Mh. Mnyika hebu tupia macho shule ya msingi Mashujaa - Sinza; ni hatari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Mnyika hebu tupia macho shule ya msingi Mashujaa - Sinza; ni hatari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kurunzi, Mar 21, 2012.

 1. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Najua unakazi nyingi na majukumu mengi lakini naomba utiweke kwenye ratiba yako shule ya msingi mashujaa sinza hali ni mbaya sana, shule ni kama haina vyoo kwani vilivyopo haifai kabisa na havistahili kutumika.

  Najua shule ina kamati ya shule lakini kamatati ya shule imeshundwa kutimiiza wajibu wake ni kama haipo kabisa.

  Sorce Mlimani Tv.
   
 2. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #2
  Mar 21, 2012
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Kurunzi, Asante kwa taarifa. Ki mamlaka na majukumu, kamati ya shule iko chini ya wananchi kupitia kwa wazazi na kiuongozi inasimamiwa na diwani na mtendaji wa kata kupitia kamati ya maendeleo ya kata (WDC). Nimemjulisha Diwani na Mtendaji waniletee taarifa rasmi ya haraka kuhusu hatua ambazo wamechukua.

  Kirasilimali, katika mazingira ya kawaida matengenezo ya shule bajeti yake iko chini ya Halmashauri baada ya kupokea ruzuku kutoka serikali kuu pamoja na vyanzo vya ndani vya halmashauri. Kuna matatizo makubwa ya vyoo katika shule nyingi za Dar es salaam kwa kuwa zilijengwa chini ya kiwango miaka mingi ya nyuma na sasa ndio madhara yameanza kuonekana. Aidha, sehemu kubwa ya vyoo ni vya shimo badala ya Asian type, hali ambayo ni hatari zaidi vinapodidimia. Kwa kutambua hali hii tumetaka Halmashauri ifanye tathimini ya vyoo vyote kuangalia vilivyo katika hatari na matengenezo yanayohitajika. Baadhi ya shule tayari tumepata ripoti na kuelekeza hatua za kuchukuliwa, baadhi bado kazi inaendelea. Baada ya kupokea taarifa toka kwenye kata, nitawasiliana na Halmashauri kwa ajili ya hatua zao.

  Ingawaje nikuhimize Kurunzi na wengine kwamba si kila kitu kwenye kata lazima mbunge afuatilie, mambo mengine ni ya kawaida sana ambayo yanahitaji tu hatua za wananchi na viongozi wa mitaa. Kama uko Sinza, nawe tembelea shule hiyo uunganishe jitihada za pamoja. Sina hakika kama nitaweza kwenda mashujaa kesho au kesho kutwa kutokana na majukumu mengine ambayo tayari yako kwenye ratiba, hata hivyo hata nisipokwenda nitaendelea kufuatilia kwa njia nyingine hatua zichukuliwe ikiwa ni sehemu ya wajibu wa kuwawakilisha wananchi na kuisimamia serikali kuu na serikali za mitaa.

  JJ
   
 3. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Nashukuru sana kwa jibu Mh.Mnyika na pole na majukumu,
  Kwa upande wangu nimepanga kwenda hapo kesho then nione jinsi gani nitaweza kusaidia kidogo na kupata taarifa rasmi.
   
 4. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Mnyika ninakushukuru kwa responce yako ya upesi na kueleza kwa umakini nini kiko kwa nani na kipi kifanyike namna gani. Unathibitisha kuwa uko makini.

  Nakutakikia usiku mwema na utendaji mwema wa majukumu yako ya kila siku.
   
 5. p

  politiki JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  ukisikia kitu kinaitwa effective communication ndio hii. hongera sana mnyika kwa kuwa karibu na wananchi wako
   
 6. d

  dada jane JF-Expert Member

  #6
  Mar 22, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli ubungo ina kiongozi wa kisasa. Heri yenu wenzetu mpeni support.
   
 7. M

  Majasho JF-Expert Member

  #7
  Mar 22, 2012
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  mheshimiwa Mbunge, maji ubunge muheshimiwa... ukimaliza bila maji ubungo sikupi tena kura!
   
 8. F

  FredKavishe Verified User

  #8
  Mar 22, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,090
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Maji tatizo lipo toka keenja alipokuwepo anajitahidi sana kufuatilia maji jamani sijaona mbunge kama mnyika hapa dar.
  Katoa laki moja kwa diwani ili washuhulikie barabara ya ubungo inahitajika milioni moja wananchi tunaweza kutoa support kuongezea hizo ela ili barabara ipitike.
   
 9. Dullo

  Dullo JF-Expert Member

  #9
  Mar 22, 2012
  Joined: Oct 24, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama bongo yote ingekuwa na wabunge kama Mnyika, tungesogea mbele japo kwa hatua chache.
   
 10. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #10
  Mar 22, 2012
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Hili la maji ni janga la kitaifa,nategemea kuona mkakati wa kitaifa wa kukabiliana na hili janga badal ya hzi blah! blah! za wiki ya maji ambayo kwangu mimi ni upotezaji wa fedha za umma mchan kweupe..
   
 11. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #11
  Mar 22, 2012
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Majasho, Naendelea kuchukua hatua kama sehemu ya kuwawakilisha wananchi na kuisimamia serikali kuwezesha maendeleo katika sekta ya maji. Naomba tushirikiane pamoja katika kilele cha: JOHN MNYIKA: WIKI YA MADAI YA MAJI, unaweza kuingia hapo ukapata maelezo zaidi na kuchukua hatua kwa upande wako pia. Kuwa wakala wa mabadiliko na maendeleo unayotaka kuyaona.

  JJ
   
Loading...