako na chama kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2020; Isimamie.

Mh. Mnyika ninakukumbusha kwamba vijana tupo tayari kuwaunga mkono kama mpo tayari kushirikiana nasi katika harakati za kuyabadili maisha yetu ikiwemo kudai ajira (zisizo na ubaguzi).

Mh. Mnyika tunaomba muungane na sisi katika kuyaleta madiliko ya kweli na ninakuhakikishia suala la 'ajira' ndilo kiboko ya watawala wabovu tangu kuanza kwa ustaarabu wa siasa duniani. Hebu tazama Tunisia, Libya, Sudani na kwingineko utajihakikishia pasi na shaka.

Mh. Mnyika ninakukumbusha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom