Bongolander
JF-Expert Member
- Jul 10, 2007
- 5,067
- 2,197
[h=2]wana JF kuna wakati naona huwa tunatumia vibaya uhuru wa kuongea tulio nao. NI mejaribu kuosma hii excerpt kutoka kwenye gazeti la Guardian Online version la tarehe 23 Januari. Mh mbunge John Mnyika anajaribu kutoa maoni kuhusu hali ya uchumi, hebu soma kidogo......
"Serikali ilete mpango wa kunusuru uchumi: Mnyika"[/h]
Mnyika ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, aliitaka Serikali kupeleka mpango wa dharura wa kuimarisha uchumi na kupunguza gharama za maisha kwa wananchi katika vikao vya kamati ya bunge vinavyoendelea kabla ya kuwasilisha katika mkutano wa bunge unaotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu.
Mnyika aliitaka Serikali kuongeza uzalishaji na usambazaji wa vyakula katika soko la ndani pamoja na kuwawezesha wazalishaji wadogo na wa kati katika kilimo na viwanda ili kuongeza mauzo nje ya nchi.
Serikali inapaswa kuharakisha matumizi ya gesi asilia na utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme itekeleze mkakati wa kupunguza manunuzi yake ya nje kwa bidhaa na huduma ambazo zinapatikana nchini, alisema Mnyika.
Hivi kweli anayoongea Mh Mnyika ni realistic? Nani atamsikiliza? Ni kweli serikali yetu kupitia waziri wa fedha Mustafa Mkullo ina uwezo wa kuja na plan ambayo inayoweza kurescue uchumi wetu? NI kweli serikali inaweza kuongeza uzalishaji na usambazaji wa chakula katika soko la ndani? Ni wapi serikali inakozalisha chakula? Au ndio yale ya kuongea jukwaani na kuwataka wananchi walime heka mbilimbili za mahindi bila kujali uwezo wao, hali ya hewa, shughuli zai kiuchumi au hata kama wtu wenyewe wanataka kufanya hivyo au la.
Anaposema serikali "itekeleze mkakati wa kupunguza manunuzi yake ya nje kwa bidhaa na huduma ambazo zinapatikana nchini" ni manunuzi gani yanayofanywa na serikali kwa bidhaa za nje zinazopatikana nchini?
Ukiangalia kwa undani inaonekana kuwa baadhi ya hoja zinatolewa na waheshimiwa wetu bila kuwa makini. Hivi kweli kwa serikali hii tuliyonayo sasa ambayo imeshindwa kuplan hata katika wakati usio emergency, inaweza kuplan nini cha dharura? katika full article mheshimiwa pia ameongelea issue ya umeme, sijui kama kweli anaelewa ni nini kinaendelea serikalini kuhusu issue nzima ya umeme. Serikali imeshindwa ku deal na suala la umeme toka day one, hivi kweli anaamini kuwa serikali hii inaweza kudeal na tatizo la umeme?
My point here is naona mheshimiwa anaongea vitu ambavyo ni unrealistic. Mh Mnyika najua unasoma hii post naamini utaifanyia kazi.