Mh Mbowe na Hoja binafsi ya salamu mpya kitaifa inayoshiriksha makundi yote ya dini, vyama na rika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh Mbowe na Hoja binafsi ya salamu mpya kitaifa inayoshiriksha makundi yote ya dini, vyama na rika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mikael P Aweda, Jul 3, 2012.

 1. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #1
  Jul 3, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mwasisi wa Chadema, M/kiti wa Chadema Taifa, na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni heshima yako. Leo naomba nikusumbue kidogo kuhusu salamu mpya ya kitaifa.
  Hoja yangu;
  Nchi yetu haina salamu rasmi ya kitaifa inayoweza kutumiwa ktk mikutano ya hadhara inayoshirikisha wananchi wa makundi yote (rika, vyama na dini)
  Kuna salamu za makundi ya kijamii kama vyama kisiasa, Makundi ya kidini, rika nk, lakini hatuna salamu za kitaifa. Nitafafanua kwa kwa mfano;
  Ukiwa kama M/kiti wa tume ya katiba Ukisimama mbele ya mkutano mkubwa wa hadhara wa watanzania wa mkundi yote, Jaji Joseph S. Warioba atatumia salamu gani kati salamu zilizoko hapo chini au atatumia zote kwa kuwa makundi yote yatawakilishwa ktk mikutano yake?

  [TABLE="class: MsoNormalTable, width: 497"]
  [TR]
  [TD="width: 22, bgcolor: transparent"]
  [/TD]
  [TD="width: 129, bgcolor: transparent"]Kikundi
  [/TD]
  [TD="width: 112, bgcolor: transparent"]mwanzisha salamu
  [/TD]
  [TD="width: 152, bgcolor: transparent"]Mpokea salamu
  [/TD]
  [TD="width: 249, bgcolor: transparent"]Maoni yangu
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 22, bgcolor: transparent"]1
  [/TD]
  [TD="width: 129, bgcolor: transparent"]CCM
  [/TD]
  [TD="width: 112, bgcolor: transparent"]CCM HOYEE
  [/TD]
  [TD="width: 152, bgcolor: transparent"]HOYEE
  [/TD]
  [TD="width: 249, bgcolor: transparent"]Kwa wanaccm tu.
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 22, bgcolor: transparent"]2
  [/TD]
  [TD="width: 129, bgcolor: transparent"]Chadema
  [/TD]
  [TD="width: 112, bgcolor: transparent"]Chadema
  [/TD]
  [TD="width: 152, bgcolor: transparent"]Vema
  [/TD]
  [TD="width: 249, bgcolor: transparent"]Wanacdm tu
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 22, bgcolor: transparent"]3
  [/TD]
  [TD="width: 129, bgcolor: transparent"]CUF
  [/TD]
  [TD="width: 112, bgcolor: transparent"]Haki
  [/TD]
  [TD="width: 152, bgcolor: transparent"]Kwa wote
  [/TD]
  [TD="width: 249, bgcolor: transparent"]Wanacuf tu.
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 22, bgcolor: transparent"]4
  [/TD]
  [TD="width: 129, bgcolor: transparent"]Waislamu
  [/TD]
  [TD="width: 112, bgcolor: transparent"]Asalaam Aleikum
  [/TD]
  [TD="width: 152, bgcolor: transparent"]Dini ya kiislamu
  [/TD]
  [TD="width: 249, bgcolor: transparent"] Makundi ya waislamu zaidi
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 22, bgcolor: transparent"]4
  [/TD]
  [TD="width: 129, bgcolor: transparent"]Wakristo
  [/TD]
  [TD="width: 112, bgcolor: transparent"]Bwana asifiwe, tumsifu yesu kristo, shalom
  [/TD]
  [TD="width: 152, bgcolor: transparent"]Amin, tumsifu yesu kristo, shalom
  [/TD]
  [TD="width: 249, bgcolor: transparent"]Hii ni za makundi ndani ya dini ya kikristo.
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 22, bgcolor: transparent"]5
  [/TD]
  [TD="width: 129, bgcolor: transparent"]Wadogo kwa wazima
  [/TD]
  [TD="width: 112, bgcolor: transparent"]Shikamoo
  [/TD]
  [TD="width: 152, bgcolor: transparent"]Marahaba.
  [/TD]
  [TD="width: 249, bgcolor: transparent"]Ina mipaka ya rika
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 22, bgcolor: transparent"]6
  [/TD]
  [TD="width: 129, bgcolor: transparent"]Mkubwa kwa mdogo
  [/TD]
  [TD="width: 112, bgcolor: transparent"]Hamjambo
  [/TD]
  [TD="width: 152, bgcolor: transparent"]Hatujambo Shikamoo
  [/TD]
  [TD="width: 249, bgcolor: transparent"]Ina mipaka ya rika
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 22, bgcolor: transparent"]7
  [/TD]
  [TD="width: 129, bgcolor: transparent"]Wenye umri sawa
  [/TD]
  [TD="width: 112, bgcolor: transparent"]Habari
  [/TD]
  [TD="width: 152, bgcolor: transparent"]Nzuri
  [/TD]
  [TD="width: 249, bgcolor: transparent"]Ina mipaka ya rika
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 22, bgcolor: transparent"]8
  [/TD]
  [TD="width: 129, bgcolor: transparent"]Vijana kwa vijana
  [/TD]
  [TD="width: 112, bgcolor: transparent"]Mambo
  [/TD]
  [TD="width: 152, bgcolor: transparent"]Poa
  [/TD]
  [TD="width: 249, bgcolor: transparent"]Ina mipaka ya rika
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  A)1 – 3 hapo juu ni za vyama, Warioba hajaenda kwa niaba ya chama cho chote.
  B)3 – 4 ni inawakilisha makundi ya kidini – Hakuna dini iliyomtuma
  C) 5- 8 ni makundi ya rika – yote yatakuwepo ktk mikutano. Je, anaweza kusema Shikamoni, habari, mambo vipi! Hamjambo nk.
  Kwa maoni yangu hakuna salamu yo yote itakayomfaa Jaji warioba kati zote hizo zilizopo hapo juu. Vinginevyo, atalazimika kutumia zote - upotevu wa muda.
  Ndiyo maana Rais mstaafu ndugu B.W.Mkapa nimemsikia mara kadhaa akiwa madarakani akizitumia salamu zote mpaka inachosha. Salam aleikum, bwana asifiwe, Tumsifu yesu kristo, vijana mambo! Wakubwa shikamoni, wanarika wenzangu habari nk.
  Nimesikia pia John Mnyika mbunge wa Ubungo akijaribu mara nyingi kushirikisha makundi yote kama afanyavyo mzee Mkapa.

  Jambo hili pia naona aliliona Mh Edward Ngoyai Lowasa pale alipoanzisha salamu za
  Hongera kwa kazi sikumbuki alipendekeza nini iwe mwitikio wake. Ila kabla hajaachia ngazi nimemsikia akilishikia bango.

  Mapendekezo yangu
  .
  Kwa kuwa makundi ya wanasisa na wananchi wote wanapenda amani, na
  Kwa kuwa makundi ya dini za kikristo na kiislamu ndani ya salamu zao kuna neno amani, mfano wakristo (shalom = amani) waislamu ( Salaam aleikum = inahusisha amani)
  Hivyo, basi napendekeza salamu za Taifa letu ktk mikutano inayohusisha watz wote bila kujali makundi ya kijami
  iwe Nawatakia Amani, kiitikio cha wengi Ahsante nawe pia. ili tumrahisishie mzee Warioba kazi yake.Salamu hizi zitakuwa zinalenga kudumisha amani na umoja ktk nchi yetu.
  Ni kwa sababu hii nimeamua kumtumia Kamanda wa Ukweli Freeman Aikaeli Mbowe apeleke hoja binafsi bungeni ili wabunge waijadili na kuipitisha. Si lazima wakubaliane na pendekezo langu, jambo la muhimu ni wao kuja na Salamu za kitaifa itakayowaunganisha watz wote. Najua tume ya katiba imeanza kazi ila mimi sidhani kama jambo hili linahitaji kusubiri katiba mpya. Vazi la Taifa limechukua miaka mingi, hata salamu za kitaifa linatushinda?
  Ikumbukwe kuwa baadhi ya wanasiasa wanaotumia salamu hizi wanaposahau kundi mojawapo kutokana na uwepo wa makundi mengi labda kwa bahati mbaya inaleta hisia za ubaguzi kwa kundi lilisahauliwa. Jambo hili si jema.
  Mwisho naomba nikupongeze Mh Mbowe kwa jinsi unavyoongoza chadema kwa mafanikio makubwa na ubunifu wa hali ya juu ikiwepo kauli mbio zenye kuleta tija ya M4C na vua gamba, vaa gwanda. Naamini hoja hii haitakataliwa na speaker.
  Great thinkers naomba maoni yenu. Mbowe kazi kwako.

   
 2. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,621
  Likes Received: 2,042
  Trophy Points: 280
  Hizio ni salaamu za kutiana hamasa tu pia katika shughuli zote za kiserikali hakuna salaam ya shikamoo kikubwa ni habari za saa hizi mabibi na mabwana hayo mambo mengine ni manjonjo tu ndugu Mikael P Aweda
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Aweda, Umedhamiria tudiscuss hii kitu katikati ya Mazongezonge yote haya yaliyotuzunguka?
   
 4. s

  step Senior Member

  #4
  Jul 3, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 190
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  I concur with you. Tumetingwa na mambo mengi jambo la kwanza ni kudhibiti wale wanaotaka kutugawa ili watutawale milele hayo mengine yatafata.
   
 5. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,621
  Likes Received: 2,042
  Trophy Points: 280
  Ni kweli mkuu kinachotakiwa ni kupambana kama watu hawasikii tunaingia humu kutoa dukuduku letu mpaka kielewe
   
 6. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #6
  Jul 3, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Inawezekana timining siyo nzuri sana, hata hivyo hoja ina tija kwa taifa. I though we can discuss both issues.
   
 7. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #7
  Jul 3, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Nashukuru, je watoto nao tunawagawa ktk makundi la mabibi na mabwana?
   
 8. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #8
  Jul 3, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  what is this?
   
 9. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #9
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,621
  Likes Received: 2,042
  Trophy Points: 280
  Kama watakuwa ni 2% katika mkutano itabidi waingie kwenye mkumbo kwa kuwa mwonekano wao utakuwa negligible lakini sidhani kama mikutano ya kukusanya maoni itakuwa ina wajumbe mfano idadi sawa kati ya wakubwa na watoto kwa vyovyote watapita kwa wanafunzi wa vyuo ambao karibu wote ni watu wazima (above 18 years hawa ni mabibi na mabwana), wanaweza kupita mashuleni hawa wengi ni below 18 years pia watapita katika makundi mbalimbali. kiukweli ukitaka upate maoni mazuri itabidi upite katika makundi tofautitofauti katika jamii ili upate nondo za uhakika maana ukichanganya watoto, wanafunzi, wasomi na n.k kuna uwezekano wa watu wengine kufuata mkumbo wa hoja za wengine na ndio maana tunapokuwa shule unaweza soma topic moja O-level, ukaikuta A-level na ukaikuta chuo lakini katika level zote hizo inakuwa inakautofauti hivyo hata katika kuchangia hoja watu tumetofautiana hoja kutokana na uzoefu na elimu wa kujua mambo na vitu vingine vingi. Akienda kwa watoto ambao wengi ni watoto atasalimia hamjambo vijana
   
 10. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #10
  Jul 3, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Rekebisha kwanza hili, MBOWE siyo mwasisi wa CHADEMA. Hata tofauti za ZITTO KABWE au kwa vile mwasisi wake ni BABA yake? Mkuu naona wewe kama uko usingizini, vyama vyennyewe hivi msingi wake ni udini, ukabila na ukanda, sasa wataachaje kuenzi misingi hiyo?
   
 11. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #11
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,269
  Likes Received: 655
  Trophy Points: 280
  Umuofia kwenu
   
 12. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #12
  Jul 3, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mbowe ni miongoni mwa waasisi wa Chadema, kwa taarifa zilizopo. Yeye alikuwa mwasisi mdogo kuliko wote kwa mujibu wa maelezo ya waasisi yaliyosomwa siku ya msiba wa BOB MAKANI.
   
 13. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #13
  Jul 3, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mods,
  Paw nakushukuru kwa kuondoa comments za kijinga kabisa ambazo hazifai kuwepo JF - the home of great thinkers.
   
Loading...