Mh Mnyika chukua saini yangu na hoja zangu juu ya SSRA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh Mnyika chukua saini yangu na hoja zangu juu ya SSRA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kimilidzo, Aug 5, 2012.

 1. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2012
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Mh Mnyika hongera sana kwa kuamua kuwa sauti ya wanyonge. Mimi ni mmoja wa wanufaika wa mafao ya kujitoa na najivunia kusema bila withdrawal benefit nisingekuwa hapa nilipo kielimu na kimaendeleo binafsi.

  Baada ya kumaliza digrii yangu mwaka 2004 niliajiriwa katika kampuni binafsi kwa miaka mitatu hadi 2007 nilipogundua kuwa kamshiko kangu kule NSSF kwa kujumlisha michango yangu na ya mwajili kwa asilimia 10 each katafikia box 7.5 katikati ya mwaka. Nikaamua kuapply kwa ajili ya Masters degree huku nikijua kabisa ada yote itapatikana kwenye fao langu la kujitoa. Nilifanikiwa kupata admission ya chuo na mwezi wa tisa mwaka 2007 nilijilipua kwa kuacha kazi kabisa, private sector hakuna utaratibu wa kusomesha wafanyakazi au kutoa ruhusa mtu akasome na kumaintain ajira yake, unatakiwa either uache kazi ukasome au uendelee na kazi kwa elimu uliyonayo.

  Kilichonipa kiburi cha kuacha kazi ni fao langu la kujitoa ambapo nilikuwa najua box zangu 7 zinatosha ada ya miaka miwili na gharama za research. Nikiwa na mzigo kidogo niliosave nikaingia chuo na baada ya miezi sita nikaanza safari za NSSF na kupigwa njoo kesho na njoo jumatatu ijayo kwa miezi mitatu, na hata nilipopata mzigo ulikuwa sio box 7.7 kama nilivyojipigia hesabu za mchango kwani jamaa walinikata kama kilo nne hivi na sikuona riba yoyote ikiongeza mafao.

  Nikapiga shule na 2009 nikamaliza Masterz yangu na kurudi kazini kwenye sekta binafsi, industry ileile but muajiri tofauti na nikaanza kazi na mshahara mara 2.5 ya ule wa kabla sijaenda chuo. This time niko PPF na nilijiunga specific kwa vile hakuna kusubiri miezi 6 ili kuchukua fao langu. Toka 2009 hadi sasa nikijipigia hesabu naona nina box 21, baada ya miezi 12 toka leo nitafikisha box 31. Sitaki mkopo wa nyumba wala fao la afya nataka kuchukua mzigo wangu kama ulivyo ili niendeleze biashara zangu na utaratibu wangu wa maisha.

  Mh Mnyika watanzania wengi hawajui kuwa hata kama hii sheria kandamizi ikiendelea kutumika sio kila mfanyakazi aliyechangia atapata pensheni, mfano NSSF ili u qualify kupata pensheni lazima uchangie miezi 180 mfululizo au miaka 15. Mfanyakazi atakayepunguzwa baada ya miaka 13 akiwa na miaka 45 atasubiri kwa miaka 10 kulipwa hela yake ileile aliyochangia bila kupata pensheni na maisha yake yote ya uzeeni yatakuwa mikononi mwake.

  Pia serikali hii dhaifu chini ya rais dhaifu haina huruma na maisha ya baadaye kama inavyotulaghai saizi ili wachukue hela zetu. Hakuna utaratibu wowote wa kurasimisha kazi wanazofanya mamilioni ya watanzania kuwa ajira rasmi ili nao wapate pensheni. Watu kama madereva wa daladala na makondakta wao, madereva taxi, wahudumu wa bar na migahawa ya uswahilini, mama na baba lishe, wafanyakazi wa ndani, wauza maduka ya watu mitaani wote wanafanya kazi za mshahara na wanalipwa kila mwezi mikononi, wengi hawana mikataba na wote hawana pensheni kwa maana hiyo maisha yao ya uzeeni ni utata.

  Serikali hii dhaifi ianze na hawa warasimishiwe ajira zao na kulipiwa mafao na wao kuchangia halafu ndio ije kuleta mchezo mchafu kwenye hela zetu. Pia itueleze wakulima, wasukuma matorori n.k utaratibu wao wa pensheni ukoje? Sio kujifanya inajali maisha yetu ya baadaye lakini kumbe inachojali ni fedha zetu tu. Huu ni udhalimu.

  Mwisho mheshimiwa nijulishe utaratibu wa kutuma electronic signature ili mimi na jamaa zangu tutume saini zetu haraka iwezekanavyo.
   
 2. B

  Bukutonaga JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2012
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 246
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Big Up mkuu serikali dhaifu ni ukweli,Naomba kujua namna ya kutuma electronic signature haraka
   
 3. m

  mwanza_kwetu JF-Expert Member

  #3
  Aug 6, 2012
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 684
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Very nice presentation. Kama umeshiriki ktk mdahalo wa kielectronic wa mnyika basi ana hoja chunu mzima asanate sana mnyika; asante mwaanzisha thread
   
 4. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #4
  Aug 6, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,960
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  Go Mnyika go! Yule gamba anayezunguka migodini awe makini saaaana, la sivyo, . . . . !
   
 5. I

  Iramba Junior Member

  #5
  Aug 6, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu nikutoe wasiwasi yule DOGO si Gamba, I kwon the guy since Minaki Sec as well as at University .. ni mkweli na mzalendo
   
 6. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #6
  Aug 6, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  mkuu mleta mada mi naona kama hao NSSF walikusumbua sana na sijui ni ofisi ya wapi hiyo ....kwa upande wangu nilienda NSSF nikiwa na barua ya kuacha kazi na ile ya admission ya chuo...ilichukua wiki 3 pesa zangu zikatoka...kuna sheria hiyo ipo...kwa hili SSRA kusuzuia mafao ya watu mpake eti wazeeke sijui kustaafu ndio upuuzi unaotakiwa kupingwa kwa nguvu sana..
   
 7. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #7
  Aug 6, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  This time tutalipuana tu, mwenye ufahamu wa electronic signature tusaidieni mapambano!! Na kwa hali hii vijana wengi hawatajitokeza kwenda kukomboa ile sehemu ya ziwa Nyasa kwa sababu za ulafi wa viongozi!
   
Loading...