Mh. Membe yuko wapi?

Indume Yene

Platinum Member
Mar 17, 2008
2,950
711
Wadau nimekutana na hii picha mtandaoni ikionyesha ugeni aliokuwa nao JK kule New York. Mgeni wa JK alikuwa kiongozi wa waasi wa Libya ambaye kwa sasa ndiye Rais wa serikali ya mpito (Mustafa abdel-Jalil). Tunakumbuka kasheshe ya Membe na balozi wa Libya nchini Tanzania. Sasa Prezidaa kaonana na kiongozi wa huyo balozi, lakini Mh. Membe haonekani kwenye hayo mazungumzo zaidi ya JK na balozi Ombeni. Membe kaona aibu na kuingia mitini.Angalia mwenyewe.



libya4.jpg
 
membe ni kati ya viongozi wasiopima nn wanaongea na nafasi zao, unapokuwa mwanadiplomasia hupaswi kuwa mnafikinafiki na unayetoa kauli zisizo na mwendelezo, nakumbuka kauli yake kuwa 'hatuwezi kukubali nchi kuongozwa na mchesha disco, dj' akimaanisha rajoelina wakati wa sakata kati yake na ravalomanana huko madagascar, na kauli yake ya juzi kuwa 'hatuwezi kuwatambua watu wanaoongoza ndani ya pick ups' akihusisha namna wakomboaji wa libya walivyokuwa wakitumia pick ups katika harakati azo za kumwondoa qadhafi.

Membe ni lazima aoen aibu kuu
 
Hili ni tatizo kubwa kwa diplomasia yetu, mwanadiplomasia hata kama amechukia hawezi kuwa sawa na mhandisi au mkulima, lugha anayoitumia ni tofauti na hawa niliowatja na hata anapotoka nje ya ukumbi kutokana na kutoelewana hawezi kumaliza maneno yote kama mtu aliyepewa talaka. mahusiano ya baina ya mataifa yana lugha zake.

Kwenye hii picha, ni kuwa, JK kasahihisha makosa ya aliyemteua
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom