Mh. Mbowe muulize maswali haya waziri mkuu pinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Mbowe muulize maswali haya waziri mkuu pinda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sisala, Jul 3, 2012.

 1. s

  sisala Member

  #1
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 14, 2012
  Messages: 74
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  MH. MBOWE MUULIZE MASWALI HAYA WAZIRI MKUU SIKU YA ALHAMISIKIPINDI CHA MASWALI YA PAPO KWA PAPO TOKA KWA WABUNGE.
  1. Kwakuwa Manyanya ni mkuu wa mkoa, kwa hiyo sualaalilo litoa bungeni kuwa Chadema wanahusika na mgomo wa madaktari ni kauli yaserikali, je serikali inasemaje kuhusu hilo.
  2. Je magwanda waliovaa watesi wa Dr. Ulimbokayanafananaje na yale ya Chadema wakati nguo hiyo huweza valiwa na kila mtu, sababumagwanda hayana nembo ya Chadema.
  3. Manyanya anaposema Mungu amemwepusha Dr.Ulimboka na mauaji ya Watanzania wasio na hatia ndiyo maana kafanyiwa vitendovya kinyama kiasi hicho, je serikali inaafiki unyama huo? Je Manyanya anaonakitendo hicho ni sahihi ili kuwafanya madaktari warudi kazini?
  4. Nchemba anaposema Chadema hawana uchungu na mh.Serasini kwa hiyo hawana haki ya kuwa na uchungu na Dr. ulimboka, je Dr.Ulimboka kapata ajali?, ana uhakika gani wa kiintelijensia kuwa Chadema hawahangaiki na matatizo yaliyomfika mh.Serasini?

  Tafadhali Mh. Mbowe muulize Waziri Mkuu.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  PM atalia akiulizwa maswali hayo Mkuu.
  Lakini kimsingi Manyanya ameidhalilisha serikali kwa utumbo aliomwaga jana. Ndio shida ya vyeo visivyo na vetting.
   
 3. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,818
  Likes Received: 36,917
  Trophy Points: 280
  Alafu its so simple kumdondosha mbunge ambaye pia ni mkuu wa wilaya/mkoa, case study: monica mbega iringa.
  Ilikua so easy kumdondosha kama kupapasa maiti vile.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 4. kinya

  kinya JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 483
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Mkuu hivi manyanya si mbunge wa dezo?nikimaanisha hanajimbo kwa hiyo ukitaka kumdondosha inabidi umdondoshe aliempatia fadhila au mnasemaje wadau
   
 5. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Maamuzi magumu yanatakiwa yafanyike dhidi ya Manyanya!
   
 6. D

  DCM Senior Member

  #6
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 165
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Hayo ndio matokeo ya vyeo pasipo hata kuangalia upeo wa mtu,sasa hivi ni ilimradi tu kujuana utapata cheo!Nashangaa hata kuona baada ya Dr kupigwa waziri wa mambo ya ndani na kova walitofautiana kimaelezo,ina maana hwana hata mawasiliano kwanza,kazi ni kukurupuka tu!
  Ni aibu kwani siasa imeingia hata ktk utendaji wa mambo ambayo ni nyeti,aim ni kudanganya watanzania waliowengi waichukie chadema,ila mwisho wa siku ukweli utajulikana tu
   
 7. U

  Uswe JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hapo kwenye red, tukiiweka hivi inakuwaje!

  3. Manyanya amenukuliwa akisema Mungu amemwepusha Dr.Ulimboka na mauaji ya Watanzania wasio na hatia ndiyo maana kafanyiwa vitendovya kinyama kiasi hicho, Je serikali inaamini kutekwa na kuteswa kwa Dr ulimboka kumesaidia kuokoa mauji ya watanzania wasio na hatia kwa sababu madaktari sasa wataogopa kugoma?

   
 8. r

  reformer JF-Expert Member

  #8
  Jul 3, 2012
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 387
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Utamouna Spika kasimama na kusema swala hilo la Dokita Ulimboko na mgomo wa Modokita lipo mahakamani..hairusiwi kuliongelea bungeni. Period.
   
 9. kiraia

  kiraia JF Gold Member

  #9
  Jul 3, 2012
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  Pia mheshimiwa Mbowe Muulize Waziri Mkuu swali hili

  • Nini Msimamo wa serikali ya Tanzania kuhusu meli za Irani kubeba Bendera ya Tanzania?
   
 10. U

  Uswe JF-Expert Member

  #10
  Jul 3, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  a million dollar question!
   
 11. r

  reformer JF-Expert Member

  #11
  Jul 3, 2012
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 387
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Atajibu..bado hatujapata taarifa rasmi na sisi tumesikia tu. Serikali bado inalifanyia uchunguzi wa kina jambo hili kabla ya kulitolea maelezo na msimamo wake.
  Pwa pwa pwa (Makofi mengi toka kwa magamba)
   
 12. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #12
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Kama Stell Manyanya anafikiri kwamba Mungu ndiye aliyehusika na utekaji na uteswaji wa Dr. Ulimboka huo siyo Mungu wetu tunayemuamni, huyu ni Mungu wa kina Stella na CCM yake ndiyo waliomtesa Dr. Ulimboka. Laani ikupate Stella Manyanya kumhusisha Mungu na u-mafia wenu CCM. Hiyo ni dhambi kubwa itawatafuna milele. Unashangilia mtoto wa mwenzako kuminywa sehemu za siri, kung'olewa meno na kucha, God forbid sasa ninaanza kuelewa alichofanya Mamwindu dhidi Dr. Kreluu
   
 13. T

  Talklicious Member

  #13
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sisala Naomba niongezee hili ila itabidi likae baada ya swali la 2.
  Kwasababu Manyanya ametaja wazi waliomteka Dr Uli walivaa magandwa na hadi sasa hamna aliyekamatwa kuisaidia serikali, kwanini wasimchukue yeye ili walau akatoe maelezo yanayoweza kukamatwa kwa washukiwa?
  Mmmmh kinachonishangaza hapa ni kwamba inaelekea manyanya pia alikuwa eneo la tukio hadi kufahamu waliomteka walivaa nguo gani, ilikuwaje alishindwa kuripoti muda wote huo?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #14
  Jul 3, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  sisala Tujiulize pia kama kweli alikuwa anatumiwa kuzuia watanzania walio wengi wasitibiwe ni sahihi?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #15
  Jul 3, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  alikuwa anaogopa Magwanda wasimfuate baada ya kutoka kwa Uli ndiyo maana hakutokea.
   
 16. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #16
  Jul 3, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Inawezekana Mbowe anajua ukweli wa mambo ndiyo maana amekaa kimya.
   
 17. s

  sisala Member

  #17
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 14, 2012
  Messages: 74
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  hivi manyanya ana account humu JF ili aweze kusema chochote kuhusiana na kauli yake ya jana bungeni?, kama kuna member yeyote anayejjua account yake kwenye JF naomba apost ili tubonge nae.
   
 18. a

  andrews JF-Expert Member

  #18
  Jul 3, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ​msiumize vichwa chama dhaifu huzaa serikali dhaifu kwa kupendekeza rais dhaifu ndio maana tunapata waziri mkuu wa liwalo naliwe
   
Loading...