Mh. Mnyika, January, Ngeleja na Lema address this issue ASAP (Power rationing Arusha) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Mnyika, January, Ngeleja na Lema address this issue ASAP (Power rationing Arusha)

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Saharavoice, Jun 22, 2011.

 1. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2011
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Pamoja na kwamba bushbaby, Mvumbuzi na Mo-TOWN wameandika threads tofauti kuhusu power rationing hapa Arusha, naomba nami kwa mtiririko huo huo niwaombe waheshimiwa tajwa hapo juu kwa nafasi zao walishughulikie suala hili kabla hali haijawa tete hapa jijini.
  Ndugu zangu waheshimiwa, Mgawo wa umeme upo maeneo karibu yote katika nchi yetu, hilo linatambulika kwa kila mwananchi na hii siyo hoja ya msingi hapa.
  Hoja yangu ni kwamba, Hapa Arusha tangu tarehe 18 June 2011 mpaka ninapoandika ujumbe huu kwenu, mgawo wa umeme umekuwa kero haijapata kutokea. ikumbukwe kwamba kabla ya tarehe hiyo tulikuwa na mgawo, lakini kwa lugha rahisi, ulikuwa fair.
  Kuna maeneo ya aina tatu (naomba kusahihishwa) kuhusiana na mgawo huu. eneo la kwanza ni lile la Hospitali kuu ya Mount Meru na wote waliounganishwa nao, hawa hawana mgao (sina tatizo hapo)
  Kuna kitu wanakiita phase I na Phase II. kilichotokea ni kwamba wale wa phase I wanapata umeme usiku tu mfululizo na wale wa Phase II wanapata umeme mchana tu mfululizo, kwa maana hiyo, shughuli za uzalishaji kwa wale wa phase I zimesimama tangu tarehe 18, na wakati huo huo, wale phase II wanakesha macho ili kulinda usalama wao na mali zao kutokana na giza la usiku mzima.

  Najiuliza, nini kimetokea Arusha ambacho wananchi hatutakiwi kufahamu kuhusu mgawo huu?
  Je, wale wanaotegemea umeme kujipatia riziki zao wafanye nini?
  Waheshimiwa, fuatilieni hili haraka iwezekenavyo kabla bomu halijalipuka hapa Arusha. hakutakuwa na CCM wala CDM hapo, maana wanasiasa mmezoea kila kitu kukifanya cha kisiasa.
  We need a fair power rationing as from today.
  Naomba kutoa hoja.
   
 2. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #2
  Jun 22, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Naunga mkono hoja!
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Jun 22, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Tanesco walitangaza mgao kutokana na kile walichosema matengenezo kwenye mitambo ya Songosongo. Na mgao huo ulitangazwa kuw ungeisha tarehe 26 May. Sasa Huu mgao unaondelea hivi sasa ni kwa sababu gani na unaisha lini? Dar es Salaama unakatika kwa masaa 10 hadi 15 (kwa siku). hivi naandika hapa hakuna umeme, na jana hakukuwa na umeme kuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 5 usiku!!!

  Kwa nini tanesco na wizara wasitoe tangazo tujue moja? Kuna nini kimefichwa? Mtu mwenye number ya John Mnyika tunaomba aweke hapa jamvini ili tuwasiliane naye moja kwa moja aulize swali bungeni sasa hivi. Ngeleja anatakiwa aache kazi. Huyu kijana hafai hata kidogo na sujui alipewa wizara nyeti kama hii ya madini na nishati kwa utashi gani?
   
 4. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #4
  Jun 22, 2011
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  HTML:
  
  
  Mkuu FJM, Pamoja na kuongeza hayo masaa, lakini kwa nini mgawo usiwe wa kupokezana? ili wale waliofanya shuguli za uzalishaji jana, leo nao wapumzike wawapishe wenzao waliokosa jana.
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Jun 22, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hivi lakini kuna kini pale Tanesco? mwanzo walisema mitambo ya Dowans ingepunguza mgao, sasa Symbion wameinunua na tayari wameiwasha. Inakuwaje mgao unakuwa mkali kabla ya haya mitambo ya Symbion kuwashwa? Na kama kuna mgao kwa nini wasitutangazie wananchi kama ambavyo wamefanya? Nadhani huu mgao unaondelea sasa una something fishy.
   
Loading...