Mh mbunge habibu Mnyaa-CUF-kasema ukweli

bartazary bon

Member
May 19, 2011
11
1
wana JM-jana mh huyu alisema kuna hoteli moja imeajili wageni wengi ktk nafasi kadhaa ambazo wazawa wana uwezo na elimu ya kuzifanya.Lakini wazawa hawakuzingatiwa.

Nami ningependa kuwaeleza ya kuwa,hali hii si kwenye ma hoteli tu,nenda kwenye makampuni makubwa ya uingizaji madawa na kwenye viwanda,huko ndo balaa.Ni rai yangu mamlaka husika zilifanyie kazi,

Makampuni makubwa kama salama pharmaceutical,shelys pharmaceutical,metro pharma,tata pharma.ipca pharma,philips pharma na mengine mengi tu-utawakuta wahindi na mabegi yao kwenye mahospitali na ma pharmacy wakitafuta masolo. NAWAKILISHA
 
Hapa kuna tatizo la kuthamini wageni kuliko wazawa. Mamlaka husika hazijalifanyia kazi suala hili ipasavyo na ni katika kila nyanja ya maisha. Si unasikia wabongo tunavyobaguliwa hoteli za kitalii? Migodini ndiyo basi tena! Pamoja na hayo, elimu yetu na hasa issue ya customer care tunazidiwa na wageni, hilo halina ubishi. Katika soko la ushindani lazima sana kuboresha elimu yetu iendane na wakati na siyo kulalamika tu. Kwa viwango vya elimu hii ya Saint Kayumba, tutapigwa fimbo mpaka baaasi!
 
Elimu ni muhimu sana kwenye ajira lakini pia kuna swala la uwajibikaji, ukweli watanzania tunapenda sana kufanya kazi kienyeji, hatuko serious na kazi zetu, na hii itaendelea kutucost hasa tunapoelekea kwenye soko la pamoja la ajira EA. Jambo la pilli ni enforcement ya sheria zetu, hawa jamaa ndio hawawajibiki kabisa.
 
Elimu ni muhimu sana kwenye ajira lakini pia kuna swala la uwajibikaji, ukweli watanzania tunapenda sana kufanya kazi kienyeji, hatuko serious na kazi zetu, na hii itaendelea kutucost hasa tunapoelekea kwenye soko la pamoja la ajira EA. Jambo la pilli ni enforcement ya sheria zetu, hawa jamaa ndio hawawajibiki kabisa.
Ni kweli kabisa. Hata mimi ningekuwa na kampuni binafsi, kuajiri mtz katika nafasi zisizohitaji longolongo, ningejiuliza mara mbili. Hata kazi ya kufungua gate inatushinda.
 
Na sisi Watanzania tujifunze kudeliver tunapopewa nafasi...kwani tumekuwa mabingwa wa kulalamika na kupiga porojo tu....Mfano mzuri La Kairo hotel mwanza ina wafanyakazi weengi wakenya na watanzania, ukihudumiwa na mkenya hata kama chakula kimechelewa bado kesho yake utarudi....lakini wa Watz kweli hutatamani tena kwenda hapo....
 
Tatizo kubwa ndugu zangu ni uwajibikaji na kujitoa, hata sheria zingerekebishwaje tatizo letu haliwezi kwisha endapo hatutabadili mitazamo, utendaji kazi wa watanzania wengi ungekuwa unafanyiwa tathmini tungebaini tija ni chini kulinganisha na wageni na hasa wafanyakazi wa sekta ya umma
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom