Mh. Missanga, ni chuki binafsi dhidi ya Dr. Ndalichako? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Missanga, ni chuki binafsi dhidi ya Dr. Ndalichako?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Mwanaukweli, Jul 26, 2009.

 1. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2009
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 287
  Trophy Points: 180
  Siku ya Alhamisi tarehe 23/7/2009, Mbunge wa Singida Kusini Mh. Mohamed Misanga (CCM) aliahidi kuwasilisha hoja binafsi ya kuundwa tume huru ya Bunge kuchunguza Baraza la Mitihani na Katibu wake mtendaji. Mara moja ilionekana hata katika wabunge kuna kutofautiana katika azma yake hiyo.

  Iwapo kweli Mh. Missanga anakerwa na utendaji mbaya, basi hatua yake ni ya kizalendo na inalenga kuboresha utendaji wa Taasisi hiyo nyeti. Lakini nahoji mambo kadhaa.

  Kwanza nafahamu kuwa mmoja wa Maafisa waliohamishwa ni Mkwe wa Mh. Missanga, yaani ni mume wa binti yake. Hapa napata mashaka kama kweli Mh. Missanga anatumia nafasi hii kwa kutetea ndugu yake binafsi katika wadhifa wake kama mbunge au kweli anakerwa na utendaji mbaya.

  Hivi Mh. Missanga kuhamishwa kutoka sehemu moja ya kazi kwenda nyingine ni jambo la ajabu??? Au kwa kuwa na mkwe yumo? Na je Dr. Ndalichako hana bodi inayosimamia kazi yake? Na anatoa maamuzi bila kushirikisha bodi?

  Binafsi namfahamu Dr. Ndalichako tangu akiwa Lecturer UDSM (mwalimu wangu). Ana sifa zote za kuliongoza vema Baraza la Mitihani, na mpaka sasa anafanya vizuri. Mh. Missanga ukiweza kumhusisha yeye binafsi na ufisadi wa aina yoyote, utakuwa umeleta hoja inayoweza kutushawishi na sisi.

  Nashawishika kusema kuwa kuna hujuma zinafanyika dhidi yake na watu ambao wanamchukia au kwa kuwa walihamishwa au kwa kuwa wanakwamishwa katika azma ya kufanikiwa bila jasho kwa kufutiwa mitihani, shule kufungiwa n.k. Because she is very strict and tough and does not buy in to any corrupt temptations. Prove me otherwise if you have evidence plz.

  Wateja wa mitihani ivujayo si watu wanyonge, ni wenye pesa na wenye madaraka makubwa. Hawa wanaweza kutengeneza mazingira ya kumwondoa mtu yeyote aliye kikwazo katika kutimiza malengo yao, mtindo unaotumiwa na genge la MAFIA la ITALIA. Nashawishika kuwa Mh. Missanga umo mbioni katika kutimiza azma hiyo. All the best.

  Wabunge na wengine kuweni macho na hoja ambazo zinaletwa kwa sababu za chuki binafsi.

  Ni vema kujadili issues, na si kupersonalize issues.
   
  Last edited: Jul 26, 2009
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Jul 26, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Good observation! Kwa ujumla viongozi wetu ukiona wanakomalia issue ujue kuna maslahi binafsi ndani yake! Unakumbuka issue ya Mwakyembe ya umeme wa nguvu ya upepo ilivyokuwa na link na Tume ya Richmond iliyoongozwa na yeye?
   
 3. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2009
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 287
  Trophy Points: 180
  Hii si mara ya kwanza kwa Mh. Missanga kuleta issue ya Dr. Ndalichako bungeni. Mara ya kwanza alihoji kuwa waliohamishwa wameonewa. Waziri alishangaa na kuhoji kuwa mtu ambaye amehamishwa kutoka Taasisi moja kwenda idara/taasisi nyingine ndani ya wizara ileile bila kushuswa cheo wala mshahara na analalamika analeta hisia kuwa kuna biashara fulani ambayo ataikosa huko alikohamishiwa. Biashara gani hiyo?

  Tunangoja tuone hoja binafsi Mh. Missanga.
   
 4. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2009
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 287
  Trophy Points: 180
  This time Naibu Spika Mh. Anna Makinda alikerwa na akaangalisha kuhusu personalization of issues.
   
 5. Zilla The G

  Zilla The G JF-Expert Member

  #5
  May 6, 2017
  Joined: Dec 26, 2014
  Messages: 468
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 60
  sawa!
   
Loading...